Kenya wana uwezo wa kupima watu 35,000 kwa siku, Tanzania uwezo ni 500 kwa siku, ni aibu na fedheha kwa taifa tajiri kama hili

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Ni aibu na fedheha kubwa kwa taifa lenye raia takribani milioni 60 kuwa na maabara yenye uwezo wa kupima wagonjwa wasiozidi 500 kwa siku wa corona na jirani yetu mwenye raia takribani milioni 45 kuwa na maabara yenye vifaa na uwezo wa kupima wagonjwa zaidi ya 35,000 kwa siku.

Na tunajisifu kuwa tuna huduma bora za afya nchini kweli? Huduma ni majengo au vifaa na watoa huduma?

Return Of Undertaker,

Magufuli bana kuna takwimu amezikariri na wanazirusha kwenye TBC1 na Channel 10 kwenye kipindi vya cha #Tunatekeleza. Utakuta anasema "tumejenga hospitali za wilaya na vituo vya afya 500, tumeongeza fedha ya dawa kutoka Tsh 30 Bilioni hadi 250 Bilion kwa mwaka, tumeshinda zabuni ya kupeleka dawa nchi za SADC"

Yaani ni ujinga mtupu na upumbavu anaowalisha wa Tanzania. Kwanza siyo kweli hakuna pesa ya dawa aliyopeleka MSD kwa mwaka 2019/20. Pili Tanzania haina dawa za kuuza SADC kwa sababu hata MSD yenyewe iko mufilis haina dawa.

Bahati nzuri Mungu si Athman huyo anamdhalilisha polepole kwa UWONGO wake. Hata hiyo machine moja iliyopo NIMR pale ni ya msaada wa CDC.
 
Tunapenda sana kujitutumua lakini kiuhalisia Kenya ipo mbali sana ukilinganisha na Tanzania. Siyo kwa sababu wana pesa nyingi, siyo kwa sababu ni matajiri sana bali wamebahatika kuwa na uongozi mzuri na wenye maono, na kuwa na watu ambao, wengi wao siyo wanafiki.

Tanzania tuna short sighted leadership na watu ambao tumejaa unafiki, mahaba ya kiuwendawazimu na ushabiki wa kijinga. Tunafurahia kubishana hata kwenye mambo ambayo ni dhahiri.

Nani anaweza kuamini kuwa kwenye jamii ya watu wenye akili na uongozi wenye maono, Bunge mpaka sasa lingekuwa linaendelea? Mpaka sasa 3 wameanguka na kupoteza maisha, lakini waliobakia wanawaona waliofariki, labda walikuwa na ubinadamu nusu, ila wao kwa kuwa wana ubinadamu kamili, hawawezi kuambukizwa wala kufa. Na hawa wenye akili za inzi ni viongozi, je hali ipoje kwa wananchi wa kawaida.

Tumekuwa kama inzi. Inzi 100 wakiwa kwenye mzoga, unaweza kuua 50, waliobakia watarukaruka, baadaye watarudi tena. Utaua 40, waliobakia 10 watarukaruka, kisha watarudi tena. Hata ukiua 9, aliyebakia mmoja atarukaruka na kurudi tena. Mpaka uwamalize wote.

Rasilimali kubwa ya nchi siyo fisi wa kwenye mbuga za wanyama, dhahabu au gas iliyopo ardhini BALI ni nini watu wake wamebeba ndani ya vichwa vyao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa. Watu wazima wanaongea utafikiri hawana Ubongo au wana matatizo ya akili, Wanajenga hoja za kipumbavu kwa maswala ya maana, sababu kubwa ni kulinda Chama.
 
Sisi hata hao 500 tunadanganya. Tuna magari mapya lakini ya kuzika watu 35,000 kwa siku. Nyambaf kabisa
 
Tunapenda sana kujitutumua lakini kiuhalisia Kenya ipo mbali sana ukilinganisha na Tanzania. Siyo kwa sababu wana pesa nyingi, siyo kwa sababu ni matajiri sana bali wamebahatika kuwa na uongozi mzuri na wenye maono, na kuwa na watu ambao, wengi wao siyo wanafiki.

Tanzania tuna short sighted leadership na watu ambao tumejaa unafiki, mahaba ya kiuwendawazimu na ushabiki wa kijinga. Tunafurahia kubishana hata kwenye mambo ambayo ni dhahiri.

Nani anaweza kuamini kuwa kwenye jamii ya watu wenye akili na uongozi wenye maono, Bunge mpaka sasa lingekuwa linaendelea? Mpaka sasa 3 wameanguka na kupoteza maisha, lakini waliobakia wanawaona waliofariki, labda walikuwa na ubinadamu nusu, ila wao kwa kuwa wana ubinadamu kamili, hawawezi kuambukizwa wala kufa. Na hawa wenye akili za inzi ni viongozi, je hali ipoje kwa wananchi wa kawaida.

Tumekuwa kama inzi. Inzi 100 wakiwa kwenye mzoga, unaweza kuua 50, waliobakia watarukaruka, baadaye watarudi tena. Utaua 40, waliobakia 10 watarukaruka, kisha watarudi tena. Hata ukiua 9, aliyebakia mmoja atarukaruka na kurudi tena. Mpaka uwamalize wote.

Rasilimali kubwa ya nchi siyo fisi wa kwenye mbuga za wanyama, dhahabu au gas iliyopo ardhini BALI ni nini watu wake wamebeba ndani ya vichwa vyao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru hujaji-exclude. Halafu ni rahisi tu kuhamia Kenya au bado kuna hela unaiskilizia[emoji23][emoji23][emoji23].

Ila JF bana ina raha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo takwimu ya Kenya ndo ingekuwa tz unafikiri nani angeamini?
Si bora muambiwe tu hiyo miatano maana kwanza mnapuresha badala ya pressure 😜

Tusiige kunya kwa tembo.
 
Return Of Undertaker,

Magufuli bana kuna takwimu za kipumbafu sana amezikariri na wanazirusha kwenye TBC1 na Channel 10 kwenye kipindi vya cha #Tunatekeleza. Utakuta anasema "tumejenga hospitali za wilaya na vituo vya afya 500, tumeongeza fedha ya dawa kutoka Tsh 30 Bilioni hadi 250 Bilion kwa mwaka, tumeshinda zabuni ya kupeleka dawa nchi za SADC"

Yaani ni ujinga mtupu na upumbavu anaowalisha wa Tanzania. Kwanza siyo kweli hakuna pesa ya dawa aliyopeleka MSD kwa mwaka 2019/20. Pili Tanzania haina dawa za kuuza SADC kwa sababu hata MSD yenyewe iko mufilis haina dawa.

Bahati nzuri Mungu si Athman huyo anamdhalilisha polepole kwa UWONGO wake. Hata hiyo machine moja iliyopo NIMR pale ni ya msaada wa CDC.
Utaendelea kuumia kwa sababu Mimi kwa macho yangu naona serikali inajitahidi kuimarisha huduma za afya na tuko vizuri sema bado changamoto zipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Most of the IDs here are Kenyans who pretend to comment as Tanzanians. This won't help you achieve anything. Tanzania as a nation has its ways of doing things. And if we had to copy anything for the development of our country we would rather copy it from developed countries.
 
Utaendelea kuumia kwa sababu Mimi kwa macho yangu naona serikali inajitahidi kuimarisha huduma za afya na tuko vizuri sema bado changamoto zipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe una macho au una makengeza? Maendeleo gani unayoyaona toka huyu ameyafanya? Huduma gani za afya zimeboreshwa? Mnashangilia maujinga ya kukaririshwa tu!
 
Back
Top Bottom