Tetesi: Kenya na Rwanda kujiunga jumuiya ya NATO

Tetesi: Kenya na Rwanda kujiunga jumuiya ya NATO

Ziara ya Rais wa Kenya William Ruto nchini Marekani imeibua jambo. Ruto kapokelewa na mwenyeji Rais Joe Biden na kuzungumzia Mengi.

Biden kamuomba Ruto waanzishe ushirikiano kabambe ikiwa ni pamoja na kujiunga na NATO. Pia kuna tetesi kuwa Rais wa Rwanda atafuata mkumbo huo mwezi July mwaka huu.

Mpango huu ukifanikiwa NATO itakuwa na wanachama wanne nje ya bara la ulaya ambao ni USA, Canada, Kenya na Rwanda.

Source: BBC Swahili
Ujinga mzigo. Hata huelewi nato ni nini. Ndio maana unaandika takataka hizi.
 
Kitu ambacho nimekisikia kuhusiaana na habari hii ni kwamba mataifa haya yanatarijiwa kuwa non NATO members kutoka kwa US lakini sio NATO member ,yaani kuna treatment mbalimbali watapata kutoka kwa US ikihusiana na misaada ya kifedha na mambo ya kijeshi kama key players kukabiliana na ugaidi.
 
Hawataweza kujiunga na NATO kwasababu
Ni nchi ambazo hazina nguvu kijeshi ingekua rais ivo bas Saudi arabia,UAE,Australia na japan zingekua NATO,

kwa africa Egypt na aljeria zingekua NATO lakin unfortunately mambo hayako hivo
Embu dadavua
 
Yaani Biden ndo awaombe Kenya maajabu haya
 
Ziara ya Rais wa Kenya William Ruto nchini Marekani imeibua jambo. Ruto kapokelewa na mwenyeji Rais Joe Biden na kuzungumzia Mengi.

Biden kamuomba Ruto waanzishe ushirikiano kabambe ikiwa ni pamoja na kujiunga na NATO. Pia kuna tetesi kuwa Rais wa Rwanda atafuata mkumbo huo mwezi July mwaka huu.

Mpango huu ukifanikiwa NATO itakuwa na wanachama watano nje ya bara la ulaya ambao ni USA, Canada, Uturuki, Kenya na Rwanda.

Source: BBC Swahili
wanapewa status ya non-nato member, status ambayo wanayo morocco, egypt na tunisia nadhan kwa afrika!
 
Britain's defence secretary has called on neutral countries to join NATO.
Grant Shapps cited the threat allegedly posed by Russia.

Hii Habari niliisoma juzi nikaipu

Mnajua Ada ya mwaka kuwa mwanachama wa NATO au mmnaongea tu as if you know to read and kusoma? kuna nchi zinadaiwa ada na uchumi wake upo juu... eti kenya na rwanda..

Ruta ameenda Marekani kumshangaa Shaq Oneal tu alivyo Giant
Sidhani kama Kenya imeomba kuwa mshirika wa NATO, nadhani yenyewe ndiyo imeombwa kwa hiyo suala la garama Kenya haliwahusu.
 
Hakuna nchi ya Africa au sehemu yoyote zaidi ya Ulaya na Amerika Kaskazini inayoweza kujiunga na NATO kutokana na Article 10 ya Washington Treaty.

Habari yenyewe ni kuwa US ina plan kui designate Kenya kama major ally (mshirika wake mkubwa) ambae sio mwanachama wa NATO.

Muwe mnasoma au kusikiliza habari vizuri.
Member wamekurupuka sana hawajaelewa
 
Mkuu , NATO wameshtuka karibu kunakucha.
Ujio wa BRICS ni tishio kwa umoja huo ambao hivi sasa sio tishio tena duniani.
Mkuu hiyo brics ina miaka mingapi hadi sasa, mbona hakuna la maana lilofanyika hadi sasa? Kenya toka miaka hiyo ni mshirika mkubwa wa UK, na kuna kambi yao hapo, hata USA, ana msaidia sana kwenye vita na alshabab, sio kwamba anajiunga NATO ila atakuwa ni mshirika mkubwa nje ya NATO
 
Hakuna nchi ya Africa au sehemu yoyote zaidi ya Ulaya na Amerika Kaskazini inayoweza kujiunga na NATO kutokana na Article 10 ya Washington Treaty.

Habari yenyewe ni kuwa US ina plan kui designate Kenya kama major ally (mshirika wake mkubwa) ambae sio mwanachama wa NATO.

Muwe mnasoma au kusikiliza habari vizuri.
Nato wamemkimbia Yemen pale Red Sea, sa Yemen anawafata mpa kule Mediterranean Sea.

Yemen ni kiboko wa Western, leo hio wameripua kule Mediterranean Sea.

View: https://www.youtube.com/live/9l7uF2InTdw?si=QzQ6-H468A2yrP5U
 
Niliposikia hii habari BBC Swahili, nikajua kumekucha. Nini hatma ya Tanzania na majirani hawa haswa taifa chokozi kama Rwanda? Uganda, Burundi, congo na Tanzania tutakipata kisawasawa. Just the matter of time.
Umefikiri kwa kina sana hili sio swala jepesi kama tunavyofikiria lazima Nchi iangalie mstakabali wake wa huko mbele maana hii mipango kazi ikikomaa basi tunakwisha hivi tunajiona.
 
haina shida, kama kuna faida yeyote wakifaidika Kenya au Rwanda na sisi tutafaidika. sioni shida yeyote kwanza watatusaidia kupigana na ugaidi.
 
Hata New Zealand na Australia (Members wa 5 eyes) sio NATO members, ndio itakuwa hawa wala rushwa wenzetu
 
Hakuna nchi ya Africa au sehemu yoyote zaidi ya Ulaya na Amerika Kaskazini inayoweza kujiunga na NATO kutokana na Article 10 ya Washington Treaty.

Habari yenyewe ni kuwa US ina plan kui designate Kenya kama major ally (mshirika wake mkubwa) ambae sio mwanachama wa NATO.

Muwe mnasoma au kusikiliza habari vizuri.
Dah asante sana mkuu, hii tulikuwa tushapigwa na sisi tungeenda kuwapiga wana kwenye kahawa.
 
Inaonekana kuna shinikizo kwa hizi nchi ndogo kiuchumi kulazimishwa kuchagua upande kwahiyo huwezi kuwa salama Kama hauko kati hizi pande mbili. Ni aidha uwe na Usa na NATO au uwe Mashariki kwa maana ya BRICS+,STO n.k
 
Back
Top Bottom