KENYA: Serikali yatishia kuvifungia vyombo vya habari vitakavyotangaza kuapishwa kwa Odinga

KENYA: Serikali yatishia kuvifungia vyombo vya habari vitakavyotangaza kuapishwa kwa Odinga

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
ODINGA.jpg

Serikali ya Kenya imeviamuru vyombo vya habari kutopeperusha mubashara kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani (Nasa) kama “Rais wa Wananchi” ambako kumepangwa kufanyika Januari 30, 2018, chombo cha habari cha binafsi NTV kimeripoti.

“Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto wamefanya mkutano wa pamoja na Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i, Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Kiteknolojia Joe Mucheru na Mwanasheria Mkuu Githu Muigai kwa lengo la kuvitaka vyombo vya habari kujizuilia kutangaza kuapishwa kwa Raila Odinga na Kalonzo Musyoka kuliko andaliwa na Nasa,” NTV imeripoti.

Televisheni imesema kuwa mkutano huo ulikuwa umefanyika katika ikulu ya rais Januari 26, muda kidogo kabla ya Kenyatta kutaja majina ya baraza lake la mawaziri.

“Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wakurugenzi; Rose Kimotho wa Kampuni ya habari Three Stones Media, Cyrus Maina wa Kituo cha radio cha Capital FM, Ian Fernandez wa Kituo cha habari K24 na mkurugenzi wa Kampuni ya Nation Media Group Tom Mshindi,” ripoti hiyo imeeleza zaidi.

NTV imesema kuwa serikali imeonya kuwa wale watakao tangaza sherehe hizo za kuapishwa ambazo ni “kinyume cha sheria” huko katika eneo la Uhuru Park vituo vyao vitafungiwa.

Nasa imeahidi kukaidi amri ya serikali inayopiga marufuku kuapishwa huko.

Upinzani umesema utaendelea na sherehe hizo za kuapishwa huko eneo la Uhuru Park katika mji mkuu wa Nairobi, pamoja na mamlaka husika kusema kuwa eneo hilo limefungwa kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati kwa kipindi hadi katikati ya mwezi wa Februari.

Chanzo: VOA
 
Fungua tv citizen ,ktn wote wapo live wanafatilia kuapishwa Raila. Nidhamu ya woga Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Tweende kaaaziiii
Tweendeee skumaaa
Tweeeeeendeeee
 
Waache 'baba' aapishwe kwa amani tu awe rais. Yote yaishe wakenya tuendelee na maisha kama kawa bila huu mvutano wa kisiasa.
 
Citizen tv shut down..also ntv off on free to air platforms...
 
. Fungua tv citizen ,ktn wote wapo live
wanafatilia kuapishwa Raila. Nidhamu ya
woga Tanzania.
Hehehe bado unaendelea kupata matangazo citizen na ktn hehehe nidhamu ya uoga hoyeeeeeee
 
Hehehe bado unaendelea kupata matangazo citizen na ktn hehehe nidhamu ya uoga hoyeeeeeee
Kwa taarifa yako CITIZEN ,NTV, KTN wapo live utube . Serikali imefunga mfumo wa transmission kufikia free to air channels.Kalanzo ameondoka nyumbani kwake Karen anaelekea Uhuru Park. Live bila chenga citizen tv ktn news. Happening now live ndungu yangu.Kenya siyo Tanzania.
 
Kwa taarifa yako CITIZEN ,NTV, KTN wapo live utube . Serikali imefunga mfumo wa transmission kufikia free to air channels.Kalanzo ameondoka nyumbani kwake Karen anaelekea Uhuru Park. Live bila chenga citizen tv ktn news. Happening now live ndungu yangu.Kenya siyo Tanzania.
Serikali imefunga hizo TV haijafunga youtube au Unafanishaje TV na youtube? TV zimefungwa hazijafungwa? Kalonzo hajatoka labda huyo alietoka ni Kalonzo wako wewe hakuna Kalonzo Uhuru Park acha uongo
 
Back
Top Bottom