mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,555
- 6,972
Ni ukweli uliowazi kuwa Kenya na Tanzania ni washindani wakubwa sana kiuchumi kwa Afrika Mashariki. Majirani zetu hawa ambao ni watani wetu, uchumi wao ndio mkubwa Afrika Mashariki. Kuna mengi sana sisi Tanzania tunajifunza kwenu ili kwenda sambamba nanyi ikiwezekana kuwapiku kabisa. Tanzania uchumi wetu unakuwa kwa kasi kubwa japo bado majirani zetu hawa wako mbele yetu. Na sisi tunasema tunajitutumua ili kukimbizana.
Pamoja ushindani wetu huu wakenya ni watu wazuri sana ukilinganisha na majirani wengine wa Afrika Mashariki. Watanzania na wakenya wakikutana nje hujiona karibu zaidi kuliko kuliko mataifa mengine ya majirani. Hawana majivuni, hawana dharau, hawana roho mbaya, tabia tabia za ajabu alafu wako frank. Tumekuwa na maingiliano makubwa sana baina yetu . Binafasi nikumuona mkenya namuona kama mtani wangu vile, kuna watanzania wengi sana wanafanya shuguli zao kenya,kuna watanzania wengi wanafamilia, ndugu na jamaa zao Kenya. Kuna wengine kwenda kenya ni kama kwenda mkoa ndani ya Tanzania. Binafsi najisikia niko na amani nikiwa Kenya kuliko nchi nyingine jirani. Huwa nacheka sana nikisikia mkenya akiongea kiswahili ( acha ile naongea swahili fasaha, nazungumzia ila natamka maneno vibaya).
Mbali na habari tofauti jukwaa hili, lakini naona zaidi ni ushindani wa kiuchumi, huu ushindani naupenda. Hakuna ushindani mzuri kama wa maendeleo na uchumi.
Je na ninyi mnajisikia hivyo kwetu? Mnatuona na kutuchukulia vipi sisi waTZ?