Kenya: Wabunge kuanza kutumia lugha ya Kiswahili Bungeni kila Alhamisi

Stop being much pesmism bro.
Optimistic pays much.

#YNWA
 
[QUOTE="MK254, post: 37315485, member: 1424


wewe unashangaza sana, bado umeshikilia tu hiyo research yako ya uongo, kwa taarifa yako sio kila research inatakiwa kufuatwa kwani kuna baadhi ya research hufanywa na watu wanaotaka pesa au wanaotafuta academic certificates nk.

Sasa jifunze tofauti kati ya haya maneno; kujua na kujifunza, ni hivi; kujifunza ndiko kunakomfanya mtu aweze kuongeza uwezo wa akili yake na sio kujua, katika kujifunza mtu anakuwa anafanya Mental exercises, na katika kujifunza mtu ndipo anajua.

Sasa mtu anajifunza vitu vingi sio lugha pekee, hivyo ni katika kujifunza ndipo mtu anaongeza uwezo wa akili na sio katika kujua kitu chochote ikiwemo lugha.

Waarabu mental exercises wanaita; تمارين عقلية, kama ingalikuwa kujua lugha uwezo wa akili unaongezeka basi yule Muamerika mweusi anayejua lugha zaidi ya 20 angalikuwa ni Genius katika katika mambo mengi sana.

Nasema tena unapokuja na jambo la kuokota lifanyie kazi kwanza na ule ushibe ndipo ulilete hapa, kula na ushibe kwanza kwani Nyinyi na njaa ni marafiki , No sense without food.

Angalia;
 

Sio mimi nimeshikilia, ila ndio uhalsia ulivyo, tafiti zimefanywa nyingi na zote kubaini binadamu wanaofaulu kuongea zaidi ya lugha moja wanaboresha uwezo wao wa kufikiri, wanatanua upeo wao na kimtazamo, ila mazwazwa wanaoganda kwenye lugha moja huwa wanakua kama wanakijiji ambao hawajafaulu kutoka nje ya kijiji chao.

Jiulize Tanzania licha ya kuwa na kila kitu, raslimali za kila aina, madini ya kumwaga, ardhi kubwa yenye rotuba nzuri tu, yaani kila kitu lakini bado inatajw kwenye maskini wa kutupwa, wazembe wa kutumia ubongo, mnashindwa na kainchi kadogo kama Kenya, leo hii kiuchumi Kenya nusra iwpige mara mbili, tumewazidi kwenye kila kitu, kielimu, kijeshi yaani vyote, mpo hovyoo hadi mnatia huruma.
 
Hv mtaelewana kweli [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] maana huwa nikiwasikiliza nacheka
 

mbona bado u mjinga kiasi hiki,mbali na kujua kuongea kiingereza!!!
 



Kwakweli mimi ninakushangaa kushupalia tafiti za kipuuzi zilizofanywa na mzungu au yawezekana kwa udogo wa akili yako umeshindwa kumuelewa huyo mtafiti.

Narudia, kwa faida yako na faida ya huyo mtafiti wako, Lazima ujue tofauti kati ya hivi vitu viwili: 1-kujifunza na 2-kujua. Unapojifunza ndipo unapoipa akili yako mazoezi na hapo ndipo inapoimarika na ukishajifunza yaani ukishajua hicho ulichojifunza hapo tena akili yako haiimariki tena, sasa wewe unashikilia kwamba KUJUA na sio KUJIFUNZA lugha ndipo akili inaimarika!!!, hiyo sio kweli ni uongo, hivi unashindwa hata kutumia your common sense on the issue??? Unapotezwa na tafiti za kijinga!!!, Hi black man restore your sleeping senses. ---- Sasa ni hivi; kujifunza kupo kwa aina nyingi, mtu anaweza kujifunza Hesabu, na masomo mengine kama Physics na mambo mengi kadha wa kadha hiyo yote ni Mental exercise sio tu katika KUJIFUNZA lugha pekee ndipo akili ya mtu huimarika, Zingatia maneno:- Kujua na kujifunza, ili akili ifanye kazi vyema inahitaji Exercises, mtu anapojua kitu that is not a mental exercise but only learning.

