Kenya: Wananchi wenye hasira kali wamkamata trafiki anayedaiwa kutaka kupokea rushwa

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Kwenye video ambayo inasambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, trafiki mmoja nchini Kenya ameonekana kukamatwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuwa alitaka kupokea rushwa.

Video isiyo na tarehe imewaonyesha raia wakimzingira trafiki huyo kwa madai ya kuvunja kioo cha matatu baada ya jaribio la rushwa kushindikana.

Trafiki huyo alidaiwa kuvunja kioo cha matatu hiyo baada ya dereva wa matatu hiyo kukataa kumpa rushwa.

Inaonekana Kenya raia wamechoka na suala la rushwa na kuamua kujichukulia sheria mkononi.

Soma Pia: TAKUKURU kamateni Trafiki Wala rushwa

Bongo mtu alitekwa ndani ya basi abiria wote kimyaa wakati tulikubaliana kwa sasa mtu akija kukamata bila kitambulisho tunamchangia kumpiga
 
Walikuwa na vyuma Babu. Kauli za kishujaa kwenye mitandao tu.

Nani angepambana na wajuba zaidi ya wawili (kwa mujibu wa maelezo ya shuhuda) wenye manati ya chuma zile manati za mzungu?

Wanakumwaga ubongo kwanza kisha wanaonesha vitambulisho kwamba uliwazuia kufanya kazi yao.
 
Hahaha! Dah!
 
Natamani sana hilo zali la kumwagwa ubongo huo mkono ntakavyoutembeza
 
Back
Top Bottom