Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Serikali bado imegoma kivifungulia vituo vya runinga nchi humo ikiwa ni siku ya nne toka Mahakama Kuu iamuru vituo hivyo kufunguliwa.
Serikali inasema haijachukua uamuzi wa kuvifungulia kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea juu ya urushwaji wa tukio la uapishwaji kwa Raila Odinga ambalo ni kinyume cha sheria. Hata hivyo Serikali haikuzuia tukio hilo
Vituo hivyo vya runinga vya NTV, Citizen TV na KTN vilifungiwa siku ya tarehe 30/01/2018 ambapo vilikuwa vikirusha moja kwa moja tukio la kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani (NASA) kama Rais wa Watu wa Kenya
Asasi za kiraia nchini humo zimekea na kusema ni tukio lisilo kubalika ikiwa kazi ya vituo vya habari ni kuripoti habari na tukio ambalo Serikali yenyewe iliruhusu na kuacha litokee. Pia ni kinyume cha sheria kufungia vituo hivyo bila kuvipeleka Mahakamani
Rejea hapa: NAIROBI, KENYA: Mahakama yaamuru Televisheni zilizofungiwa zifunguliwe