Kenya na Israel na ujasusi wa kiuchumi

Kenya na Israel na ujasusi wa kiuchumi

Kinaitagwa kiswahili cha kunasa samaki nchanga. 😀😀 Eti wayahudi wanaihujumu Palestina ya Afrika. Jamani, mbavu zangu! 😀
We Cheka tu na endelea kujichekesha ila huyo n'gombe COW wenu maziwa tumeyanywa na nyama tuna choma mishikaki ila tutawabakishia mifupa jirani cow alikuwa mtamu kweli
 
Nimeshindwa kusoma hadi mwisho maana dah sio kwa Kiswahili hicho, unawapa tabu sana Wanajf.
Nikirudi kwenye hoja, hehehe Israel nchi ya mbali ya Kiyahudi ihangaike kuhujumu taifa maskini kama Tanzania ili iweje, mnapenda kujikweza sana.

Mkuu Israel siyo taifa la kitoto, unajua MOSSAD jinsi ilivyo na effiency ktk kazi kuliko hata CIA?
kama hujui pole Sana ndugu.
 
Nimeshindwa kusoma hadi mwisho maana dah sio kwa Kiswahili hicho, unawapa tabu sana Wanajf.
Nikirudi kwenye hoja, hehehe Israel nchi ya mbali ya Kiyahudi ihangaike kuhujumu taifa maskini kama Tanzania ili iweje, mnapenda kujikweza sana.
Nani kakuambia Tanzania ni maskini?!! Nani kakuambia Israel ni mbali hadi Tanzania?!!kaazi kwelikweli.
 
We Cheka tu na endelea kujichekesha ila huyo n'gombe COW wenu maziwa tumeyanywa na nyama tuna choma mishikaki ila tutawabakishia mifupa jirani cow alikuwa mtamu kweli
Hamna kiwanda cha ku'process' mifupa hiyo? Bone meal, jewelery, ceramics? Washamba kabisa.
 
Mkuu Israel siyo taifa la kitoto, unajua MOSSAD jinsi ilivyo na effiency ktk kazi kuliko hata CIA?
kama hujui pole Sana ndugu.

Najua Israel sio taifa la kitoto, najua Mossad is the best, lakini najiuliza watafuata nini Tanzania, nyie mna ugomvi gani nao hadi wajishushe kiasi cha kuwahujumu.
 
Nimeshindwa kusoma hadi mwisho maana dah sio kwa Kiswahili hicho, unawapa tabu sana Wanajf.
Nikirudi kwenye hoja, hehehe Israel nchi ya mbali ya Kiyahudi ihangaike kuhujumu taifa maskini kama Tanzania ili iweje, mnapenda kujikweza sana.
nchi kubwa nyingi zinatamani kuiweka tanganyika mfukoni miongoni mwao NI wabaguzi wakubwa Israeli ili kuua ushawishi wa iran
 
nchi kubwa nyingi zinatamani kuiweka tanganyika mfukoni miongoni mwao NI wabaguzi wakubwa Israeli ili kuua ushawishi wa iran

Sasa kuwatia mfukoni ni tofauti na kuwahujumu, halafu ujue Israel inatoshana na mkoa wenu mmoja na la ajabu eti mnakosa usingizi mkiwaza kwamba watawacha kuwaza ugomvi wao na Waarabu waelekeze mawazo yao kwenu ilhali nyie hamna lolote.
 
Najua Israel sio taifa la kitoto, najua Mossad is the best, lakini najiuliza watafuata nini Tanzania, nyie mna ugomvi gani nao hadi wajishushe kiasi cha kuwahujumu.
Mkuu kwani hujui kua madini ya almasi ya Tz kampuni inayoshughulika nayo ni ya ki Israel!? Kama sijakosea nadhani kampuni inaitwa De Bear(?) huu mfupa ulimshinda hadi nyerere kwahiyo mpaka hapa utakua umepata pakuanzia kuhusu maslai ya Israel nchini Tz.
 
Mkuu kwani hujui kua madini ya almasi ya Tz kampuni inayoshughulika nayo ni ya ki Israel!? Kama sijakosea nadhani kampuni inaitwa De Bear(?) huu mfupa ulimshinda hadi nyerere kwahiyo mpaka hapa utakua umepata pakuanzia kuhusu maslai ya Israel nchini Tz.

Sasa kama kampuni yao ya madini ndio kubwa kwenu hiyo sio sababu za wao kuwahujumu nyie, in fact hapo pa kuwawachia Wasiraeli wachume kwenu panatosha kuibua ugomvi na Waarabu. Maana ugomvi wa wale huwa wanakuomba uchague mmoja kati yao, aidha Muisraeli au Mwarabu.
 
