Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ziara ya Rais Samia Kenya imewaibua wafahidhina makanjanja wasiojua chochote kuhusu umuhimu wa mahusiano mazuri kwa manufaa biashara na uchumi kati ya nchi mbili.
Wameibuka vihiyo wenye mawazo ya kijima wanaofikiri vita vya kibiashara na mahusiano mabovu katika ya Kenya na Tanzania yana faida kwetu Tanzania.
Inashangaza kuona maelfu ya nyuzi za kumpinga Rais Samia zikipanda jukwaani baada ya kuonyesha muelekeo wa kurejesha uhusiano wetu na Kenya uliporomoka vibaya miaka mitano iliyopita na kupelekea kushuka vibaya sana kwa ujazo wa biashara kati ya nchi hizi mbili.
Kuna watu wanalia na kupiga mayowe hata Kenya kuuziwa gesi na Tanzania wakisema haitutoshi, wameacha kelele za Stiglers Gorge sasa wamerudi kwenye gesi tena waliyosema imepewa mabeberu.
Nyie wafahidhina uchwara mnaofikiri Kenya inainyonya tu Tanzania ndio maana imepiga hatua kubwa katika uchumi wa viwanda kutuzidi isomeni historia vizuri muone ni jinsi gani Kenya pamoja na matatizo yake mengi walivyojenga uchumi wao endelevu wa soko wakati sisi tunakomaa na ujamaa wetu na sera kujifungia ndani kwa takribani ya miongo 3, miaka 24 ya Nyerere na 5 ya Magufuli.