KENYA Mkurugenzi wa IEBC Ezra Chiloba amechukua likizo ya wiki 3 kwenda mapumziko

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Afisa mkuu wa tume ya uchaguzi Kenya Ezra Chiloba ajiondoa

Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo.

HAYO YOTE - SERVER, SERVER, SEVER, SERVER KWA NINI HAICHUNGUZWI

=====

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini Kenya Ezra Chiloba anatarajiwa kuchukuwa likizo ya wiki tatu na hatoshiriki katika uchaguzi wa marejeo wa Alhamisi kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.

Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo.

Kulingana na gazeti hilo afisa huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu, huku mgombea wa urais wa muungano huo Raila Odinga akiitisha maandamano ya kumlazimisha kuondoka pamoja na maafisa wengine ikiwatuhumu kwa kusimamia vibaya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.

Matokeo ya uchaguzi huo hatahivyo yalifutiliwa mbali na mahakama ya juu ambayo iliamua kwamba haukufanyika kulingana na sheria.

Kulingana na Daily Nation Bwana Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula Chebukati kutaka maafisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali kung'atuka.

Mahakama ya juu ilisema kuwa haikupata ushahidi kuhusu makosa yaliofanywa na maafisa lakini wanasiasa wamelalamika na kuishutumu tume hiyo kwa kujaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo mbali na wizi wa kura.

Uamuzi huo wa kuchukua likizo ulijadiliwa na mwenyekiti na bwana Chiloba anaamini kwamba kutokuwepo kwake hakutaathiri maandalizi ya tume hiyo kusimamia uchaguzi ulio huru na haki.

-BBC
 
Jambo jema sana

Jambo Jema

Ila raila anataka kuichafua tu nchi
 
KENYA Mkurugenzi wa IEBC Ezra Chiloba amechukua likizo ya wiki 3 kwenda mapumziko.

Daah naona Uchaguzi Unlikely kufanyika.

=====

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini Kenya Ezra Chiloba anatarajiwa kuchukuwa likizo ya wiki tatu na hatoshiriki katika uchaguzi wa marejeo wa Alhamisi kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.

Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo.

Kulingana na gazeti hilo afisa huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu, huku mgombea wa urais wa muungano huo Raila Odinga akiitisha maandamano ya kumlazimisha kuondoka pamoja na maafisa wengine ikiwatuhumu kwa kusimamia vibaya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.

Matokeo ya uchaguzi huo hatahivyo yalifutiliwa mbali na mahakama ya juu ambayo iliamua kwamba haukufanyika kulingana na sheria.

Kulingana na Daily Nation Bwana Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula Chebukati kutaka maafisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali kung'atuka.

Mahakama ya juu ilisema kuwa haikupata ushahidi kuhusu makosa yaliofanywa na maafisa lakini wanasiasa wamelalamika na kuishutumu tume hiyo kwa kujaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo mbali na wizi wa kura.

Uamuzi huo wa kuchukua likizo ulijadiliwa na mwenyekiti na bwana Chiloba anaamini kwamba kutokuwepo kwake hakutaathiri maandalizi ya tume hiyo kusimamia uchaguzi ulio huru na haki.

-BBC
 
Tume ya Kenye na Mahakama wanataka Raila Odinga achukue nchi, nafikiri hivi, na Odinga anahamu ya kwenda kumalizia uzee wake The Hague...
 
RAO will have no ground to complain should the results turn out against his expectation

Yes however the principles of justices and trueth to be practical not theoretical

Those failed to run the presidential election previously must be eradicate completely to ensure faithful re-election is done.
 
Acha hizo wewe, na ukikuta mutu inaitwa jesus utasema ule uko kwa bible?

Acha urongo.
Mimi niko najua kuwa Uhuru amewahi kubali kushindwa kwenye ballot box, ina maana ana weledi ya kutosha.
Hapendagi ma citizens waingie kwa vurugu.

Raila hataki kushindwa ni aje mutu hii?

Wakenya kwisa kumkataa, mahakama imempa nafasi ajaribu bahati yake tena sasa badala ya kuwashawishi voters yeye anapambana na members wa tume inayoitwa ni huru! Anaishinikiza serikali wakati yu ajua muundo wa tume husika ni huru kabisa.

UHUSIANO YAKE NA MIGUFULI YA TANSANIA IMEMLETEA HASARA KUBWA VILE WAKENYA WANAONA BULDOZA IKIVUNJAVUNJA MAJUMBA YA WATIZII.
 
Afisa mkuu wa tume ya uchaguzi Kenya Ezra Chiloba ajiondoa

Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo.

HAYO YOTE --SERVER,SERVER,SEVER,SERVER KWA NINI HAICHUNGUZWI,ingejulika nani alishinda na hata wasinge haribu pesa.
 
Mimi niko najua kuwa Uhuru amewahi kubali kushindwa kwenye ballot box, ina maana ana weledi ya kutosha.
Hapendagi ma citizens waingie kwa vurugu.

Raila hataki kushindwa ni aje mutu hii?

Wakenya kwisa kumkataa, mahakama imempa nafasi ajaribu bahati yake tena sasa badala ya kuwashawishi voters yeye anapambana na members wa tume inayoitwa ni huru! Anaishinikiza serikali wakati yu ajua muundo wa tume husika ni huru kabisa.

UHUSIANO YAKE NA MIGUFULI YA TANSANIA IMEMLETEA HASARA KUBWA VILE WAKENYA WANAONA BULDOZA IKIVUNJAVUNJA MAJUMBA YA WATIZII.
Bulldozer lazima atakuwa amekutenda vibaya sana wewe, bila Shaka u mmojawapo wa waliotumbuliwa sababu ya kukosa cheti cha shule.
 
Makinikia tu wala hakuna sababu ingine, labda saana saana kugeuza kanuni na kufanya wapinzani ni maadui wa kupiga bunduki.
 
Unless and untill the IEBC is disbanded and hhe servers opened, RAO is holding both the moral and political highground. n
Uhuruto have an ace up their sleeves, you must know a barking dog never bites...most noisy are non other than Raila Amollo as retirement beckons.
 
Kukubali maneno sio kuwa inferior. Hapana. Nadhani Kenyatta akubali tu hiyo tume ivunjike na hizo tarehe zisogee mbele. Iundwe tume huru ingine ambayo itatajwa na Nasa na Jubilee. Baada ya hapo, tuone hao mafahali 2 ikiingia kwa votes. Ile inatajwa ndio mshindi ishinde kwa votes ya wakenya.
 
ivunjwe kisa raila?! bas hiyo nchi itakuwa ya vituko
 
Back
Top Bottom