Sasa kama kampuni yao ya madini ndio kubwa kwenu hiyo sio sababu za wao kuwahujumu nyie, in fact hapo pa kuwawachia Wasiraeli wachume kwenu panatosha kuibua ugomvi na Waarabu. Maana ugomvi wa wale huwa wanakuomba uchague mmoja kati yao, aidha Muisraeli au Mwarabu.
Hamna hoja hapa, zaidi ya wanaichukia Israel na wanaichukia Kenya. Wakaona wafanye mix. Vyote kwa pamoja. Utasikia wameanza kujiita mujahideena hivi karibuni.
 
Sasa kama kampuni yao ya madini ndio kubwa kwenu hiyo sio sababu za wao kuwahujumu nyie, in fact hapo pa kuwawachia Wasiraeli wachume kwenu panatosha kuibua ugomvi na Waarabu. Maana ugomvi wa wale huwa wanakuomba uchague mmoja kati yao, aidha Muisraeli au Mwarabu.
 
Mkuu Israel siyo taifa la kitoto, unajua MOSSAD jinsi ilivyo na effiency ktk kazi kuliko hata CIA?
kama hujui pole Sana ndugu.
Kwa taarifa yake Mossad imekuwa ikiichunguza hadi CIA. Mossad pia imekuwa ikiisaidia CIA
 
Najua Israel sio taifa la kitoto, najua Mossad is the best, lakini najiuliza watafuata nini Tanzania, nyie mna ugomvi gani nao hadi wajishushe kiasi cha kuwahujumu.
Tatizo sio ugomvi, tatizo ni rasimali za nchi. Makampuni ya Israel ndo yame monopolise soko la almasi duniani pamoja na dhahabua
 
Najua Israel sio taifa la kitoto, najua Mossad is the best, lakini najiuliza watafuata nini Tanzania, nyie mna ugomvi gani nao hadi wajishushe kiasi cha kuwahujumu.
Hi ni historia fupi ya kwa nini Israel iliamua kushilikiana na Kenya kuangusha uchumi wa Tanzania toka enzi za Nyerere na Nyerere kumchukia Israel

image-jpeg.522410
image-jpeg.522409

Ofisi ya De Beers inayothaminisha bei ya almasi(Israel),kushoto ni Herry Oppenheimer alipoenda Mwadui kumtaka Dr Williamson awauzie familia yao sehemu ya hisa za Mwadui
image-jpeg.522411

Dr Williamson akiwa "Sorting Room" na lundo la almasi
image-jpeg.522412

Mtambo wa Kuzalisha umeme mgodi wa Mwadui -1950's
image-jpeg.522413

Mwalimu wa Shule Ya Msingi Mwadui aliyeletwa na Dr Williamson
image-jpeg.522414
Gazeti la Australia mwaka 1952 likielezea ukubwa wa bwawa la Songwa Mwadui lililokuwa bwawa kubwa la kutengenezwa(Artificial Dam) duniani
GG
image-jpeg.522415

Meli iliyotumiwa na Wafanyakazi wa Serikali ya Kikoloni,kutoka Londo kuja East Africa,wakati wale wa Mwadui walitumia ndege
image-jpeg.522416

Uwanja wa Ndege Mwadui uliojengwa miaka 1940's wakati
image-jpeg.522417

Mbwa wa Mwadui,waliokuwa na mafunzo hodari ya kutumwa dukani na kupeleka barua maofisini.
image-jpeg.522418

Band ya Jeshi la Polisi Mwadui ilianzishwa mwaka 1949
image-jpeg.522419

Ujio wa Princess Mwadui akiambatana na Gavana Twinning
image-jpeg.522420

Club inayoelea katika bwawa la Songwa Mwadui,sehemu pekee ya Starehe ambayo hata Gavana wa Tanganyika alifika kujivinjari.
image-jpeg.522421

Swimming Pool iliyokuwa na viwango vya Kimataifa
image-jpeg.522422

Ofisi Kuu
image-jpeg.522423

Ndege aina ya Dakota DC 4 mali ya Dr Williamson

image-jpeg.522424


Mafundi wa Mgodi wa Mwadui,waliokuwa wanapatq uzoefu toka kwa Wataalamu wa kigeni
image-jpeg.522425
image-jpeg.522426

Kaburi la Dr Willy,nje kidogo ya mgodi wa Mwadui

Hii biashara ya madini toka enzi na enzi imekuwa ni "vita",tena ni vile vita ambayo havijawahi kumuacha mtu "salama".Iwe ni mfanyabiashara au mwanasiasa anayetazama maslahi ya watu wake kuliko yale ya mabepari wanunuzi wa madini husika.