Unataka kudanganya umma eti Wachina, warusi, na wajapani wengi wanajua kiingereza!!, huo ni uzandiki, sio kweli, hao wanapenda sana lugha zao na ndiyo maana wamezifanya kuwa ni medium of instruction katika nchi zao, wao sio watumwa na brain washed kama nyie kukumbatia Kiingereza na kuacha lugha yenu nzuri ya kiswahili na huo ni aina fulani ya Slavery.

Unasema tumeganda kwenye lugha moja na ni uzembe!!, nasema wewe unasumbuliwa na kasumba ya kiingereza kwamba mtu asiyejua kiingereza basi ni dhalili, mjinga na mzembe, kwani hujui mkataa kwao ni mtumwa, wewe ni mtumwa wa waingereza na inaonekana ungalikuwepo katika zama za kudai uhuru wa Kenya bila shaka ungalikuwa msaliti na kibaraka dhidi ya Waafrika wenzako, usingependa Waingereza waondoke, angalia sisi tunajivunia Kiswahili na Lugha zetu za asili, kiswahili ni lugha ya pili kwa ukubwa Africa, kiswahili leo kipo AU na kinasambaa Africa nzima na duniani kote, sasa unatokea wewe kibaraka wa wazungu na kudai kwamba kujua kiingereza kunaongeza akili!!! What a stupidity !!,--- kwa hiyo Wakikuyu, Wajaluo, Wakamba, Wakalenjin nk, wanaojua hizo lugha zao za asili pekee hawana akili??, au huko kwenu wakenya wote wanajua Kimombo pekee???, haya tufanye wanajua hizo lugha zao za asili na kiingereza pia, sasa kuna tofauti gani kati ya Wtz Wanaojua Kiswahili na Lugha zao za asili na hao nduguzo???, In that case We are all bilinguals therefore none among all of us should stand condemning and contempting the other.

Eti, Viongozi wetu wameshindwa kwenda nje kwa kutojua Kimombo!!!, (that's a nonsensical stereotype) kwani Kiongozi wa China alipokuja hapa Tz aliongea kiingereza?? au imesemwa kiongozi wa Africa anaposafiri kwenda nje lazima ajue kiingereza na lazima akifika huko aongee kiingereza???, au kuongea kiswahili awapo nje ni haramu??, huko nje hakuna watu wanaojua kiswahili??, Je hakuna wakalimani??, Mbona Wakenya wengi ndio wapo huko nje wakifundisha Kiswahili kibovu kwa wageni je hao nao ni wajinga??, je hawapati mkate wao kupitia hicho kiswahili unachokibeza???


Kumbuka mtu hujifunza mambo kwa haraka kupitia lugha mama kinachotakiwa ni lugha hiyo iwe imejaa elimu za kutosha, mfano Kiingereza , Kirusi, kijerumani, kijapani nk, hizo ni lugha mama zilizojaa elimu zinazotumika kufundishia respective natives na ndiyo maana hao natives wapo juu katika nyanja mbalimbali. Zamani katika karne ya 16-17 Lugha ya elimu ilikuwa Latin lakini Waingereza wakaona watu wengi hawajui Latin na hivyo walikosa nafasi ya kujua mambo mengi hivyo wakaamua kubadilisha na kuingia katika kiingereza; wakatafsiri elimu nyingi kutoka Latin kwenda kiingereza ndiyo maana leo kiingereza ni moja ya lugha kubwa za Elimu duniani.

Sasa ni wakati wetu sisi sote Wana Afrika mashariki kushirikiana kufanya kiswahili iwe lugha ya Elimu ni kupitia njia hii tutakuza vipaji na uelewa wetu wa mambo mbalimbali kwani a man understands /acquires better through his mother tongue language than through a learned language.

Kumbuka tofauti ya haya maneno; "kujua na kujifunza"---- mtu hakuzi akili yake akiwa kishajua kitu bali anakuza akili yake kipindi anapokuwa anajifunza na kuna aina nyingi sana za kujifunza vitu na mambo and on the course of the process /exercise a man strengthen his mental capacity and not the otherwise.
 

