Tatizo sisi waafrika hatuhoji maswali ya maana, tunapelekeshwa na kukubali tuu, kwa kuwa ni UN.
Kutumia kigezo cha dola moja/mbili kama kipimo cha umasikini, si sawa. Kipimo halisi ni uwezo wa hiyo dola kuweza kutumika (PPP) kati ya nchi na nchi.
Hapa US kula vyakula vyenye Afya (Organic) ni gharama sana, watu wengi hawamudu. Maziwa ya kawaida (feki), kwa mfano; Walmart wanauza gallon moja (3.7liters) kwa $1.8 wakati organic milk (real) $6.8. Sasa mtanzania wa kawaida anakula kila kitu organic, kuanzia nyanya, machungwa, mchele n.k. Sasa kama ukichukua kila kitu anachokula mbongo "masikini" na kulinganisha bei yake US utaona watanzania wengi siyo masikini kiivyo, kwasababu wanamudu mahitaji ya kula chakula cha hadhi ya juu (organic).
Sasa badala ya watu wetu kuhoji hivi vipimo vya umasikini kulingana na nchi husika, tunakubali kukokotwa kama mkokoteni, kisa UN kasema.
Umeongelea hali ya nyumba wanazoishi n.k lakini tunarudi pale pale, hizo nyumba niza madeni mpaka utosini. Watu wanaishi paycheck to paycheck, tatizo dogo likitokea mtu anakuwa homeless sasa utasema hiyo jamii ni ya tajiri?