Kenya na India Zaipiku Tanzania Kwa Mauzo ya Tanzanite

Kenya na India Zaipiku Tanzania Kwa Mauzo ya Tanzanite

watu wengi hamuelewi hii biashara inavyofanyika mimi binafsi nafanya hii biashara kusema mawe yanapitishwa kwa magendo si kweli sbb serikali wala haikatazi kusafiri haya mawe yakiwa yamefanyiwa carting mi husafirisha tena sio peke yangu na watanzania we zangu kibao unalipia tu wizarani na hamna hata rushwa yoyote .wahindi ndio ni wanunuzi wa kubwa sana mtu anakuja kununua mawe ya 1ml dolla wewe utakataa kumuuzia maana wanauziwa na watanzania tu wanaochimba.na kunakitu watu hawajui kuhusu wahindi niwatu wanaojua kucontro soko yani na maanisha kwa mlaji wa mwisho huko wamebana price kiasi kwamba unaamua tu kumuuzia yeye ukiangalia bei ya rejareja nje tofauti sio kubwa sana na hapa yeye anamjua mpaka broker wakumpelekea beyoncé we utamjulia wapi? Ndio maana wao wanaonekana wanauza zaidi kuliko hapa kinachozungumzwa ni soko la nje maana mawe yote ya nanunuliwa hapa.ngoja nitolee mfano mozambique wana contro ruby pale ni watanzania na wachimbaji wengine pia walitoka tanzania tena watu wa kawaida tunawauzia wa thailand huyo mozambique hata m thai hamjua

..kwa jinsi ulivyoelezea ni kama vile hatuna ujanja na tukubaliane na hali halisi....hii haikubaliki...kumbuka we monopolize this resource...
 
Mkiambiwa serikali ya ccm imejinyea mnabisha. Wako wapi sasa wanalumufumba wanaojidai kutetea mafisadi? Wako wap? Au uzi hausomeki tuwatafutie miwani. Aibu sana.
 
Watu wengi hamuelewi hii biashara inavyofanyika mimi binafsi nafanya hii biashara kusema mawe yanapitishwa kwa magendo si kweli sbb serikali wala haikatazi kusafiri haya mawe yakiwa yamefanyiwa carting mi husafirisha tena sio peke yangu na watanzania we zangu kibao unalipia tu wizarani na hamna hata rushwa yoyote .wahindi ndio ni wanunuzi wa kubwa sana mtu anakuja kununua mawe ya 1ml dolla wewe utakataa kumuuzia maana wanauziwa na watanzania tu wanaochimba.na kunakitu watu hawajui kuhusu wahindi niwatu wanaojua kucontro soko yani na maanisha kwa mlaji wa mwisho huko wamebana price kiasi kwamba unaamua tu kumuuzia yeye ukiangalia bei ya rejareja nje tofauti sio kubwa sana na hapa yeye anamjua mpaka broker wakumpelekea Beyoncé we utamjulia wapi? Ndio maana wao wanaonekana wanauza zaidi kuliko hapa kinachozungumzwa ni soko la nje maana mawe yote ya nanunuliwa hapa.ngoja nitolee mfano Mozambique wana contro ruby pale ni watanzania na wachimbaji wengine pia walitoka tanzania tena watu wa kawaida tunawauzia wa Thailand huyo Mozambique hata m Thai hamjua

Bora hapa nimeelewa.
 
Usianze kulaumu bila ktafakari.tatizo la tanzania kuwa na wanasiasa wababaishaji.nasema hili watoroshaji wakubwa wa madini yetu sio tanzanite pekee hata dhahabu ruby nk ni wachimbaji wadogowadogo ambao kwa bahati mbaya wanatetewa sana na wanasiasa.ili hali inajulikana udhibiti wao ni mgumu sana.katika kujua mapatao yao na control ya mauzo ikiwa pamoja na ulipaji kodi.

