Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Tujenge mfumo rafiki na unaotabirika wa kodi,Utahamasisha ulipaji kodi kwa hiari kwa kuwa utachochea ukuaji mitaji,tuumize akili Tanzania inufaike na nafasi yake ya kijiografia kujenga uchumi unaozalisha,aidha tujiulize wanaostahili kulipa kodi ni watu milioni 27 lakini wanaolipa kodi sasa ni watu milioni 4.7 wakati pale Kenya wanaostahili kulipa kodi ni milioni 15 lakini wanaolipa kwa sasa ni milioni 8.2..shida nini hapa kwetu mbona watu wachache wanabeba mzigo mkubwa sana? Ukienda Uganda unajikutana na watanzania kibao wametoka kununua nguo,viatu,mashuka na vitenge.
Zamani nilikuwa nadhani Congo wanazalisha vitenge na vipodozi kumbe vinapita hapa hapa kwetu kwenda nchini kwao na sisi tunavifuata uko uko halafu tunavirudisha tena hapa Tanzania.
Tax payment is affected by
1. Tax system
2. Tax procedure
3. Tax policies
Kuna mahali tunazingua
Kuna msemo "buli kuundi buli kumbali" (kama siyo shida yako, iko pembeni/siyo shida yako) na ukitaka kujua uhondo wa ngoma ingia ucheze,sasa awa wafanyabiashara ni wao wanaojua mambo wanayoyapitia,ni wao wanaopata hasara kama wakifunga maduka,lakini kama wameona heri wapate hasara kuliko faida wanayoipata inayoambatana na kero wanazozilalamikia,pengine zinazo wapa pia hasara na kushindwa kulipa kodi wanayotakiwa walipe,halafu hatua waliyoichukua ili kero hizo ziweze kufanyiwa kazi,unakuja wewe usiyepata hizo kero/hasara uone ni utoto,naona ni ukosefu wa consideration na ni lack of good judgement,ni vyema kuwajali wengine kuliko kujijali wewe mwenyewe,ubinafsi sio mzuri,kama zipo kero Wafanyabiashara wa Kariakoo wasililizwe na kero zitatuliwe,tuweke mazingira bora wafabiashara waongeze mitaji yao, Wafanyabiashara wa Kariakoo waongezeke na nchi ipate kodi ya halali,
Kwa Kiongozi kuwaambia kuwa maduka sio hospitali kwamba atakayefunga hamna umuhimu wowote ni kujitoa ufahamu akitaka kumaanisha serikali haina hasara yoyote maduka yakifungwa,Serikali iondoe kero ya tra mtaani na Kodi zisizolipika,yaani unajikuta madeni hayaishi kwako Kila wakati unadaiwa na mamlaka za serikali. waseme bwana Fulani Kwa biashara Yako hii unatakiwa kulipa kiasi Fulani mwaka mzima,hivyo sawa,Sasa wanakukadiria vizuri,wakija wakaguzi mtaani wanakataa hayo makadirio Kwa kisingizio kwamba ni kidogo.Pengine mikoani haiko hivyo,pengine mikoani wanaagiza mizigo Uganda pengine Kariakoo yetu hawaijui,pengine hatuhitaji kuwa na monopoly ya watu wachache kwa soko la Kariakoo kuwa kitovu cha biashara Tanzania,
Pengine watu wanaombea Wachina wamalize fasta Ubungo Logistics Centre kukomesha utawala wa Kariakoo,pengine teknolojia inatuaminisha kuwa reli ya SGR ikitoboa Mwanza na Kigoma,basi Kariakoo zitahamia huko,hapo Kariakoo Dar es Salaam tutapauka sana,yote yanaweza kuwa ni sahihi,lakini kwa sasa Kariakoo Dar ni lango la kiuchumi la Tanzania,mwaka 2018 Kariakoo ilitangazwa kuwa Mkoa wa kikodi Tanzania,ni Kariakoo peke yake,siyo Wilaya ya Ilala,na Wala sio Mkoa wa Dar es salaam,hivyo basi Wafanyabiashara kama kuna mashinikizo,tafadhali..ioneeni huruma nchi yenu...ni ukweli biashara siyo siasa,kujiumiza uchumi inaumiza watoto na akina mama wasio na hatia lakini Serikali pia kama kuna kero kwa Wafanyabiashara, tafadhali zitatueni mapema.
Ni kweli kwa Tanzania*Mfumo wa kodi na ulipaji wa kodi kwa mujibu wa sheria za kodi na Mapato ya Serikali* na maboresho ya Sera kwa maendeleo ya watu,ni kosa kubwa sana watu kulipa kodi kwa hiari kodi ni suala la kisheria hivyo ni lazima Ulipaji wake uwe kwa mujibu wa Sheria za kodi sio hiari,pengine hapa Tanzania bara TRA wametumia hiari pengine wanawaelekeza na kuwabembeleza walipa kodi lakini shida siasa inaingilia kati,wahuni wanaanza kuupiga mwingi hadi unamwagika,siasa imezidi kila mahali imeingia hadi kwenye masuala ya kodi,mtu akishakuwa maarufu anatumia umaarufu wake kufanya Tax Evasion,wengine wanataka walipe kodi kama wanalipa sadaka kwa kubembelezana sio kwa mujibu wa Sheria za Kodi na mapato ya Serikali awa wahuni ndio wanaofanya Wafanyabiashara wengine waonekane wahuni,
Nimalizie kwa kuuliza swali,Je Unadhani kupata mtaji wa kufungua biashara Kariakoo ni rahisi?, uwa nasikia watu wametoa kafara kupata mitaji na kuweza kuendesha biashara Kariakoo nilipouliza pale Kariakoo niliambiwa si uchawi wala kafara bali ni nidhamu yako ya matumizi ya pesa,unashindia hindi hili upate mtaji biashara iende,sasa unapokuja kumpiga kodi ya bilioni moja basi Mfanyabiashara huyo atazirai na kufa,nitoe maoni,TRA wabuni mfumo wa E-Assesment & Return payment,ili kuondoa hii migogoro,mashine za EFD zisiuzwe kupitia mawakala,kuwepo na kikokotoo rasmi cha kulipa na fine zitungiwe kanuni zitambulike.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.