Haitokuja siku tufanane, Tanzania mko nyuma sana kabla kuifikia Kenya, tuliumia sana mpaka tukapata huu uhuru wa maoni tulio nawo.
Fahamu kwamba sheria Kenya ziko bayana, kumtukana mtu yeyote, awe rais au mwananchi wa kawaida ni kosa la jinai na utafungwa, hilo lipo kote duniani.
Lakini kwa Tanzania, kuikosoa serikali tu, imetosha utiwe lockup, tumeona jamaa wanafungwa kisa walipiga picha za kuta vyuoni, huku kwetu wewe kosoa unavyotaka, ukiweza hata mtuhumu rais kwenye kila aina ya ufisadi, mseme vyote unavyohisi kisha nenda kajilalie zako, hamna atakayekufuata, ila kuwa makini usinywe gongo/chang'aa ikutume utamke maneno kama 'rais Uhuru ni mbwa', hapo rais yeye kama binadamu utakua umemkosea na ana haki ya kukushtaki.