Acha porojo wewe. Tatizo linajulikana, kwa nini serikali isitatue? Hao wachimbaji wadogo wadogo wana tofauti gani na korosho, kahawa na mazao mengine ambayo serikali inawalalia wakulima? Ni uozo wa ccm na ufisadi wao ndio umetufikisha hapa.
 
nairobi ndo soko lao kuu hao mabroker na ndo mahali wanauza kwa bei nzuri kuliko hapa Tanzania

Suala sio kuuza Nairobi au India, kwani finally Tanzanite lazima tu itauzwa nje!

Suala hapa ni kwamba hiyo Tanzanite iliuzwa Kenya na India kwa njia ya magendo na ndiyo maana inaokana Kenya na India ndio muuzaji mkubwa wa Tanzaneti. Lakini kama Tanzaneti hiyo ingeuzwa kwa njia halali na serikali ikapata kodi yake, hata kama ingeuzwa baadaye huko Ulaya kutokea Kenya ingejulikana Tanzaneti sources yake ni Tanzania na sio Kenya.

Tatizo ni nini? Ni CCM wanaofanya wafabiashara ku smuggle Tanzanite to Kenya badala ya kuiuza kwa mfumo unaotambulika.
 
wadau,nijifiche wapi kwa aibu hii?natamani kujiua kuliko kuona fedheha hizi.
 
Hapa uwezi kuona maccm yanakuja kuchangia huu uzi!!!
 
wadau,nijifiche wapi kwa aibu hii?natamani kujiua kuliko kuona fedheha hizi.

Nchi yangu Tanzania!!!!!! shamba la bibi,,hii nchi hii ni bora usiijue kiundani utaishi kwa amani maana ukiijua sana waweza kuugua magonjwa ya kudumu,
 
Acha porojo wewe. Tatizo linajulikana, kwa nini serikali isitatue? Hao wachimbaji wadogo wadogo wana tofauti gani na korosho, kahawa na mazao mengine ambayo serikali inawalalia wakulima? Ni uozo wa ccm na ufisadi wao ndio umetufikisha hapa.

unataka kulaumua au kujua sababu
 
Uongozi mbovu ndiyo kisababishi kikubwa cha haya yote, hatuna vision ya kuona mbali na kuzuia upuuzi kama huu, inasikitisha sana mpaka machozi yananilenga
 
Tatizo hapa ni hii Serikali dhalimu ambayo haina vision. Wangewapa mtaji mkubwa STAMICO ili wanunue Tanzanite kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo kwa bei kubwa kuliko ya hao middle men wa kihindi. Hili lingewezesha kabisa kuongeza pato la Taifa kutoka Tanzanet kwa kiasi kikubwa sana na hivyo kuzipita nchi za India na Kenya kwa mbali sana. Hii ni aibu kubwa sana na kama sikosei Kenya si ya pili bali ni USA, Kenya ni ya tatu. Kulikuwepo hapa uzi miaka ya nyumba ambao kama sikosei ulionyesha pato la US linalotokana na Tanzanite ni la pili kwa ukubwa duniani baada ya India labda miaka ya karibuni hali imebadilika au hawakuweza kuzipata namba za US.

India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni)
Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni)
Tanzania iliuza Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.



Uongozi mbovu ndiyo kisababishi kikubwa cha haya yote, hatuna vision ya kuona mbali na kuzuia upuuzi kama huu, inasikitisha sana mpaka machozi yananilenga
 
What hii taarifa naielewa vzur au daaah Tanzania yangu kweli madin yapo nyumban then sisi ndo.washika mkia
 
Kwa mujibu wa Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, kwa mwaka jana pekee, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya Tanzanite kwenye soko la dunia.

India pia imekuwa ikiuza kwa wingi mno kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India.

IKUMBUKWE kwamba madini ya Tanzanite " yanapatikana" Tanzania pekee.

Source: Mwananchi, Nov 19
 
Nadikiaga Hasira na Roho kuniuma, nikidikia vitu kama hivi , husani kwenye hii secta ya Madini..

Tanzania ni nani Katuloga ...?
 
kuna channel ya kuuza vito vya thamani kuna mdada alikuwa anaisifia tanzanite sana uku anaelezea inatokea Tanzania.
Tena Ilikuwa inauzwa bei na ni ka dogo tu.nikakumbuka Tanzanite inakotoka watu masikini balah.

