KENYA: Serikali imeendelea kuvifungia vituo vya Runinga ikiwa ni siku nne toka Mahakama Kuu iamuru vifunguliwe

KENYA: Serikali imeendelea kuvifungia vituo vya Runinga ikiwa ni siku nne toka Mahakama Kuu iamuru vifunguliwe

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971

Serikali bado imegoma kivifungulia vituo vya runinga nchi humo ikiwa ni siku ya nne toka Mahakama Kuu iamuru vituo hivyo kufunguliwa.

Serikali inasema haijachukua uamuzi wa kuvifungulia kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea juu ya urushwaji wa tukio la uapishwaji kwa Raila Odinga ambalo ni kinyume cha sheria. Hata hivyo Serikali haikuzuia tukio hilo

Vituo hivyo vya runinga vya NTV, Citizen TV na KTN vilifungiwa siku ya tarehe 30/01/2018 ambapo vilikuwa vikirusha moja kwa moja tukio la kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani (NASA) kama Rais wa Watu wa Kenya

Asasi za kiraia nchini humo zimekea na kusema ni tukio lisilo kubalika ikiwa kazi ya vituo vya habari ni kuripoti habari na tukio ambalo Serikali yenyewe iliruhusu na kuacha litokee. Pia ni kinyume cha sheria kufungia vituo hivyo bila kuvipeleka Mahakamani

Rejea hapa: NAIROBI, KENYA: Mahakama yaamuru Televisheni zilizofungiwa zifunguliwe
 
Baba wa demokrasia Uhuru Kenyatta. Hongera kwa kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na mahakama. Hii ndio demokrasia, nchi nyingine zijifunze toka kwako.
 
Watanzania kwa unafik bana. Kama demokrasia ya rais Uhuru Kenyatta hamuipendi si muige ya Jacob Zuma? Au ya Mohammed Fatah Al-Sisi au hata ya Buhari? Aliyelazimisha muige chochote kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta ni nani? Swali langu kuu, sisi wakenya nasi tutaiga demokrasia ya nani? Mnaponda chochote kizuri kutoka Kenya ila mabaya mnayafurahia sana. Team roho mbaya!
 
Huku Tanzania tunaambiwa tuige ya kwenu Kenya.
 
Huku Tanzania tunaambiwa tuige ya kwenu Kenya.
Waulize wanaowaambia muige vya Kenya kwanini musiige vya nchi nyingine. Sisi huku Kenya hatuigi vya Tanzania, wala sijasikia yeyote ule akituambia tuige vya nchi yeyote ile.
 
Da MANGE ficha my Id[emoji1] [emoji2]
 
Waulize wanaowaambia muige vya Kenya kwanini musiige vya nchi nyingine. Sisi huku Kenya hatuigi vya Tanzania, wala sijasikia yeyote ule akituambia tuige vya nchi yeyote ile.
Wanaotuambia tuige ya kenya ni kakikundi fulani ka siasa hapa tz kanajiita ukawa...sifa yao kubwa ni unafki!
wao pia ni maarufu kupinga kila anachofanya magufuli.
kwa ufafanuzi huo nadhani umenielewa
 
Wanaotuambia tuige ya kenya ni kakikundi fulani ka siasa hapa tz kanajiita ukawa...sifa yao kubwa ni unafki!
wao pia ni maarufu kupinga kila anachofanya magufuli.
kwa ufafanuzi huo nadhani umenielewa
Asante
 
Ni safi kabisa kuna watu walisema tujifunze demokrasia kutoka kwa wakenya, haya hii ndo elimu ya Kenyatta.
Hapa tuwe waangalifu-kuna katiba na utekelezaji wa hiyo katiba. Binafsi naipenda katiba ya Kenya ukilinganisha na hii ya kwetu Tz (ambayo hata JKN alishasema ni rahisi kutengeneza dikiteta kwa katiba hii). Kujifunza toka Kenya haina maana ya Kenyatta lazima yawe mazuri. Kuna vitu katiba inamlazimishe afanye au apelekwe kwa pilato.
 
Mbna hajafungulia vile vituo kama alivyoamrishwa na mahakama, ni kipengele gani kinachompa nguvu ya kuidharau mahakama, kma cyo kwamba rais yupo juu ya mihimili yote kama huku kwetu mkuu?
 
Tuliambiwa tuige ya baba wa demokrasia,sa wenye vyombo mjipange
 
Safi sana unajua kuna kujidanganya mambo ya mihimili mitatu hiyo nadharia haipo. Rais ni juu ya kila kitu sio kuichokoza serekali unakimbilia mahakamani anbako nako wanangoja huruma ya Rais wapate kula.

Kenya ilishataka kuwa Jamuhuri ya Kambale sasa kila mtu anasharubu safi sana Kenyatta
 
Mbna hajafungulia vile vituo kama alivyoamrishwa na mahakama, ni kipengele gani kinachompa nguvu ya kuidharau mahakama, kma cyo kwamba rais yupo juu ya mihimili yote kama huku kwetu mkuu?
Raisi anatumia ubabe na siyo kwamba yuko juu ya mihimili yote. Sisi Raisi akivunja katiba wengi wetu tunalalamika tu, kwa nchi nyingine kitu kama hicho huamzisha maandamano kwenda mbele na manung'uniko yatakayo mfanya Raisi achue corrective action au ajiuzulu. Huwezi ukavunja katiba au sheria ukawa salama. Ndo maana kuna impeachment-Mugabe war veterans walipomgeuka alijua lazima atasalim amri, kwa wenzetu wananchi wakisema basi-basi inatosha. Katiba nzuri inasaidia lakina haihakikishi chochote kama maoni ya wananchi hayaheshimiwi.
 
Back
Top Bottom