Kenya wanapanga kufuta majimbo/ Constituency 27. Tanzania tunaongeza wanaaminishwa italeta maendeleo

Kenya wanapanga kufuta majimbo/ Constituency 27. Tanzania tunaongeza wanaaminishwa italeta maendeleo

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,532
Reaction score
14,164
Kenya uchahaguzi mkuu ujao wanaoanga kupunguza majimbo 27 na hivyo wabunge 27 wanwenda kukosa kazi. Raia wa Kenya wanataka idadi ya Wabunge ipungue na sio iongezeke.
==================
Aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Farmers, Irungu Nyakera, Aonya Kuhusu Hatma ya Majimbo 27 Nchini Kenya

Aliyekuwa Kiongozi wa Farmers Party, Irungu Nyakera, ameonya kuwa majimbo 27 nchini Kenya yanaweza kufutwa endapo mchakato wa mapitio ya mipaka, ambao umechelewa, hautaanzishwa haraka. Hali hii inaweza kuathiri Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Katika taarifa aliyoitoa Jumanne, Aprili 22, Nyakera alieleza kuwa endapo suala hili halitatatuliwa mapema, majimbo hayo yanaweza kusitishwa kisheria. Hii ingemaanisha kuwa hakutakuwa na Wabunge walioko kwenye majimbo hayo katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Sasa njoo Tanzania Jamhuri ilio jaaa wajinga sisi tunaongezewa majimbo na kuaminishwa yanaleta maendeleo. Kwamba Wabunge wakiwa wengi Bungeni basi na maendeleo tutayaona kwa kasi sana.

Kwa sasa maendeo yanachelewesha na idadi ndogo ya Wabunge na pssible kuna mpango wa kuja kujenga ukumbi mpya wa Bunge ili ku accomadate idadi zaidi.

Na utakuta huko mtaani raia choka mbaya ndio wanao shangilia majimbo kuongezwa bila kujua hakuna kitakacho badilika kwemye life lao la kila siku.
 

Attachments

  • Screenshot_20250427_201502.jpg
    Screenshot_20250427_201502.jpg
    286 KB · Views: 28
FIFA wakisema World Cup timu shiriki ziongezwe kutoka 48 mpaka 58 . possibility ya Tanzania kushiriki inakuwa kubwa si ndio?

Serikal ikiongeza viti vya ubunge kufikia viti 800 yaani hata kama NI wewe possibility ya kupata ubunge inakuwa kubwa Sana si ndio?

Si kila Jambo NI la kupinga . mengine n neema.
 
Back
Top Bottom