Kenya vs Tanzania: Mbona Kuna Chuki?

Kenya vs Tanzania: Mbona Kuna Chuki?

Tanzania nimepaishi miaka kadhaa, na nimekatiza mikoa mingi na wilaya nyingi, nimeingia maeneo mengi sana huko na kuhititmisha kwamba kuna aina tofauti tofauti za Watanzania.
- Kunao ambao walikaririshwa mambo fulani fulani dhidi ya Wakenya tangu enzi za ujamaa, hawa hata ufungue nyuzi ngapi humu hawatabadilisha mawazo na mitazamo yao, ni wazee wazee na cha kuhuzunisha walipokeza mitazamo ya kihivyo kwa watoto wao. Hawa walikaririshwa kwamba Kenya ilijengwa na mzungu na ndio sababu imewashinda kiuchumi hadi leo.

- Kuna wale japo huiskia Kenya, lakini ukimuuliza iko upande gani kwenye ramani hawana habari, hawa hujifanya wajuzi sana wa masuala ya Kenya, na wapo hata humu JF. Sampuli ya hawa utawakuta vijiweni Tanzania wakiijadili Kenya, nilikua nakaa pembeni kuwaskliza hadi naishia kicheko.

- Kuna ambao kwa kweli wanaipenda Kenya, hawa aidha wamewahi kuishi na kusomea Kenya maana kila nikijadili nao walikua wanaonekana kuwa na habari za Kenya hadi za hivi punde. Unakuta Mtanzania anawajua wabunge wetu hata kunizidi, anaweza akaongea siasa za maeneo kama Nyandarua, Trans Nzoia n.k. yaani maeneo ambayo hata mimi binafsi sina habari nini kinaendelea huko, wa hivi nilikua na urafiki nao sana na mpaka leo huwa tunapigiana simu.

- Kuna wengine japo wamewahi kuishi Kenya, lakini kuna kituko kiliwatendekea wakaishia kulea chuki dhidi ya Kenya, aidha alinyang'anywa bidhaa, au kiwanja au fursa fulani, kuanzia hapo akaanza kuishi full majungu na machungu dhidi ya Kenya, na wapo humu.

- Kuna sampuli ya wengine ambao walizembea kazini kwao huko halafu Wakenya wakaalikwa na kuajiriwa kwenye hizo nafasi, unakuta mwajiri Mtanzania ameamua kumlipia Mkenya au Mhindi gharama zote za usafiri, makazi, vibali vyote ilihali ameacha Watanzania wenzake. Sasa hapa jamaa wanaishia kulea chuki na hawawezi kubadilika hata ufanye nini.

- Kuna wengine ambao hutuchukia kwa ajili ya uwezo wetu wa kuongea kingereza ilhali wao wamehangaika kwa muda mrefu, unakuta tukiingia vikao ambavyo kingereza ndicho kinatumika, inakua rahisi kuwajua Wakenya humo ndani maana wanaonekana kujiamini na waongeaji ilhali Watanzania kimyaaa. Vikao vya namna hii nilivihudhuria sana, Watanzania walikua wanalea chuki japo kimya kimya.

- Lakini pia humu JF kuna wale ambao ni mamluki wa CCM, hawa hukesha humu wakiponda Kenya, wao hawana chuki lakini wapo kikazi zaidi. Awali nilikua najadili nao lakini nilipogundua kwamba ni kama robots, yaani kazi yake haimruhusu kuwa na mtazamo tofauti, hivyo hata kama uko sahihi kivipi hatokubali hata kama uzi utaishia kwenye kurasa ishirini, ikabidi niwe nawakwepa.

Zaidi ya yote, kuna Watanzania wazuri tu, mnahusiana nao vizuri hawana chuki wala nini, tena wachapa kazi nimefanya nao kazi, wana uzalendo wa Kiafrika, yaani wao hupenda kuona maendeleo kwenye nchi yoyote ya Afrika. Na hutawakuta wakichangia kwa chuki, wao hutoa hongera wanapokumbana na hatua zozote chanya zitakazoikomba Afrika kiuchumi. Wapo wa hivi humu lakini wachache sana.
Niaina gani yawatu walio wengi from your list? To what extentent to they talk about the country.. will like to know.
 
