KENYA: Shambulio la Al Shabaab laua Maafisa 5 wa Jeshi la Polisi

KENYA: Shambulio la Al Shabaab laua Maafisa 5 wa Jeshi la Polisi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Maafisa nchini Kenya wamesema maafisa watano wa polisi wameuawa leo kufuatia shambulizi ambalo limefanywa na washukiwa wa kundi la itikadi kali la Kiislamu karibu na mpaka wa nchi hiyo na Somalia. Maafisa hao waliuawa wakati washukiwa hao wa kundi la Al Shabaab walipovivamia vituo vya polisi karibu na mji wa Lafey jimbo la Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Afisa mkuu mshirikishi wa serikali katika eneo hilo Mohamud Saleh amethibitisha kisa hicho akisema shambulizi hilo lilifanyika asubuhi ya Ijumaa. Mtambo wa kuwezesha mawasiliano ya simu pia uliharibiwa kabla ya shambulizi hilo.

======
Four police officers and a reservist have been killed after al-Shabab attack in Fino area, Mandera. The militants also hurled a hand grenade to Safaricom mast to cripple communication in the area.

The more than 50 heavily armed militants attacked the camps at the border town of Fino, Lafey sub-county before retreating back to Somalia just five km away.

The confrontation lasted for close to three hours. Several other officers were injured during the 2 am attack.

"The injured officers whose number was not immediately established were rushed at Fino dispensary for treatment before being airlifted to Nairobi for specialized treatment," North Eastern regional commissioner Mohamud Saleh said.

Saleh said the terrorists were revenging Tuesday's killing of 40 militants by KDF in Fafadul area, Gedo region in Somalia.

Among the killed were two senior commanders. “We suspect that this rag tag militants were on a revenge mission following the heavy casualties they suffered in the hands of our troops,”Saleh said.

“We have accounted for all our officers at the two camps of AP and regular police. We are in pursuit of the militants some of whom sustained injuries following the heavy exchange of gun fire,” Saleh said.

This is the third time the al Shabaab have attacked security installation in Lafey Sub County. Two weeks ago, three teachers were killed at Qarsa primary school in similar attacks.

Source: The Star Kenya
 
Kenya inapitia nyakati ngumu sana lakini! Poleni ma askari mliopatwa na Janga
 
Poleni sana wakenya..!

Nashindwa kudadavua ni kwanini kenya mna uhasama na al-shabab?

Mwenye kujua anijuze..!
 
Nilifikiri wamekufa hawa wetu kama ni Kenya poleni sana
 
Who among the two is Jon Snow(10marks)
game-of-thrones-season-7-episode-6-leak-jon-snow-s-captured-wight-s-identity-revealed-230004.jpg
 
Itakua ni kisasi..ila hili kundi kama linaoungua nguvu hivi..
 
Halafu wakifanya tukio wanabeba silaha??tuanzie hapo kwanza
 
Mimi kinachonishangaza ni kwamba, mbinu wanayotumia ni hiyo hiyo mara zote na wanafanikiwa, Kenya ni vichwa ngumu sana kujifunza kutokana na makosa ya nyuma. Njaa nayo ni hivyo hivyo, kila mwaka wanasingizia ukame, sasa kwanini msijiandae mapema kama mnajua Alshabaab wanakawaida kushambulia vituo vya polisi vilivyoko mipakani nyakati za Usiku?. Nigeria nao ni hivyo hivyo, wanafunzi wa shule za Bording kutekwa na Boko haram.
 
Hata wakijitayarisha bado ni vigumu kwa sababu maafisa wa polisi ni wachache lakini Al shabaab ni wengi. Watu wengi wanapita mipakani kila waki na huwesi jua nani Al Shabaab na nani refugee. Na hawa Al shabaab nimeona wanashambulia kwa wingi kwa hivyo hata ukijitayarisha na askari kumi bado mtashindwa na Al Shabaab hamsini.
 
Kaka ninakuomba uniruhusu nikupinge kwa nguvu zote, Polisi wa Kenya wanawazidi kwa idadi Alshabaab zaidi ya mara tano, ukichukua idadi ya polisi na KDF inaweza kuwazid Alshabaab zaidi ya mara kumi. Inakisiwa kwa sasa Alshabaabu hawazidi elfu 4, wote kwa ujumla, ndiyo sababu hawapigani vita wanavizia na kukimbia.

Hivi vituo vya polisi huko mpakani havizidi mia moja,, kwanini nchi nzima ishindwe kulinda hivi vituo?, au eneo zima la kaskazini mashariki mwa Kenya, linaukubwa kiasi gani kwa nchi kuweza kudhibiti usalama wa eneo hilo?.
 
Back
Top Bottom