Mkuu, kuuza gas mbona jambo jema sana. Hakuna hata mmoja mwenye kupinga, maadam tunapata inflows of cash.
Watu wengi tunashangazwa na kuona taarifa mkuu wa nchi akisaini mkataba wa makubaliano ya kujenga pipeline. Hatujawahi kusikia huko nyuma kuwa kuna mazungumzo ya awali na Kenya kuwazia gas na itafanyika kwa kujenga pipeline.
ila itoshe kusema, tuna imani na madam President, ni mzalendo sana kama alivyokuwa mwendazake. Ila pengine mode of operandi kwake ni tofauti na mwendazake.
Kenya hakuna anaewachukia, ila inafahamika, wale ni wakora. Walipora mali nyingi za East Africa baada ya jumuia kufa. KQ kwa asilimia kubwa imejijenga juu ya assets za jumuiya na wangekuwa waungwana baada ya jumuia kufa kuwa na mgao wa mali na madeni.
Viwanda vya chai na kahawa vingi vilikuwa mali ya EA; Tanzania ikiwa na mashamba makubwa, wao wakiwa wanafanya processing. Baada ya jumuiya kufa, walipora kiroho safi. Ukiumwa na nyoka, au kama umewahi kudhulumiwa na mtu huyo huyo, uwoga ni akili.
Dangote amekwenda kuwekeza Kenya kiwanda cha Cement wakataka rushwa akashindwa mpaka akakimbilia Ethiopia. Mburushi wa Igunga nae amekwenda kujaribu kuwekeza kwenye gas na mtaji wa USD 30mil; jamaa wamemzungusha kwa miaka minne.
Nyerere alikuwa mtu muungwana sana na bingwa wa kutatua mizozo, kuna wakati Wakenya hawahawa walizingua to the extent Tanzania kufunga mipaka na Kenya.
JK one of the top diplomat, walishindwana na Wakenya, mpaka wakamtenga na Kenya akiwa ring leader wa coalition of the willing.
Hii major shift ya madam President ile kufanya ziara tu, na kusaini mradi wa bomba la gas, swali , kwanini imekuwa haraka kiasi hicho?
Sio zamani sana, ni miaka 3 imepita, Balozi wa Kenya hapa nchini alimshika mkono mfanyabiashara mmoja wa Kenya na kampuni yake ya Indo Power Solutions, akasaini mkataba wa awali kununua 100,000 tonnes za korosho za thamani ya US$180.2 million (sawia na TZS 417.4 bn)
Kenyan ambassador to Tanzania Dan Kazungu is on the spot for endorsing a local firm that took John Magufuli government for a ride in a Sh410 billion cashew nut deal.
www.thecitizen.co.tz
Haikuwa mbaya kujaribu kusaini mkataba wa awali, ili angepata pesa za mkopo na kulipa, angechukua tani laki 1 za korosho. Cha ajabu hakununua na baadhi ya media zao baada ya hapo wakaja na habari za uwongo kuwa serikali ya Tanzania imegoma kumuuzia Mkenya licha ya kuwa one the highest bidder!
Tanzania haijawahi kumwonea wivu Kenya, ndio maana Tanzania imefungulia goli kwa kampuni nyingi tu za Kenya kuwekeza Tanzania, unlike wao kufunga milango.
Hapa ni lazima kuwa na equitable way of doing business kati ya nchi hizi mbili.