Tatizo la wakenya kujenga TAVETA Airport siyo challenge kwa serikali kuboresha uwanja wa ndege wa KIA tu. Wakenya wamefanya tathmini ya mambo mengi sana ambayo yatawaletea faida kubwa kutokana na biashara ya utalii hasa kwenye mlima wa Kilimanjaro. Wanataka waweze kupokea watalii wote watakaokuwa na nia ya kutembelea mlima Kilimanjaro, kwani wataweza kushukia hapo mpakani holili kwa urahisi na watatumia uwezo wao mkubwa walionao kutuzidi katika matangazo. Pia bila shaka watajenga Hotel za kimataifa zenye huduma bora kuliko za kwetu, hivyo wataweza kukaa na watalii mudawote na kuwaleta Tanzania kwaajili ya kupanda mlima na pindi wakishuka moja kwa moja wanaelekea kenya. Hii itatufanya tuambulie only park fee na kukosa mapato mengi kwenye mahoteli na biashara nyingine pia. Hivyo basi, serikali inabidi ifanye jitihada za kufanya maboresho makubwa katika uwanja wa ndege wa KIA kama ulivyopendekeza, tufanye jitihada kubwa zaidi za kujitangaza kiutalii ikiwemo mlima Kilimanjaro ambao wengi wakijua upo Kenya kutokana na wakenya kujitangaza sana, pia kufanyike kufanyike maboresho katika mahoteli yetu hasa katika huduma. Tusipokuwa makini tutashindwa kupata mapato na kubaki kulialia tu kwa uzembe wetu wa kutotaka kufikiria na kuona mbali.