Kenya imemrejesha nchini Balozi wake aliyekuwa Somalia na kumwamuru Balozi wa Somalia nchini humo kuondoka mara moja, baada ya nchi hiyo (Somalia) kupiga mnada vitalu vya utafutaji mafuta na gesi katika eneo la bahari linalogombewa na mataifa hayo. Mnada ulifanyika Februari 7 jijini London.