Vita hii ilimkumba Dr John Williamson,mwanajolojia Mcanada mwanzilishi na mmiliki wa mgodi wa Mwadui,vita hivi vilimsumbua Julius Nyerere,mwana wa Afrika na Rais wa Tanzania.Mapambano haya hayakuziacha salama nchi zenye ukwasi wa madini kama DR Congo,Angola na Siera Leone.

Biashara ya madini duniani,imekamatwa na familia MBILI tu za Kiyahudi.Moja ikijielekeza kwenye madini ya dhahabu (na jamii zake) ambao ndio BARRICK na moja katika madini ya almasi ambao ndio DE BEERS.Hawa ndio "wamiliki" wa madini yote ya dunia,bila kujali mipaka ya nchi walipo na kule yalipo madini.

Familia ya Kiyahudi ya Oppenheimer (waliohamia South Africa) wenye kampuni ya "De Beers Group of Co.",ndiyo "imejimilikisha" madini yote ya almasi yaliyopo katika dunia hii baada ya "kumpoka kwa nguvu" umiliki wa kampuni Cecil Rhodes.Kuanzia madini ya India na Brazil,Afrika Kusini na Angola,Siera Leone na Botswana,Mwadui Shinyanga hadi Siberia ni "mali" ya De Beers.

Mwaka 1940,Dr John Williamson alifungua mgodi wa almasi Mwadui,nje kidogo ya mji wa Shinyanga.Mwadui ilikuwa na mkanda wa "kimberlait" wenye hifadhi nyingi ya almasi.Dr Williamson raia wa Canada,akautengeneza mji mdogo wa Mwadui na kuwa moja kati ya miji bora sana kusini mwa jangwa la Sahara (Mwadui Township).

Kufikia mwaka 1947,Dr Williamson alikuwa amejenga nyumba bora za wafanyakazi,hospital ya kisasa,shule za msingi tatu,mbili za wafanyakazi wa kiafrika na moja ya wafanyakazi wa kizungu ambayo ndio ilikuwa moja ya "English Medium School" ya kwanza Tanganyika.Akajenga chuo cha Ufundi wa aina zote ndani ya mgodi kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi,chuo cha kilimo na shule ya upili.Huko kwao waliita "School Near The Equator".Ilikuwa shule bora na ya kisasa.
.

Dr Williamson akajenga uwanja wa ndege wa kisasa ndani ya mgodi mwaka 1940's,akanunua ndege mbili za mwanzo aina ya Dakota DC 3 na Cessna180 wakati huo hata serikali ya Kikoloni ya Muingereza ikiwa haina wazo la ndege,wakati serikali ya Tanganyika ikiwa haina uhakika wa uwanja wa ndege kupokea ndege kubwa aina ya Dakota DC4,Dr Williamson alikuwa tayari na uwanja huo,ambapo wageni toka London Uingereza,ndege zilitua Malta,Khartoum-Sudani na baadae Nairobi (Wakati huo ukiitwa Embakasi Airport),na baadae kuchukuliwa na ndege moja kwa moja mpaka Mwadui Shinyanga,ambapo Serikali ya Kikoloni ilikuwa na afisa mmoja wa uhamiaji. Dr Williamson alijenga kanisa na msikiti bora na wa kisasa kwa ajili ya wafanyakazi wake
Wakati huo,usafiri pekee wa watumishi wa serikali ya Kikoloni ilikuwa ni meli maarufu ya "The Braimer Castro" iliyokuwa inatoka Ulaya mpaka Mombasa.Yeye Dr Williamson na wafanyakazi alioajili walikuwa wanapanda ndege kupitia Embakazi na baadae Mwadui.

Williamson akajenga "Power House" yenye uwezo wa kuzalisha 900kw kwa mitambo ya diesel na 750kw kwa Gas Turbine na hivyo kuwa na umeme wa uhakika kuliko hata jiji la Dar es Salaam achilia mbali mkoa wa Shinyanga.Wakati huo umeme wa Dsm ulikuwa unategemea ule mtambo ulioweka pale makao makuu ya Wizara ya Nishati kama makumbusho.

Ndani ya mgodi wa Mwadui,Dr Williamson alijenga "Sailing Club",yaani Club inayoelea katika bwawa alilichimba eneo la Songwa.Hii ndio ilikuwa Club pekee inayoelea Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara.


