KENYA: Walimu waiomba Serikali kuruhusu wanafunzi wachapwe shuleni, wadai nidhamu imeshuka

KENYA: Walimu waiomba Serikali kuruhusu wanafunzi wachapwe shuleni, wadai nidhamu imeshuka

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Baadhi ya walimu Nchini Kenya wanataka adhabu ya viboko kurudishwa shuleni, ili kuwaadhibu wanafunzi wasiokuwa na nidhamu.

Adhabu ya viboko ilipigwa marufuku katika shule za Kenya mwaka 2001 na sheria inawalinda watoto dhidi ya manyanyaso ya aina yoyote.

Lakini baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari wanasema kuondolewa kwa adhabu kwa wanafunzi kunadumaza mamlaka ya waalimu.

Mwenyekiti wa Muungano wa Waalimu wa Shule za Sekondari Nchini Kenya, Kahi Indimuli amesema kwamba kazi ya kusimamia nidhamu ya wanafunzi ni ngumu sana kwa shule yoyote.

Walimu wakuu wa shule za sekondari wanakutana wiki hii kwa kongamano la kila mwaka kujadiliana kuhusu visa vya utovu wa nidhamu vinavyoendelea kuongezeka Kenya.

Shule kadhaa za sekondari zilichomwa moto mwaka uliopita, wanafunzi wakitajwa katika visa hivyo.

Source: Voice of Africa
 
Tatizo kuna baadhi ya walimu hupitiliza, inakua kama ana ukichaa fulani hivi anaushushia kwa mtoto, ila kiukweli vitoto vya Kiafrika bila kutembeza mboko havitulii.
Niko nao hapa nyumbani wapo likizo, na wametembelewa na binamu zao hivyo nyumba imejaa utadhani darasa, ila sasa wanafahamu mziki wangu maana mimi ni old school, nidhamu kwangu hapa ni mwendo wa kijeshi yaani, kabla hujagusa video games zozote lazima utimize shughuli zote kuanzia usafi wa mwili wako, mavazi yako, usome na unieleze ulichokisoma, kazi za nyumba......kila kitu kikinyooka uko huru ingia kwenye PS au simu au chochote fulu WiFi nimewawekea.

Ukizingua tu unalo tena huwa sikawii...
 
Back
Top Bottom