Kwa wale mlioko state mtakuwa mnaijua hiyo channel
 
Na mahindi yataozea kwenye maghala ya taifa huku nchi nyingi zinahitaji chakula
 
Kama kuna jambo ambalo limewaacha wananchi wengi katika mfadhaiko mkubwa ni habari kwamba nchi za Kenya na India zimeipita Tanzania kwa mbali kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee. Ni habari za kushtusha ambazo ni vigumu kuingia akilini, kwamba Taifa la Tanzania liko katika usingizi wa pono, huku madini yetu ya Tanzanite yakizinufaisha nchi ambazo hazijawahi kuwa na migodi ya madini hayo.


Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja alisema juzi kuwa, mwaka jana Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito na kwamba nchi hiyo ilisafirisha na kuuza nje Tanzanite yenye thamani ya Sh173 bilioni tofauti na Sh45.5 bilioni iliyouzwa na Tanzania. Alisema kwamba katika kipindi hicho, India iliuza Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Sh509 bilioni, kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa wa madini hayo, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India.


Hizi ni habari mbaya zinazodhihirisha kwamba Tanzania ni kichekesho cha dunia, kwani nchi nyingine duniani hulinda rasilimali zake kwa udi na uvumba pasipo kutoa mianya kwa mataifa ya nje kuzidhalilisha na kuzinyonya kiuchumi kama inavyofanyika kwa Tanzania. Ni aibu na janga kubwa kwa nchi yetu kukubali kugeuzwa shamba la bibi na nchi za kigeni zinazopora rasilimali zetu kama vile Tanzania haina mwenyewe. Tunashuhudia Serikali ikitazama upande wa pili, huku wanyamapori na rasilimali nyingine nyingi kama madini na misitu zikiporwa na wageni kwa kiwango na kasi ya kutisha.


Ni Tanzania pekee ambayo inaweza kuruhusu na kuvumilia hali hiyo ya kuporwa rasilimali zake mchana kweupe na asilimia kubwa ya wananchi wake wakiishi maisha ya udhalilishaji na umaskini uliopitiliza. Ni matokeo ya viongozi wengi kukosa uzalendo kiasi cha kutokuwa na uchungu na rasilimali za Taifa. Matokeo yake ni kuwapo rushwa na ufisadi uliokubuhu unaochochewa na mikataba mibovu inayosainiwa na viongozi wetu kwa kisingizio cha kuwavutia wawekezaji. Tumebakia kulewa sifa kutoka mataifa ya nje kwamba Watanzania wana utamaduni wa upole, amani na utulivu. Hatujiulizi kama sifa hizo zinatusaidia kujitambua ama zinatupumbaza zaidi kiasi cha kuwaachia wageni na washirika wao hapa nchini wapore rasilimali zetu.


Itakuwa ndoto kwetu kujikwamua kama viongozi wetu hawatabuni mifumo rasmi ya kibiashara badala ya kulalamika. Kamishna wa Madini anasema asilimia 80 ya Tanzanite inayopatikana Mirerani, mkoani Manyara huuzwa kwa njia za panya nje ya nchi. Hata hivyo, Serikali haionyeshi kutambua kwamba watoroshaji wakubwa wa madini ni wachimbaji wadogowadogo, wengi wao wakiwa ni matajiri wakubwa hapa nchini, lakini hawalipi kodi. Tunaambiwa Serikali inakusudia kuwasilisha muswada bungeni kurekebisha Sheria Namba 6 ili kumpa madaraka Kamishna wa Madini kutaifisha madini yanayomilikiwa kinyume cha sheria, ingawa bado ina safari ndefu kama hakutakuwapo utashi wa kisiasa.


Tunaambiwa pia kwamba kikosi kazi kitakachojumuisha askari kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kukabiliana na utoroshaji madini nje ya nchi kitaundwa. Sisi tunadhani kwamba juhudi zote hizo hazitazaa matunda yoyote kama viongozi na wananchi kwa jumla hawataonyesha uzalendo na kuwa na uchungu kwa nchi yetu na rasilimali zake.
 
Back
Top Bottom