Ha ha ha ha, eti mseme rais unavyotaka. Nyie mmeipaka mafuta mwaita eti hate speech na incitement lakini kimsingi ni yaleyale tu. Ha ha ha
Niambie kama Bongo unaweza kumuita rais 'mtoto wa mbwa' 'mwizi, mbwa, fisi' na ukabaki hai, tazama hizi video
Kwani Kenya unaweza? Ingekuwa inawezekana kusingekuwa na kesi ya kujibu kwa huyo mbunge.
Ama kumdunga sindano za usingizi Miguna Miguna na kujipata yuko Canada. Eti mahakama ziko huru, acha kabisa ni maigizo tu mnafanya mahakamani mbona Miguna hajarudi pamoja na maigizo ya mahakamani. Bro is just the same monkeys video in different forest
Kenya unaweza kumtukana rais ila utashtakiwa kwenye mahakama ya kawaida maana kumtukana mtu yeyote ni kosa la jinai, lakini kwenu huko mwanafunzi kupiga picha ukuta wa chuo, au mwingine kapiga picha ya mahangaiko ya maji kisha akatoweka. Kuna yule jamaa anaitwa Kabendera anaozea gerezani kisa kaikosoa serikali.
Mpo bado sana, ni aibu sana kwa nyie kujaribu kujifananisha na Kenya, level yenu mkapimane na akina Burundi huko.
KWahiyo kwetu kumtukana mtu yoyote na rais si kosa la jinai? Kusema watu kupotea Kenya ndo wanaongoza kwa kupoteza watu watu.
Kwani kosa la Miguna Miguna ilikuwa nini si kuwakosoa serikali? Na prof yule aliyetunguliwa kwenye helkopita huko Kenya? Sahivi mnamwinda hata Makamu wenu wa Rais Ruto. Wacha kuwa kama ostrich kuweka kichwa kwa mchanga mwili mwingine nje eti umejificha. Kenya kwa ku assasinate watu ni beyond repair in relation to Tanzania.
Nikutajie kabisa maana utaleta longo longo hapa.
1.Jacob Juma
2.Chris Msando
3.George Muchai
4.Meshack Yebei
5.Sheikh Abubakar Shariff aka Makaburi
6.Aboud Rogo
7.Careen Chepchumba
8.George Thuo
9.Mercy Keino
10 Oscar Kamau King’ara
........
Tatizo unabwabwaja na kuchanganya hoja incoherently, kutaja taja matukio ambayo hayaendani.
Kenya upuzi wa mtu kutoweka huwa aidha ni high level politics, mibabe wa kisiasa wanawindana kwenye high level. Lakini nyie hapo maskini mwanafunzi kidagaa kapiga tu picha inatosha kutoweka.
Ni kwasababu kwenu vidagaa vinapotea na hamna wa kuvipazia sauti. Lakini kwenu vidagaa vinapotea sana beyond repair. Police wa kenya anaweza kuamka tu barabarani akaua watu 10 akasema wakora. Ha ha ha , bora Tanzania wanapotea na kurudi kwenu wanaua mchana kweupe na mnaufyata na hauongelewi sababu hana pesa.
Hutakuta Mkenya anateswa na serikali kisa kakosoa, hayo yalikua ya miaka 80s, ambayo nyie mpo sasa.
Nakuhakikishia mambo ambayo hufanywa na Wakenya wa kawaida, jinsi wao hukosoa serikali na kuanika kila kitu, hamjafikia level hiyo na hamuwezi, na haitokuja siku.
Kwenu huko mtu wa kawaida kukosoa labda awe nje ya nchi, na hata akiwa nje ya nchi inabidi afiche uso asionyeshe sura, hehehe nakumbuka hii video yaani kituko kabisa, unalazimika kuficha sura wakati wa maandamano ambayo unayafanyia nchi ya mbali, inaonyesha namna gani mnaishi masha ya hatari hata kuizidi North Korea, nilicheka sana kwa hii video, Mange tu ndio huwa na ujasiri, sema naye aishie mbali huko asiwahi kuota hataa siku moja kwamba amaerudi nyumbani
Wale tausi wamesha totoa?Haitokuja siku tufanane, Tanzania mko nyuma sana kabla kuifikia Kenya, tuliumia sana mpaka tukapata huu uhuru wa maoni tulio nawo.
Fahamu kwamba sheria Kenya ziko bayana, kumtukana mtu yeyote, awe rais au mwananchi wa kawaida ni kosa la jinai na utafungwa, hilo lipo kote duniani.
Lakini kwa Tanzania, kuikosoa serikali tu, imetosha utiwe lockup, tumeona jamaa wanafungwa kisa walipiga picha za kuta vyuoni, huku kwetu wewe kosoa unavyotaka, ukiweza hata mtuhumu rais kwenye kila aina ya ufisadi, mseme vyote unavyohisi kisha nenda kajilalie zako, hamna atakayekufuata, ila kuwa makini usinywe gongo/chang'aa ikutume utamke maneno kama 'rais Uhuru ni mbwa', hapo rais yeye kama binadamu utakua umemkosea na ana haki ya kukushtaki.