Kenya: Pacha wawili waomba kuolewa na mwanaume mmoja ili wasitenganishwe. Jamaa akubali kuwaoa

Kenya: Pacha wawili waomba kuolewa na mwanaume mmoja ili wasitenganishwe. Jamaa akubali kuwaoa

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Huko Kenya, pacha wawili wamemuomba mwanaume mmoja awaoe ili wasitengane.

Pacha hao wenye miaka 20 wamesema hawataki kutenganishwa hivyo waolewe na mwanaume mmoja.

Bwana Oleman Learat mwenye miaka 26 amekubali kuwaoa Anna na Emily wenye miaka 20 ili tu wasitengane.

Soma mwenyewe hapa chini.

----
mapacha.png
Mtangazaji wa redio ya kijamii ya Wambaz ya nchini Kenya, Oleman Learat, mwenye umri wa miaka 26, amepanga kukimbia ukapera kwa kuoa wasichana pacha.

Pacha hao, Anne Samken na Emily Salaon (miaka 20), wameamua kuolewa wote na kijana huyo wakisema hawawezi kutenganishwa, kwa hivyo, wamekubaliana kwamba ni afadhali waolewe na mume mmoja.

“Nimeiambia familia yangu kuhusu nia yangu ya kuwaoa hawa pacha haijakataa lakini wanauliza maswali mengi,” Oleman ameliambia gazeti la Taifa Leo na kuongeza kwamba yeye anaona kama anaoa ‘msichana mmoja’ tu kwani wanafanana kwa kila kitu!

Japo Oleman anasema atawajengea kila mmoja nyumba yake katika boma moja, pacha hao ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha KCA cha jijini Nairobi wamesema itakuwa vigumu wao kukaa mbalimbali.

“Sisi hatujawahi kutenganishwa tangu tukiwa shule ya chekechea,” anaeleza Emily.

“Walimu walitutenganisha kwa mwaka mmoja tukiwa shule ya Sekondari mwaka wa 2021 (wakiamini ndio tutafanya vizuri katika masomo) lakini tuloishi kwa huzuni na upweke sana.”

Oleman anasema alianza uhusiano na warembo hao mwaka jana 2023 na kwamba mwanzo ilikuwa ngumu kuwatofautisha lakini sasa anaweza kuwatofautisha, hasa kwa namna wanavyoongea.

Mwanahabari Oleman amesema alikutana kwa mara ya kwanza na pacha hao katika hafla za burudani na kuvutiwa nao.

“Niliona wanafanana kwa kila kitu. Ukiuliza swali, wanajibu pamoja. Nikaanza kuwachumbia na wakanipenda. Kimsingi huwezi kuongea na mmoja akamtenga mwenzake. Kwa hiyo hata nikipiga simu, lazima niwajumuishe wote wawili,” amesema.

Chanzo: Taifa Leo
 
Hawana gharama hawa unajenga nyumba moja tu, ndani unaweka mchele kilo 100, unga kilo 50 inabaki kazi ya kutafuta mboga na kubadilisha chakula siku mojamoja.

Sijapenda tu style yao ya kusuka wangesuka twende kilioni wangependeza sana.
 
Nilishuhudia mshkaji mmoja alitaka kuoa na mchumba akasema siwezi kumuacha rafiki wa damu damu, tulieishi tangu utoto kwa hiyo tuoe wote
Jamaa akawaoa wote 2
Tatizo likaanza walipochangia mme
Haikufika hata miaka miwili, mmoja wao akasema nimechoka ku share mme
Akaomba talaka mwenyewe
Nafikiria tu na sio mchawi
Niko hapa
 
Back
Top Bottom