Kenya Opens New High Commission in Jamaica to Strengthen Caribbean Ties

Kenya Opens New High Commission in Jamaica to Strengthen Caribbean Ties

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Kenya imeendelea kupanua ushawishi wake duniani baada ya kufungua rasmi High Commission mpya mjini Kingston, Jamaica, hatua inayotarajiwa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kitamaduni kati ya Kenya na mataifa ya Caribbean.

Balozi Mwenda Karisa amewasili Kingston kuanza rasmi majukumu yake kama Kenya's first resident High Commissioner to Jamaica. Kabla ya kufunguliwa kwa mission hii, masuala yote ya kidiplomasia kati ya Kenya na Jamaica yalikuwa yakiratibiwa kupitia ubalozi wa Kenya uliopo Havana, Cuba.

Kwa kufunguliwa kwa High Commission ya Kingston, Jamaica sasa inakuwa diplomatic mission ya pili ya Kenya katika eneo la Caribbean, hatua ambayo itawezesha Kenya kuwa karibu zaidi na nchi za eneo hilo na kuboresha huduma za kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kikanda.

Katika taarifa yake, Kenya High Commission ilisema hatua hiyo ni historic milestone katika uhusiano wa Kenya na Jamaica. Serikali imeeleza kuwa inatarajia kushirikiana kwa karibu na serikali na wananchi wa Jamaica ili kuendeleza maslahi ya pamoja kupitia ushirikiano wa kisiasa, biashara, uwekezaji, elimu, utamaduni na people-to-people exchanges.

Kwa miaka kadhaa, ubalozi wa Kenya ulioko Havana ulikuwa ukisimamia pia uhusiano na Jamaica pamoja na nchi nyingine za Caribbean na Amerika ya Kati na Kusini, ikiwemo Guyana, Barbados, Dominican Republic, Haiti, Panama, Trinidad and Tobago, Venezuela, Colombia, Ecuador, Bahamas, Saint Vincent and the Grenadines na St. Kitts and Nevis.

Eneo la Caribbean lina umuhimu mkubwa kwa Kenya na bara la Afrika kutokana na idadi kubwa ya watu wenye asili ya Kiafrika wanaoishi huko. African Union inalitambua diaspora ya Waafrika kama "Africa's Sixth Region," jambo linalofanya ushirikiano na mataifa ya Caribbean kuwa sehemu muhimu ya diplomasia ya Afrika.

Ufunguzi wa mission hii pia unaendana na mkakati wa serikali ya Rais William Ruto wa kupanua uwepo wa Kenya katika mataifa mbalimbali duniani tangu ilipoingia madarakani mwaka 2022. Serikali inalenga kutumia diplomasia kuimarisha biashara, kuvutia uwekezaji, kuongeza ushirikiano wa kimataifa na kufungua fursa mpya kwa Wakenya.

Inatarajiwa kuwa High Commission ya Jamaica itatoa jukwaa muhimu la kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, elimu, utamaduni pamoja na ushirikiano katika masuala ya kimataifa kupitia taasisi mbalimbali za kimataifa.

Source: eastleigh.co.ke
 
Back
Top Bottom