Ni kweli mmejitahidi, hongereni sana, niliona jana kwenye TV Mh Rais Kenyatta akiliongelea hilo katika kuhakikisha kuwa wananchi wa kawaida wanapunguziwa gharama za uunganishaji umeme, na kwa sasa Kenya mmefika 55% as per yesterday report. Tanzania bado tuko nyuma kama kawaida yetu kwa sasa tuna 35% long way to go lakini tunamatumaini kwa utawala huu tutafika tu huku hususan ukizingatia juhudi zinazofanywa katika kujenga miundombinu ya umeme. Ila kaka uwe na busara don't generalize and stereotype certain particular groups of pepole kuwa sisi Watanzania wote hatukwenda shule, hatujui kizungu, hiyo sio sahihi kwakuwa kujua lugha kwa ufasaha hakuna mahusiano ya moja kwa moja na someone's intelligence or brilliance, wewe mbona hujui kiswahili unaongea kama mshamba mmoja hivi, mbona Wakenya hamjui Kifaransa, Kijerumani na lugha zingine, kwahiyo tuseme kuwa hakuna shule kwenu kwakuwa hamjui hizo lugha, what is so special with English? English ni kama lugha ya Waluo na Wakikuyu tu so ondoa hiyo slavery mentality yako kuwa asiyejua Kizungu basi hakwenda shule. Sisi tupo huku kwenye mashirika makubwa ya Kimataifa na tunawatuma ndugu zako hapo kama tunavyotaka lakini hatuwanyanyasi they are a part of our winning team. MKATAA KWAO MTUMWA.