KENYA: Wanahabari 3 walazimika kukesha katika chumba cha habari kuhofia kukamatwa na polisi

KENYA: Wanahabari 3 walazimika kukesha katika chumba cha habari kuhofia kukamatwa na polisi

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Wanahabari watatu wa Kenya walilazimika kukesha katika chumba cha habari kwa kuhofia kukamatwa na polisi waliokita kambi nje ya majengo ya shirika la habari la Nation.

Mawakili wa wanahabari hao wamewasilisha maombi mahakamani ya kutaka hakikisho la uhuru wa wanahabari hao.

Vituo vitatu vya televisheni vilifungiwa kuonesha matangazo yao na Serikali baada ya kukiuka agizo la Serikali la kutoonesha matangazo ya moja kwa moja ya hafla ya kujiapisha kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa Rais wa wananchi.

Chanzo: DW kiswahili
 
Hili "watetezi" wa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari mnasemaje?
 
Lakini kwanini aliyejiapisha kuwa Rais wa watu anaachwa?

Halafu kukiwa na hafla White House mnawaita kwa mbwembwe. Ni vema waandishi wakapewa heshima yao
 
Kama ni kutangazwa alisha tangazwa sasa huku kuwavizia watu wengine ni uonevu tu. Habari haikuwa kumtangaza RAO bali sasa habari ni kuwavizia wanahabari
 
uhuru wa habari sio kinga kuwa mtu akiambiwa na sheria kuwa asifanye hiki yeye anaenda kufanya kisa ana haki kwa kutumia uhuru wa habari, kama kuna uhuru wa habari basi wanahabari wetu wawe wanalazimisha kwenda ikulu kujua kinachoendelea kila siku wakizuiwa wawajibu wanajeshi kuwa haki ya kupata habari (uhuru wa habari si ndio au sio) watu waliambiwa wasiende huko ni illegal wanalazimishwa kwenda wakijua kabisa ni illegal sasa wafanyweje si kukamatwa tu au.
Hili "watetezi" wa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari mnasemaje?
 
uhuru wa habari sio kinga kuwa mtu akiambiwa na sheria kuwa asifanye hiki yeye anaenda kufanya kisa ana haki kwa kutumia uhuru wa habari, kama kuna uhuru wa habari basi wanahabari wetu wawe wanalazimisha kwenda ikulu kujua kinachoendelea kila siku wakizuiwa wawajibu wanajeshi kuwa haki ya kupata habari (uhuru wa habari si ndio au sio) watu waliambiwa wasiende huko ni illegal wanalazimishwa kwenda wakijua kabisa ni illegal sasa wafanyweje si kukamatwa tu au.
Yaani ni kaaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom