Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Imeripotiwa kwamba wakati wa mkutano wa mashauriano uliofanywa na viongozi wa muungano huo katika Hoteli ya Maanzoni iliyo Kaunti ya Machakos, Raila Odinga alikataa mipango ya kumwapisha katika siku ambapo Rais Uhuru Kenyatta amepangiwa kula kiapo cha urais.
Ilisemekana alikataa mpango huo wa baadhi ya wanachama sugu wa muungano huo akisema ana hadhi anayofaa kulinda kimataifa na anaheshimu sheria ambayo alikuwa katika mstari wa mbele kuipigania.
Wafuasi wengi hasa kutoka eneo la Nyanza walisema uamuzi wake ni wa uoga kwani walitarajia aapishwe leo wakati muungano huo utakapofanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Jacaranda, Kaunti ya Nairobi.
Mjini Migori, wakazi wengi walikusanyika katika sehemu za uuzaji wa magazeti jana asubuhi kujadili hali hiyo huku wakionekana kama waliokata tamaa.
"Tulikuwa tuko tayari aapishwe kuwa Rais wetu. Mbona amekunja mkia? Sitajishughulisha tena na mambo ya NASA", alisema Joel Omondi.
Bi Rahab Matinde, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Isebania, alisema amekasirishwa sana na jinsi Raila Odinga hataapishwa.
"Nilikuwa tayari kusikia 'baba' ameapishwa, yeye ndiye Rais wa raia", alisema huku wengi walielekeza ghadhabu zao kwenye mitandao ya kijamii, ambapo Bw. Kepha Omai aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa " Kama Raila hataki kuapishwa basi ni heri astaafu katika siasa kabisa tena ahame nchi hii kabisa".
Wakili mashuhuri Bw. Miguna Miguna, ambaye pia amekuwa mfuasi wa muungano huo alisema kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter;
" Sitakuwa katika uwanja wa Kasarani kushuhudia urembeshaji wa uovu na upambaji wa madikteta. Sitakuwa katika uwanja wa Jacaranda kusalimu amri kwa walaghai. Nitaombeleza tu mashujaa wetu na waliofariki vitani baada ya ukombozi".