Mimi nafkiri watanzania tuache ligi ya mabishano na Kenya, tujikite na ishu zetu za ndani, wale jamaa wapo hatua kadhaa mbele kuliko sisi.
- Sekta ya elimu wametuacha.
- Sekta ya siasa wametuacha, sisi upinzani ulifutwa kabisa bungeni na bado tukaweka matako chini. Mtu akaamua kufuta matokeo ya uchaguzi zanzibar na bado tukampa heshima.
- Maisha yanapanda kasi sana bila ya sababu za msingi, mfumuko wa bei ktk mahitaji yetu ya msingi unaendelea kupaa, wakulima bado wana hali ngumu.
- Nishati ambayo ingekuza viwanda kwetu imekuwa ni shida.
- Tumeshindwa kuendesha bandari n.k
Muda wa kubishana na Wakenya ni heri tuwekeze mitandaoni ili kuonesha serikali hatufurahishwi na utendaji wake.