Kenya what can we learn from Rwanda's ultra-modern stadium built in 6 months

Kweli kabisa Kagame anawacha alama Africa. Rwanda kanchi kadogo sana na hakana madini wala mafuta lakini wanajenga infrastructure kubwa kubwa hadi mtu anajiuliza pesa inatoka wapi. Huo ndio uongozi bora
Pesa inatokea Kongo.
 
Hio sio kweli. Hua tunajaza Kasarani stadium hadi pomoni, watu 60,000.
sisi uwanja wa taifa tunaujaza kwenye tournament zote, local and international tournaments.

niambie lini kasarani stadium iliwahi kujaa zilipocheza local football team za kenya?

na usituletee habari za kujaa kunapokuwa na international tournament maana tunawajua wakenya mnaabudu sana vya wazungu kuliko vya kwenu.
 

Sio kweli mnajaza uwanja kwenye michuano yote, huwa mnafanya wakati kuna mtani jembe, mechi ya Simba vs Yanga.
Kenya pia hujaza ikitokea Gor vs AFC.
 
Tulien ndg zangu wakenya na sisi huku chattle na kule Ruangwa tunajenga li-indoor stadium kuuuubwa mpk wazungu watakuja kuzishangaa.

Nice discussion.
 
Pesa inatokea Kongo.

Si kuna kipindi mlijisifu sana kwamba mumemfukuza Kagame Kongo, anyway, kama zinatoka huko basi poa maana wenyeji wa Kongo hawajui kutumia raslimali zao, wacha mjanja afaidi watu wake, hamna haja kuwa na liinchi lote lenye kila kitu lakini kwenye ubongo huna chochote.
 
Sio kweli mnajaza uwanja kwenye michuano yote, huwa mnafanya wakati kuna mtani jembe, mechi ya Simba vs Yanga.
Kenya pia hujaza ikitokea Gor vs AFC.
Juzi hukuona Yanga Vs Kariobangi na Simba Vs Power dynamos uwanja ulivyo jaa! Au angalia week end hii Simba Vs Ud Songo. Tatizo AFC haiko vizuri kama zamani na Gor ilipotea kwa kipindi kirefu kwa hiyo kuna kizazi hakija ambukizwa ushabiki wa hizo timu zenu mbili zenye ushindani wa jadi. Kuna kipindi Gor na AFC zilikua kama hazipo kwenye ramani ya soka Kenya, ilikua ni Tusker, Mathare utd, Sofapaka, Oserian e.t.c.
 
Kwa hiyo mkenya wewe ni jobless
Hahaha. Mimi si jobless. Niligundua Jamii forums mwaka wa 2014 nilipokuwa namalizia university. Nilikuwa nashinda online ndio nikakutana na jamii forums. Nilikuwa nasoma akina Annael, Geza ulole, Mk254 na wengine bila kufungua account. Niliamua kujoin 2017. Kabla ya hapo nilikuwa twitter na facebook, Wakenya wengi wako huko, nenda huko utawapata. Nilipata scholarship yangu pia nikichokora internet, mimi utanipata online kila wakati inapowezekana.
 
Kweli kabisa Kagame anawacha alama Africa. Rwanda kanchi kadogo sana na hakana madini wala mafuta lakini wanajenga infrastructure kubwa kubwa hadi mtu anajiuliza pesa inatoka wapi. Huo ndio uongozi bora
Report iliyotoka majuzi inaonesha Rw inaongoza kwa kutumia vizuri pesa za ndani barani Africa ikifuatiwa na Tz. Ila Kagame amefanikiwa sana kuwavutia wawekezaji. Kwa udogo wake Rwanda imekua ina attract FDI kubwa kuliko Kenya kwa miaka takribani zaidi ya mitatu iliyopita. Swali la kujiuliza Rwanda inawezaje kufanya PPP kwenye infustructure projects kubwa wakati kaka zake wanashindwa? Je sheria yao ikoje? Angalia jinsi Nai-Msa express way inavyo pigwa kalenda kwa majadiliano yasiyo kwisha. Mwanzo ilibidi iwe PPP sasa nasikia ni mkopo! Huku Tz sheria ya PPP ili badilishwa majuzi (imekua ya kizalendo zaidi) ila bado haijaleta matunda. Kuna shule Kagame anatupa.
 
Ila sisi Kenya na Tanzania tuna kiburi. Hatuwezi enda kumpigia Kagame magoti ili atujuze siri iko wapi. Sisi tutampuuzilia mbali tu kama wazimu aliye na kichaa maana hatutaki kuonekana wanyonge mbele ya kanchi kadogo size ya Nairobi.
 
What uchungu! Tunaelezana facts!
Hio Sigiri bridge ndio ulitegemea kutumia kuingia Kenya Kutoka Tanzania lakini ilipovunjika sasa huna njia nyingine ya kuingia Kenya. Hio ndio maana una machungu sana
 
Sio kweli mnajaza uwanja kwenye michuano yote, huwa mnafanya wakati kuna mtani jembe, mechi ya Simba vs Yanga.
Kenya pia hujaza ikitokea Gor vs AFC.
simba day na siku ya wananchi pia uwanja wa taifa huwa unajaa sana.

kumbuka hizo ni events ambazo zinakuwa organized na team zenyewe, hazihusiani na tournament yoyote.

sasa lini gormahia au afc imewahi ku organise event halafu uwanja ukajaa?.

simba day[emoji116][emoji116][emoji116]

siku ya wananchi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…