KENYA: Watu watano wafariki kwa ajali ya gari wakiwa wanaelekea kwenye mazishi

KENYA: Watu watano wafariki kwa ajali ya gari wakiwa wanaelekea kwenye mazishi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Watu watano wakiwamo wanawake wanne na mtoto mmoja wameripotiwa kufariki kwa ajali ya gari wakati wakiwa wanaelekea kwenye mazishi. Ajali hiyo ilihusisha Malori mawili pamoja na gari dogo aina ya Saloon.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Murula yaliyopo katika njia panda ya Naivasha nchini Kenya. Aidha, Kamanda wa Polisi aitwaye John Kwasa amethibisha kutokea kwa ajali hiyo.

Akifafanua zaidi kuhusu ajali hiyo, Kamanda John anaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa gari dogo (Saloon) kujaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake, ndipo akakutana uso kwa uso na Malori wawili yaliyowabana katikati na kusababisha kifo chao papo hapo.

Ama kwa upande wa dereva wa Malori, Kamanda John anaeleza kuwa madereva hao wamepata majeraha kiasi na wameelekea katika hospitali ya Naivasha ili kutibiwa.


accident2.png
 
RIP Mungu aziweke roho za marehem mahala pema

Na Mungu awatie nguvu wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi
 
Back
Top Bottom