Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameamua kujiliwaza katika mbuga za nchi hiyo huku akisubiri hatma ya kesi.
Picha hizi za Rais mteule Uhuru Kenyatta zimepakiwa katika akaunti zake za Twitter, Instagram akiwatazama tembo na kumeandika kama ifuatavyo;
"Tukijiliwaza katika urithi maridhawa wa taifa letu huku tukisubiri hatma ya mchakato wa mahakama, itunze amani". Ameandika Kenyatta
Mahakama ya juu katika kesi hiyo iliyowasilishwa na Raila Odinga ambaye alikuwa mgombea urais kupitia Muungano wa Upinzani NASA, inatarajiwa kutoa uamuzi kufikia Ijumaa.