May 2,1952,Gazeti Kongwe la "The Cairns Post" (Est.1882) liliandika juu ya uwepo wa bwawa la Songwa,Mwadui-Shinyanga,Tanganyika.Gazeti hilo la Australia lilielezea bwawa la Songwa kama moja kati ya "Artificial dam" kubwa zaidi duniani,lenye uwezo wa kuchukua "two thousands million gallons of water".Mradi ambao hata serikali ya mkoloni iliushangaa.

Mwadui kulikuwa na mfumo wa maji safi na maji taka yaliyotibiwa na wataalamu waliosomeshwa na mgodi.Huduma ya elimu ya watu wazima na elimu ya uchumi wa nyumbani "home economics" kwa wamama waliokuwa nyumbani.Kufikia mwaka 1970,karibu 97% ya wakazi wa mgodi huo ambao walifikia 60,000 walikuwa wanajua kusoma na kuandika,na wamama wakiwa na ujuzi wa ushonaji,upishi nk.

Dr Williamson aliajiri mpishi maarufu toka Ufaransa,ambaye alikuwa akipika na kuandaa chakula katika "mesi" kubwa ndani ya mgodi wa Mwadui.Mfaransa huyo alifundisha wapishi wengi wa Kiafrika na alikuwa kama "chuo" cha wapishi wengi wa maafisa wa serikali ya kikoloni,na hata wapishi wa mwanzo wa Ikulu ya Dsm baada ya Uhuru,walipita katika mafunzo ya "mesi" ya Mwadui.Kufikia mwaka 1950,Tanganyika ilikuwa na vyumba viwili tu vyenye hadhi ya kulala familia ya kifalme ya Uingereza,chumba kimoja katika Ikulu ya sasa ya Dsm na kingine kwenye "rest house" ndani ya mgodi wa Mwadui.

Mgodi wa Mwadui chini ya Dr Williamson,uliweza kujenga kiwanja cha golf chenye mashimo tisa,ambacho kilikuwa ni moja ya viwanja vikubwa na vya kisasa Afrika nzima.Mwaka 1952,Dr alishawishi mpaka mashindano makubwa ya kombe la Malikia la Golf nchini Canada yafanyike Mwadui,kila kitu kilikubalika isipokuwa hali ya uwanja wa Embakasi Kenya haukuwa sawa sababu ya vuguvugu la vita vya Maumau lililotishia usalama wa kiwanja.Swimming Pool za viwango vya Olympic tatu ndani ya mgodi

Viwanja vya tennis,pamoja na viwanja vitatu bora vya mpira wa miguu vilivyokuwa na viwango vya kimataifa vilijengwa ndani ya mgodi wa Williamson.Timu ya mpira ya Mwadui Mining ilishiriki mashindano ya kitaifa kwa ubora mkubwa.Waamuzi wakongwe wa viwango vya kimataifa kama Mshangama na Mashishanga(RC wa zamani) ni matunda ya Dr Williamson.

Ustawi wa maisha ya mgodi na kushamiri kwa faida ya Dr Williamson kuliwauzi "wamiliki" wakubwa wa biashara ya madini ya almasi ambao ni De Beers Group of Co.Almasi ya Mwadui iliingia kwa kasi sana katika soko la dunia jijini London.De Beers wakashindwa kumdhibiti Dr Williamson na almasi yake,akafanya almasi ya Afrika Kusini kushuka thamani katika soko la dunia,njia pekee iliyobaki kwa De Beers ilikuwa kumtaka Dr Willy aungane nao katika biashara.

Dr Willy alikataa,akataka kuupeleka mgodi kwa namna yake,hakutaka kuwanyonya Waafrika na wafanyakazi wake,ndoto zake ilikuwa ni kuijenga "Quebec ndogo ndani ya Tanganyika",alitaka kuonyesha tofauti ya thamani ya madini na maisha ya wazawa kwa kuutumia mgodi wa Mwadui.Aliiishi Afrika Kusini na kuona jinsi wazawa wa kando ya migodi na wafanyakazi wasivyofaidika na madini katika ardhi yao.

.
Dr Willy hakutaka hali hiyo itokee.Mkoloni na De Beers walichukia uamuzi wa Dr Williamson kuufanya mgodi wa Mwadui kama "Ulaya ya Afrika".Walim-fustrate kwa kukataa kuipokea almasi yake katika viwanda vya wachonga almasi kule London (diamond Cutting).Mwaka 1950,Serikali ya kikoloni kwa Shinikizo la familia ya Oppenheimer wakataka kuutaifisha mgodi wa Mwadui ili uwe mali ya serikali ya mkoloni na si mtu binafsi.