Unahangaika wakenya ambao hata hiyo nchi tunaweza kufanya koloni letu pambafu kabisa hamjui kipindi cha ukoloni tz ikukuwaga mashamba na wakoloni wakimaliza kulima wanakuja kenya kutumia pesa williamson muanzili wa mwadui alikuwaga anakuja kunywa tea kwa ndege nairobi anarudi kuchimba hamuoni aibu kushindana na kushidwa na manamba wenu kipindi cha ukoloni
Wewe mleta mada unaona huyu ndugu yako anavyotiririsha povu kiasi hiki, unataka sisi tufanye nini kwenye situation kama hii.? Lazima ale za uso huyu nyangau kabisa
 
Sina cha kuongeza, Kenya inabidi ichague kushirikiana na USA au kushikamana na nchi zingine za EA, Kagame, Mseven na Magufuli walishasema hawatotushwa na vitisho vya Marekani katika hili, at least Kagame na uncle Magu ninawajua wakisema wamesema, hata uwachinje hawawezi kubadilika, tutaona mwisho wa Kenya katika hili.
Every country acts in the interests of it's Citizens. Kenya Export to the U.S under Agoa is very big hence cannot afford to loose the market.

Kweli nyani haoni Kundule, Tz more than one's has blocked Kenyan businesses to Tz citing 'protecting local companies'.

Kenya is the leader in the region and cannot follow...
 
Every country acts in the interests of it's Citizens. Kenya is Export to the U.S under Agoa is very big hence cannot afford to loose the market.

Kweli nyani haoni Kundule, Tz more than one's has blocked Kenyan businesses to Tz citing 'protecting local companies'.

Kenya is the leader in the region and cannot follow...
Tatizo akili zenu hazina akili, nani kasema msilinde maslahi yenu?, mbona sisi tulikataa mkataba wa EPA kwa kulinda maslahi yetu, tatizo ni pale mliposaini na kukubaliana na mkataba huo, lakini mara baada ya vitisho toka US, mkajitoa, hilo kamwe hamtoeleweka na lazima mtalipia gharama ya huo usaliti wenu, mngekataa toka mwanzo hakuna mtu angelalamika.
 
Vipi mleta mada mount Kilimanjaro na oldvai mshavirudisha tuliwaachia mtambe kuwa vyenu ila sisi ndugu tunatgemeana tangu enzi za mzee kenyata na nyerere mkizingua watz pia watawazingua hongereni mliwahi kupata exosure
 
Tatizo akili zenu hazina akili, nani kasema msilinde maslahi yenu?, mbona sisi tulikataa mkataba wa EPA kwa kulinda maslahi yetu, tatizo ni pale mliposaini na kukubaliana na mkataba huo, lakini mara baada ya vitisho toka US, mkajitoa, hilo kamwe hamtoeleweka na lazima mtalipia gharama ya huo usaliti wenu, mngekataa toka mwanzo hakuna mtu angelalamika.

Unajua nimarangapi Tz imekiuka mikataba ya E.A??? Your hate makes you short sited...
 
Unajua nimarangapi Tz imekiuka mikataba ya E.A??? Your hate makes you short sited...
Naomba ulete kwa ushahidi ni mkataba gani Tanzania tulisaini kisha baadae tukajitoa, hiyo siyo tabia ya Tanzajia hata kidogo, sisi tunakuwa wagumu sana katika kukubali na tunachukua muda mrefu sana kufikia maamuzi, lakini tukishafikia maamuzi haturudi nyuma, hii ni kinyume kabisa na Kenya, ambayo inakubali kila mikataba haraka sana, na kuivunja hiyo mikataba kirahisi sana.
 
