Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Ripoti katika eneo hilo zinasema kuwa washambuliaji hao waliwashinda nguvu polisi mmoja katika lango la nyumba hiyo na kuingia ndani.
Ufyatulianaji wa risasi uliendelea katika nyumba hiyo ambayo imezungukwa na maafisa wa polisi.
Bwana Ruto hakuwepo wakati huo.
Kisa hicho kinajiri siku 10 kabla ya Kenya kufanya uchaguzi wa Rais, Ubunge na ule wa Kijimbo.
Makamu wa Rais alikuwa alikuwa ameondoka saa chache kabla ya uvamizi huo ili kuhudhuria mkutano wa kampeni katika mji wa Kitale, ambapo alijiunga na Rais Uhuru Kenyatta.
Kenyatta anatetea kiti chake cha urais mwezi ujao.
Huku uchaguzi wa 2013 ukifanyika kwa njia ya amani kulikuwa na ghasia mbaya za baada ya uchaguzi 2007 ambazo zilisababisha vifo vya watu 1000 huku wengine 600,000 wakiwanchwa bila makao
Hata hivyo wataalamu wanasema hawatarajii kuona kiwango cha ghasia kama hicho kufuatia uchaguzi wa Agosti 8.
Chanzo: BBC
PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana