JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mvita Maxwell Agoro akizungumza na mmoja wa raia 40 wa Jordan waliokamatwa. Picha: Kwa hisani
Polisi wa Mombasa Nchini Kenya wanawashikilia watalii 40 raia wa Jordan baada ya kukutwa wakiombaomba katika Mitaa ya Old Town na Marikiti ili wakusanye fedha ya kwenda Nairobi.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Mvita, Maxwell Agoro amesema waliwakamata baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wenyeji, ambapo waliokamatwa watu wazima ni 19 na watoto ni 21.
Watalii hao walikuwa na ‘visa’ halali lakini kuombaomba ni kukiuka masharti ya hati zao za kusafiria.
---
Polisi mjini Mombasa wamewashikilia watalii 40 kutoka Jordan baada ya kuonekana wakiomba katika barabara za jiji hilo. Watalii hao waliripotiwa kuonekana wakiomba katika mitaa ya Old Town na Marikiti Market siku ya Alhamisi ili kuchangisha pesa za safari yao ya Nairobi.
Bw Maxwell Agoro, Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mvita, alithibitisha kukamatwa kwa polisi hao, akisema polisi walikwenda kuwakamata watalii hao baada ya kupokea kidokezo kutoka kwa wenyeji. Wageni hao, watu wazima 19 na watoto 21, walikuwa na viza halali za kitalii, lakini kuombaomba kulikiuka masharti ya hati zao za kusafiria, na kupelekea kukamatwa kwao, alisema Agoro.
“Baada ya kuwapata polisi waliwapeleka kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano. Walipatikana wakienda kinyume na utaratibu wa visa kwa kujigeuza ombaomba kinyume na kuwa watalii,” akasema akiongea na Nation. Bw. Agoro aliendelea kusema kuwa uchunguzi wa awali ulifichua kuwa watu hao 40 walikuwa wakielekea Eastleigh jijini Nairobi na ilibidi waombe kupata pesa za safari yao.
Wageni hao watapelekwa ofisi ya uhamiaji kwaajili ya taratibu nyingine kufuata, wakati huu wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Pwani ambapo wanaendelea kuhojiwa.