Acheni kulialia hapa JF, Wakenya mnaadika kama vile nyinyi ni watakaifu. Hakuna cha utakatifu wala nini, ukweli ni kwamba wakenya hampendi kushirikina na wenzenu kama hakuna pesa mbele. Hakuna hata siku moja utasikia msemo huu kutoka kwa Mkenya "kizuri kula na ndugu yako", wengi wenu mnatuambia kila mara Kenya haina undugu kwenye biashara, haya sasa, Uganda, Rwanda, Tanzania Buruindi S.Sudan wanajivuta pembeni mpaka mjielewe kama majirani zenu wana thamani kubwa kwenye ustawi wenu.

Msimamo wa Kenya bado utabaki huo huo, biashara haina undugu ila maslahi, hebu wapelekee hao wafanya biashara wa Dar hayo mambo yenu ya undugu uone kama hamtawafilisi ndani ya wiki moja.
Ufahamu kuwa Mrundi anatoka mbali sana na kuja kutumia bandari ya Kenya na kusahau undugu wenu naye kwa sababu anapiga mahesabu ya kibiashara, vivyo hivyo Mtanzania anayetokea Kaskazini anatumia huduma zetu maana ndizo ninamfaa kibiashara. Mboreshe huduma na muache uzembe wa kutegemea undugu.

Sijaelewa hapo unasema tunatengwa na majirani wakati takwimu zinaonyesha asilimia ya mahusiano yetu ya kibiashara na majirani wetu wote zinaongezeka. Biashara ni sayansi, hamna cha hisia au pumba za kuitana ndugu.

Halafu nimesema mara nyingi humu, Watanzania tumeunganishwa nao kwenye kiuno hata kama hatuna undugu hatuwezi kuwakwepa, nenda kafuate tarakimu za uhamiaji wakuambie idadi ya Watanzania wanaoingia Kenya imezidi wanaoenda kwenye mataifa mengine mliopakana nao, ipo siku mtafunguka na kupanua ufahamu na uelewa.
 
Tatizo unatoka kwenye nchi iliyo katoka vipande vipande, tukiacha nyinyi wa magharibi wenye roho mbaya na wapenda pesa, watu pwani wala hawama roho mbaya. Mpaka Islamic bank wamewaleta mnakopa bila riba.

Majirani wanawatenga kwa kutokuelewana kwa sera ya biashara ya nje. Mnalabiliwa na maamuzi magumu na majirani wamesha weka msimamo wa kutokurufi nyuma. EPA, Mitumba, mpaka tariffs.
 
Hatutaki watu wanaojikomba kwetu kwa madai ya kufunganishwa kwenye kiuno, mbona wazungu wanatemebelea Kenya kwa wingi lakini hamsemi wamefunganishwa kwenye viuno, mbona wasomali hamjafunganishwa kwenye viuno na wamejaa hapo Kenya?, mnaitegemea Tanzania kwa sana na ndiyo sababu wakenya wengi wanakuja kutembea Tanzania na investors wa Kenya wamejazana kutafuta biashara baada ya kuona uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi wakati wa Kenya unaporomoka, Kenya needs Tanzani badly my friend.
 
Kwa kweli mimi kama mtanzania nikiona mtz anatukana wakenya najiskia vibaya sana. Hakuna taifa tunalofanana nalo na kuwa na ukaribu nalo kama Kenya. Tunashea nao hadi makabila mfano masai na wajaluo. Pia tuna mpaka mrefu nao kuliko taifa jingine lolote. Binafsi nilipokua ughaibuni wakenya ndo walikua marafiki zangu na tuliishi kama ndugu.
 
We unajua nini???
Unajua kitu kinaitwa COW figisu ambalo lilitokea hadi ccm na upinzani Tanzania wakataka serikali ijitoe EAC ??? Unajua histori ya Kenya kuusu ukombozi wa bara la Africa hadi Leo ukitaja mkenya South Africa wanaona umewatajia mzoga wa mbwa unajua Kenya iliunga mkona makaburu dhidi ya wazawa wa afrika kusini yako mambo mengi sana toka kale wakenya ni wahuuni wahuuni tu
 
Back
Top Bottom