Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimepata habari toka Kenya kuwa elekezo limetolewa kwa askari wa kawaida na trafiki kuacha mchezo wa kukaa barabara kuu kusimamisha magari ili kukagua au sijui mambo ya spidi. Wameambiwa askari wa trafiki kazi yao kubwa iwe ni kusimamia magari maeneo ya mijini sio kuvizia magari huko porini kwenye njia kuu. Na kama wakitaka kuweka kizuizi au kwenda mahali njia kuu basi lazima kuwe na sababu maalum na wapewe kibali maalum. IGP wa Kenya amesema trafiki waende kwenye maeneo ya ajali tu sio kukaa barabarani wakivizia magari.
Kwa upande wa Tanzania askari trafiki njia kuu imekuwa ni kero. Hadi wanajificha mitini. Wakati tunakubali kwamba lazima madereva waendeshe magari kwa viwango vinavyotakiwa sehemu za miji, labda serikali ifikirie utaratibu wa kuweka matuta badala ya trafiki kuvizia watu kuwa umeendesha gari 55km/hr badala ya 50km/hr. Hata mara nyingine wanakuvizia kuona kama unazidisha spidi mita 5 tu baada ya alama ya 50km/hr. Au trafiki anakusimamisha bila kuona kosa, bali akutafutie kosa baada ya kuzunguka gari kama mara tatu. Huo ni upumbavu sio tena kufuatilia sheria.
Ikumbukwe kwamba mwaka 2018 Uganda nayo ilipiga marufuku trafiki barabara kuu, pale Museveni aliposema hawafanyi lolote bali kuomba rushwa tu huko barabara kuu.
Hongera sana Kenya.na Uganda. Mnajitambua sana maana siku hizi Tanzania kuwa na gari imekuwa karaha kutokana na usumbufu wa trafiki. I wishi I kudu be in Kenya or Uganda