Kenya ni Nchi isiyo hisha Vituko... hawaogopani, wapiga dili

Chillah

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2016
Posts
8,870
Reaction score
10,066
KENYA: Wananchi wamekasirishwa na taarifa kuwa Wabunge 20 wamesafiri kwenda nchini Urusi kutazama Kombe la Dunia kwa fedha za umma

Wabunge hao walikwenda kutazama michezo minne na watakaa nchini humo kwa muda wa wiki 2 huku wakitarajiwa kutumia maelfu ya dola

Kwa upande wake Waziri wa Michezo Rashid Echesa, amesema kwamba alitoa idhini kwa Wabunge 6 pekee kusaifiri, ili wakajifunze jinsi matukio makubwa ya kimataifa yanavyoandaliwa

Wananchi kupitia mitandao ya kijamii wamehoji kwamba inakuwaje Wabunge wasafiri maelfu ya kilomita kwenda kushuhudia tukio ambalo hawana uwezo wa kuliandaa?

Pia Wananchi wamehoji ni kwanini Wabunge hao hawawezi kuhudhuria michezo ya ligi ya nchi Kenya lakini wamesafiri hadi Urusi kushudia michuano washiyoshiriki
 
Na furahishwa na hoja kuwa wameenda kujifunza jinsi ya kuandaa... wakati maandalizi yana anza hawa kwenda kujifunza ila wakati wa tukio hisika ndio wana enda jifunza....

Hahahahahahahahaha... majirani zetu uhuru (kipenzi cha wakenya) ana kazi sana kuikwamua hii nchi...
 
huyo tukunyema naye vipi hapo uwanjani[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Pumbavuu zao, ila wacha iwe hivyo ndio ndugu zangu Wakenya tunapokwenda kuchagua viongozi bila kutumia akili yanatukuta ya kihivi, halafu hamna cha uchama wakati wanafanya pumba kama hizi maana humo kuna wa upinzani na wa mlengo wa serikali.
Hii imenipa hasira balaa, hongera sana wabunge, fanyeni yenu tu....
 
Hahahah... waendelee kula mali ya umma sio???
 
Hiki kituko ipo siku kitakuja kutokea hata hapa... ni bahati tu ya ukali wa Magu ndio una waogopesha kwa sasa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…