Kenya: Watu 279 wamedhurika baada ya chanjo ya covid19, mmoja afariki

magufuli umetuacha baba.

ona maono yako yalihitajika kusaidia mpaka ndugu zetu kutoka kenya,sasa wanaumizwa.
Na chanjo za Ndui na Polio ambazo zinatoka kwa mabeberu na zenyewe tuache?
 
Kenyans are jokers
 
Tuendelee kujifukiza R.I.P JPM

ulikataa chanjo ulikuwa una maono
 
Waliochanjwa kwa ujumla ni 370,000. Hakuna anayelazimishwa chanjo, leteni chanjo wanaotaka wapate. Muhimu kuzingatia sheria na masharti yake hasa ya utunzaji.
 
Lumumba ndio maana tunawaita Ma ZERO brain yaani haujaelewa kabisa logic ya swali langu.
Wewe unataka tuangalie walichanjwa na hawajapata madhara ili tupuuze hao wachache ambao wamepata madhara,maana huo ndio utetezi wenu kwamba watu wengi wamechanjwa na hawajapata madhara hivyo mnahalalisha kuwa hizo chanjo hazina shida lakini uhalisia unakataa.
 
Waliochanjwa kwa ujumla ni 370,000. Hakuna anayelazimishwa chanjo, leteni chanjo wanaotaka wapate. Muhimu kuzingatia sheria na masharti yake hasa ya utunzaji.
Hoja ni kwamba tunaambiwa hizo chanjo ni salama na ndio maana hao watu wakakubali kuchanjwa sasa haya yanayoibuka yanatakiwa yatolewe majibu na sio kusema hawajalazimishwa. Huko Saudia ili uende kuhiji unalazimishwa chanjo kama hutaki hauendi.
 
Tupate chanjo za Pzifer au Moderna. AstraZeneca imekuwa na habari zisizo nzuri karibu nchi zote.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kwa chanjo ambazo zimegundulika hadi leo, Astrazeneca ndio most affordable. Hivyo, kwa nchi maskini hii ndo preference yao kwa mass immunisation.
 
Mimi na wenzangu wanaozitaka, siko mwenyewe. Nyie ambao hamzitaki muendelee kupiga nyungu na kula malimao tu ila chonde chonde hamtapata mitungi ya oksijeni tena baada ya chanjo kusambazwa.
Upate wewe hapo, usitujumuishe.
 
Wakishamaliza kuchanja watu wao huko Ulaya na Marekani hata hizo nyingine zitakuwa rahisi tu kwa sababu demand itapungua.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kwa chanjo ambazo zimegundulika hadi leo, Astrazeneca ndio most affordable. Hivyo, kwa nchi maskini hii ndo preference yao kwa mass immunisation.
 
Mimi na wenzangu wanaozitaka, siko mwenyewe. Nyie ambao hamzitaki muendelee kupiga nyungu na kula malimao tu ila chonde chonde hamtapata mitungi ya oksijeni tena baada ya chanjo kusambazwa.
Kwani sasa hivi watu wanagombea mitungi ya oksijeni?
 
Hata ALU ,fansida ,quinine baadhi ya watu zinawaletea madhara ni hivyo hivyo hata Astrazeneca kwamba baadhi ya watu itawapa madhara ndio maana nikataka uweke idadi ya waliochanjwa ili kuweza kujua % ya athari isije ikawa kama takwimu za ulaya/US waliochanjwa zaidi ya 15m ila waliothirika ni 45 tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…