Mimi kawaida nikisoma sentensi ya kwanza nione mtu ameandika utopolo, huwa sihangaiki kusoma insha yote maana humo ndani hamna kikubwa zaidi ya pumba, umedhihirisha ukilaza wako kwenye hiyo sentensi ya kwanza eti unaponda tafiti zote zinazopigia upatu uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja kisa zimefanywa na wazungu.

Hata utumie nguvu nyingi kiasi gani, uzembe wenu wa kutokujua kingereza utaendelea kuwatesa sana, nimeishi Bongo miaka mingi sana na nimeshuhudia namna kutokujua kingereza huwatesa Watanzania, haswa walio maofisini, kwa nchi ambayo haijitegemei kwa chochote hata kiwanda cha sindano haina, kila kitu lazima muagize kutoka kwa "wazungu", hamna jeuri ya kutunisha misuli kwenye suala la lugha.
Binafsi napenda Kiswahili sana, lakini sijajiachia nigande kama zezeta kwenye lugha moja, naongea lugha yangu ya asili, pia naongea Kiswahili, Kingereza na zaidi naongea lugha kadhaa za asili za huku Kenya ikiwemo Kijaluo, Kiluhya na hata huko Bongo nilikua najifunza Kipare na Kihaya japo waongeaji ndio hawakua wengi, huko kwenu wengi hamjui kuongea lugha zenu za asili, hata salamu pekee zimewashinda kwa mlivyo wazembe, na Kiswahili chenyewe uandishi wenu hutia kinyaa, hamna hata lugha moja mliyoimudu.

Bure kabisa nyie watu... Sema Wabongo wachache wanaojua Kingereza huwa na maisha nafuu sana, sijakuta Mtanzania hata mmoja anayejua Kingereza halafu anahangaika ajira.
 


Mimi huwa sisomi habari nzima baada ya kuona neno la sentensi ya kwanza tu lilivyokuwa tenge.

Wewe ni mtumwa wa Kiingereza, Full stop. Mimi natumia kiingereza na kiarabu katika shughuli zangu lakini sio mtumwa wa hizo lugha, ninapenda kiswahili na lugha yangu ya kikabila kwa maana hiyo ninajua lugha 4, kwa fasaha zaidi ya zingine ninajua kiswahili.

Sijasoma utumbo wako hivyo naishia hapa.
 

Safi sana komea hapo na uzembe wenu huo, acha kuandika andika insha zisizodhihirisha matumizi ya ubongo, tutaendelea kuwashinda kwenye kila kitu hadi vizazi vyenu vya miaka zaidi ya 100 ijayo, haya kwaheri....
 
Safi sana komea hapo na uzembe wenu huo, acha kuandika andika insha zisizodhihirisha matumizi ya ubongo, tutaendelea kuwashinda kwenye kila kitu hadi vizazi vyenu vya miaka zaidi ya 100 ijayo, haya kwaheri....


Nawe komea hapo na upuuzi wako wa kitumwa kuabudu lugha za wenzako na kudharau lugha zako, utaendelea kuwa mtumwa wa watu weupe hadi siku ya kiyama.

Isitoshe nenda kajifunze mambo na uongeze uwezo wa akili yako finyu uliokufanya unukuu tafiti za kijinga nakuja nazo humu bila haya.

أنت مجنون
 

Lugha "zangu" ni moja tu, yangu ya asili, nyingine zote hizo nimeletewa nizitumie ili kuwasiliana na watu wasio wa asilia yangu, nikiwa kwetu natumia yangu ya asili kuzungumza na watu wa asili yangu, nikiwa nje nikutane na Wakenya wenzangu inabidi nitumie Kiswahili maana hawajui lugha yangu ya asili, nikikutana na majirani wote kasoro Watanzania, natumia Kingereza maana kinaninufaisha kwenye kuwasiliana nao, kinanipa uwezo wa kuwasiliana na watu wa mataifa yote dunani.
Nyie wazembe kimewashinda mumeishia ngonjera tu....eti kujua kingereza ni utumwa, hovyoo kabisa na bora muendelee kwenye huo uzembe maana ndio mtaji wa Wakenya wengi wanaoitwa huko kufanya baadhi ya kazi zinazohitaji ufahamu wa Kingereza.
 