Hali hii ilichanganya sana Dr Williamson,akawa mlevi wa kupindukia wa whisky ya Scotland,akawa "chain Smoker" na kwa sababu alikuwa "bachelor" hakuwa na mtu wa kumtuliza mawazo.Mwaka 1952,mwezi Machi, kampuni ya De Beers ilimtuma mtoto wa kwanza wa mmiliki wa kampuni,Herry Oppenheimer kuongea na Dr Williamson namna ya kuuza sehemu ya hisa kwa De Beers ili aweze kuwa "salama",Dr Williamson alisitasita sana,akawaza jinsi wafanyakazi wake wa kiafrika na wale aliowaleta toka Ulaya watakavyonyanyasika,akawaza jinsi ndoto yake ya kujenga "Mji wa Quebec wa Afrika" inavyopotea.


Mwaka 1956...Princess Margareth akiambatana na Gavana wa Tanganyika na ujumbe wake walitembelea mgodi wa Mwadui wakiwa ndani ya ndege aina ya Dakota DC4 mali ya Dr Williamson.Ulikuwa ni ushawishi kumfanya Dr aachie sehemu ya hisa za mgodi

Kwa shingo upande akatoa 50% yake kwa kuwauzia De Beers kwa £ 4 milioni,miaka michache baadae akagundulika kuwa na saratani ya koo, ugonjwa uliochukua maisha yake miaka michache baadae(japo ilisimekana ulipandikizwa ili kumuondoa).Aliomba kuzikwa ndani ya eneo la Mwadui kwani kwake Mwadui ndio ilikuwa nyumbani.

Mwaka 1958,Herry Oppenheimer ndio akawa mwenyekiti wa Mgodi wa Mwadui,sehemu ya hisa za Dr Williamson aliachiwa dada yake,na kwa sababu hakuwa na uzoefu wa mambo ya madini,De Beers wakamshauri aziuze.De Beers na serikali ya kikoloni wakawa na 50/50 ya umiliki wa mgodi na almasi yote ya Mwadui.Ndoto za De Beers na familia ya Oppenheimer ikawa imetimia....Nayo ni "KUMILIKI MADINI YOTE YA ALMASI CHINI YA ARDHI YA DUNIA


Julius Nyerere alipochukua nchi 1961,baadae aliamua kutaifisha mali zote,akaunda Stamico isimamie sekta ya madini.De Beers iliwauma sana kufurushwa na Nyerere.Hawa Waisrael wakaunda team ya namna ya kumkomesha Julius Nyerere,kwanza waliweka fitna katika soko la almasi pale London,wakazishawishi "Diamond Cutting and Polishing Companies" kule London ziisusie almasi ya Mwadui,Mwalimu akawa mbishi na kuimarisha "TunCut Diamond Co" pale Iringa.

De Beers akazidi kuweka fitna kwenye viwanda vinavyotengeneza vipuri vya mitambo iliyopo Mwadui.Kuanzia mitambo ya kuchimba,kusafisha na kuchambua almasi.Mwishowe vifaa vikachakaa bila kuwa na ukarabati.Uzalishaji ukapungua na almasi ya Mwadui ikapotea katika soko la dunia.Wataalamu toka nje waliokuwa katika mgodi wa Mwadui wakaondoka.Ikawa ni hasara juu ya hasara.


Mwaka 1993,De Beers kupitia Herry Oppenheimer yuleyule wa enzi za Dr Williamson walirudi Tanzania kupitia mtoto wao Nicolaus
Oppenheimer,wakaishawishi serikali ya Tanzania,na hatimaye De Beers Group of Co. wakauziwa 75% ya hisa za mgodi wa Mwadui.Hatimaye ile ndoto yao ya kumiliki madini yote ya almasi ya dunia ikaendelea kutimia.

Hawa ndio De Beers,familia ya Kiyahudi ya Oppenheimer.Wanaosadiki kuwa almasi yote inayopatikana katika uso wa dunia hii ni mali yao.Walimsurubu Dr John T. Williamson,mzungu-msukuma aliyetaka mali ya ardhi ya Mwadui ilete thamani kwa Waafrika na Tanganyika.Hawa ndio De Beers waliomtikisa Mwalimu Nyerere,hawa ndio familia ya almasi duniani,wanaochochea yale ya Angola ya Savimbi,Siere Leone ya Foudah Sankho na DR Congo ya M23 ili waendelee kuchota utajili wa Afrika.
 
Wakenya wametumika sana na hao wazungu kuwafanyia fitna waAfrika wenzao mana viongozi wao wengi walikua walafi tu wakiwekewa fungu wanafanya kazi zote chafu za hao mabwana zao ila sasa mambo yanabadilika wajicheki sana
 
Back
Top Bottom