KENYA: Wanawake wadhalilishwa kingono baada ya kujifungua

KENYA: Wanawake wadhalilishwa kingono baada ya kujifungua

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu ameamrisha uchunguzi kufanywa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.

Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao zinadai kina mama waliojifungua wamekuwa wanashambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.

Chumba hicho cha watoto huwa ghorofa tofauti na wadi za wanawake waliojifungua.

Wasimamizi wa hospitali hiyo wamesema hawajapokea malalamiko yoyote.

Yote yalianza baada ya ujumbe kuandikwa aktika ukurasa wa Facebook kwa jina Buyer Beware ambao mara nyingi hutumiwa kuwatahadharisha wateja na wanunuzi wa bidhaa na huduma.

Ujumbe uliwatahadharisha kina mama wanaojifungulia katika hospitali hiyo kwamba wamo hatarini ya kudhalilishwa kingono na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo.

Wanawake wengine walichangia na kudai wamewahi kudhalilishwa au jaribio kufanywa, au jamaa na marafiki zao wakadhalilishwa.

Wengi wanadai kina mama waliojifungua waliviziwa wakiwa njiani kuelekea chumba hicho cha kunyonyeshea watoto au wakirudi chumba chao baada ya kunyonyesha.

Baadhi ya wanaodaiwa kunyanyaswa kingono, ujumbe unasema, walitendewa kitendo hicho siku chache baada yao kujifungua kupitia upasuaji.

Waziri Mailu ameagiza uchunguzi wa dharura kufanyika na ripoti kamili kuwasilishwa kwake kufikia Jumatatu.

Afisa mkuu mtendaji wa hospitali hiyo Lily Koros amesema hakuna mwanamke hata mmoja aliyewahi kulalamika kwamba alidhalilishwa kingono hospitalini humo.

Amesema hospitali hiyo huwa chini ya uangalizi wa kamera za usalama (CCTV) wakati wowote na hakuna kisa hata kimoja kilichogunduliwa.

Amewataka walio na habari kupiga ripoti kwa maafisa wa hospitali au polisi.

BBC Swahili
 
Niliona taarifa hii citizen tv mama mmoja anahojiwa, nilishangaa sana!
 
Cctv zipo hospitalini kotee, stori na porojo tu hizo
 
labda kama kinafanywa kwa kishirikika, lakini kwa akili ya kawaida, mbunye iliyojifungua hata wiki moja tu vile inavyokuwa na vile mwanamke anavyokuwa, ni shetani tu anaweza kufanya icho kitu. ila wakati wa ujauzito nafikiri wengi tu hata hapa tz wanabakwa kwasababu ya joto la mimba.

wanawake wengi sana hasa wanaolazwa hospitalini ukiona unaambiwa ndugu asiwepo/asilale pale usiku ule, hao manesi wa kiume wanapigaga sindano ya usingizi na kubaka wengi tu sema wanawake hawasemi tu. nilikutana na kesi moja nesi wa kiume amembaka mwanamke aliyelazwa, ndugu waliambiwa hawatakiwi kulala hapo hospitalini siku hiyo mwanamama huyo akabaki peke yake, usiku akajifanya kupiga sindano, kuja kustuka mama anajiona kachafuka na mbunye anasema imechoka kama ametoka kufanya ngono, kuangalia na shahawa zinamtoka, mama kakomaa hadi jamaa kapelekwa polisi. sijui iliishia wapi ile.
 
Back
Top Bottom