Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kwa miaka mingi Tangu nyakati za Uhuru Kenyatta na sasa Ruto serikali ya Kenya ilikuwa katika bonanza la kukopa pesa ndani na nje ya nchi kwa pupa huku ikiwaaminisha raia wake deni lao ni himilivu na kwa ajili ya maendeleo yao. Umefika wakati sasa madeni yameiva, theluthi mbili(60%) ya mapato yanayokusanywa yanaelekezwa kulipa mikopo, wengine wanasema kila sh 10 za nchi hiyo zinazokusanywa sh 7 ni kwa ajili ya kulipia madeni katika hili serikali haina namna nyingine zaidi ya kuongeza kodi na kupunguza huduma za kijamii zinazogharamiwa na serikali. Raia wa Kenya hasa vijana wa GenZ wamegoma kufungua milango yao serikali inapowagongea hodi kulipa deni. Demokrasia sio dawa ya matatizo yote kama haya ya madeni.