maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Wakati wa kampeni za kugombea urais nchini Kenya kiongozi wa kambi ya upinzani bw Raila Amolo Odinga alikuwa akijinadi kwamba akishinda katika uchaguzi ule moja ya mambo ambayo angeyapa kipaumbele ni kuyaondoa majeshi ya KDF nchini Somalia.
Huku Tanzania kuna wakati Rais Kikwete naye alijibaragua baada ya kufanikiwa kumtoa Mohamed Bacar, kiongozi wa mapinduzi haramu ya visiwa vya Anzouan huko Comoro na kutaka eti jeshi letu la JWTZ litoe mafunzo kwa majeshi ya Somalia lakini kelele zilizotoka kwa wananchi zilimtisha na akaamua kuusitisha mara moja mpango ule wa kishetani.
Naamini kuwepo majeshi ya Kenya huko Somalia kuna hasara kubwa kwa maisha ya raia na uchumi wa Kenya kuliko faida kwa Kenya na hata kwa jumuiya ya kimataifa inayoyafadhili majeshi hayo.
Mashambulizi na mauaji yanayofanywa na askari wa Al Shaabab dhidi ya raia na askari wa Kenya walioko Somalia yanatosha kuionya Kenya kwamba hiyo ni vita ambayo hata siku moja hawataishinda.
Suluhu ya yote hayo inafaa Kenya iyarudishe nyumbani majeshi yake kana matakwa ya Raila yalivyokuwa.