Kenya: Wizara ya afya imeanza kupambana na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana na ambao umeathiri zaidi ya watu 200

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wizara ya afya nchini Kenya imesema ipo mbioni kupambana na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana na ambao umeathiri zaidi ya watu 200 katika vijiji vitatu vya jimbo la Kisii eneo la Nyanza Magharibi ya Kenya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anayehusika na afya ya umma Mary Muthoni anasema tayari maafisa wa serikali kwa ushirikiano na serikali ya jimbo la Kisii tayari wamefika maeneo yaliyoathiriwa kuchukua sampuli za vipimo zitakazofanyiwa uchunguzi chanzo cha maradhi hayo.

Amesema matokeo ya uchunguzi wa maabara yatatolewa kesho Jumanne. Dalili za ugonjwa huo usiojulikana ni pamoja na kuhara damu, kutapika, homa kali na maumivu makali ya kichwa.

Wakaazi walioathiriwa ni wa vijiji vya Nyamarondo, Nyarigiro, Nyabigege vinavyopatikana eneo la Mugirango Kusini.

Vituo vya afya eneo hilo tayari vimeripoti kushindwa kudhibiti idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kutafuta matibabu ya ugonjwa huo ulioripotiwa kwa mara ya kwanza eneo hilo karibu wiki tatu zilizopita.

Hivi sasa idadi kubwa ya wagonjwa imelazimisha wengi kutumia kitanda kimoja na baadhi yao wamepelekwa jimbo jirani la Migori kwa matibabu.

Chanzo: DW
 
Wakenya wakiona ni ugonjwa mbaya, watazusha kuwa ugonjwa huo umetokea Tanzania.
 
Back
Top Bottom