Kenya: Watu watatu wauawa na alshababi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Watu watatu wauawa na wengine watano wajeruhiwa katika shambulio lilitokea februari 19, 2020 la watu wanaodhaniwa kuwa ni al shababi katika kaunti ya Mandera

Basi hilo linalomilikiwa na kampuni ya Moyale Raha lilikuwa linatoka Mandera likielekea Nairobi. Dereva wa basi hilo ni mmoja kati ya watu waliojeruhiwa.

al Shabaab wamezidisha mashambulizi yao dhidi ya kenya tangu mwaka mpya

Januari waliwauwa wamerekani watatu katika kambi ya jeshi ya Manda huko Lamu

Mwezi huo huo pia, wanafunzi wane waliowawa katika mapigano ya risasi kati ya polisi na wanamgambo wa al shababi

Januari 13 pia waliwapiga risasi walimu watatu wa shule yam sing Kamuthe, iliyopo Garissa

Mwanzoni mwa mwezi huu magari mawili ya kutengeneza barabara yalichomwa moto, alshababi walituhumiwa kwa tukio hilo

Chanzo: Citizen tv
 
Inamaana walivamia basi andika vyema basi tuelewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…