Wewe ni hopeless, mimi sijasema kujua lugha nyingine ni utumwa, mimi mwenyewe najua Lugha tano 5, 1-- kiingereza, 2 kiswahili, 3 kiarabu 4, 2Vernacular languages.

Kama kujua kiingereza ni utumwa basi na mimi ni mtumwa!!!;

Mada ilianza kwa wewe kusema kwamba kujua lugha zingine kunaongeza uwezo wa akili (mental ability) na ukanukuu tafiti kutoka kwa mjinga mwenzako, mimi nikakupa somo usilolipenda kwamba kujifunza ndipo akili ya mtu huimarika na sio kujua na kujifunza kupo kwa aina nyingi sio kujifunza lugha tu.

Kilichofuatia ni wewe kudanganya umma kwamba Warusi, Wachina, Wajerumani, Waingereza, Wajapani wanajua lugha zaidi ya lugha zao ili kuunga mkono upuuzi wako kwamba kujua lugha zaidi ni kuimarisha uwezo wa akili, watu walio wengi wa hayo mataifa hawajui lugha zaidi ya moja na wapo mbele zaidi yenu nyie mnaotambia kujua kiingereza na hizo lugha zao ndio media of instructions katika nchi zao.

Ukaleta hoja ya kukejeli kwamba sisi ni wazembe na hatujui kiingerza kwa kushikilia kidwahili tu na ndio maana tupo nyuma nk, Mimi nikakupa hoja kwanba hata huko kwenu Wapo wasiojua kiingereza, wanajua kilugha na kiswahili tu na huku Tz ni hivyo wapo wanaojua kiswahili na vilugha tu sasa hapo nani wa kumlaumu na kumcheka mwenzake???.

Kuabudu lugha ya mwenzako ndiyo utumwa, unajifaharisha kwa kujua vizuri lugha ya mwenzako (japo nahakika bado huwezi kujua kama native Englishman ) na unasahau lugha yako Kiswahili inayokuwa kwa kasi duniani huo pia ni utumwa.

Mimi ni mswahili hasa na ndiyo maana natukuza kiswahili changu jinsi a native Englishman esteems his English language.

Acha hizo sterotype za kitumwa wewe ni mtu mweusi tii usijifanye mzungu.
 
Watuaribia lugha hao.
kipindi Magufuli ni waziri wa kilimo na uvuvi kuna mbunge mmoja wakenya alitamka"muheshimiwa wasiri wa kilimo na"uvivu"
 

Unazidi kuonyesha ulivyo bogus, unatumia nguvu nyingi kuandika hizi insha ambazo sizisomi maana nina uhakika zimesheheni pumba, sentensi moja ya kwanza imetosha nione ulivyo na upeo mdogo. Acheni uzembe mjifunze kuandika, kuongea na kusoma zaidi ya lugha moja hususan Kingereza maana ndio lugha ya dunia inayotumiwa kuunganisha dunia, leo Mchina akitaka kuuza bidhaa zake duniani, lazima ajifunze kingereza.
Ndio maana huwa mnapigwa sana kwenye mikataba ya raslimali zenu, kila kitu mnaangukia pua, korosho, gesi n.k. Tatizo uzembe wa kuganda kwenye lugha moja.

Kuna Watanzania wachache wanalielewa hili https://www.jamiiforums.com/threads...taifa-umuhimu-wa-lugha-ya-kiingereza.1104749/
 
TANZANIA na sisi kila ALHAMISI tutumie KINGEREZA kwenye BUNGE LA KINA BABU TALE.
 
Labda kama alizindua kwa lugha ya Kiswahili, ila huu mfumo wa bunge(Tanzani, kenya na nchi nyingine) tumerithi kwa wakoloni waingereza.

"Westminster" model of parliament.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…