Kenya: Wosia wa bilionea Tob Cohen wawekwa hadharani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
NAIROBI,KENYA.


Wosia ulioachwa na bilionea Tob Cohen umewekwa hadharani mbele ya familia yake.

Wosia huo ulifunguliwa jana Ijumaa Septemba 20 mbele ya wanafamilia na marafiki wa bilionea huyo jijini Nairobi.

Hata hivyo, mke wa mfanyabishara huyo, Sarah Wairimu ambaye kwa sasa anashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mumuwe kupitia wakili wake alikataa kuutambua wosia huo na kusema kuwa ni batili.

Aprili mwaka huu Sarah na bilionea Cohen walifungua kedi ya talaka ambako hata hivyo, haikuamuriwa mpaka mfanyabishara huyo alipopoteza maisha.

Mapema jana asubuhi wakili wa mfanyabishara huyo, Chege Kirundi, ambaye ndiyo msimamizi wa wosia huo aliwaambia waandishi wa habari kwamba yaliyomo katika wosia huo yatabaki ya binafsi isipokuwa kama familia ya Cohen itaagiza vingine.

"Hatutajadili maelezo yoyote yaliyomo kwenye wasioa huo kwa wakati huu,” alisisitiza wakili Kirundi na kuongeza kuwa wosia huo utasomwa wakati suala hili litakapofika mahakamani kwa ajili ya kusikilizajwa

Kwa upande wake wakili Cliff Ombeta, anayemwakilisha dada wa bilionea huyo, Gabrielle Van Straten alisema mawakili wa Sarah walialikwa kwenye hafla hiyo lakini walikataa kwa maelekezo kutoka kwa mteja wao.

"Tulimwalika Sarah lakini hajafika. Tumewasubiri kwa muda mrefu lakini hawajafika wala hawakutuma mwakilishi,” alisisitiza wakili huyo.

Hata hivyo, familia ya mfanyabishara huyo akiwamo kaka yake Bernard waligoma kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa zaidi za wosia huo.

Marehemu Cohen imeacha kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti za benki, hisa katika kampuni mbalimbali na mali isiyohamishika.

Credit : Mwananchi
 
Huyo mwanamke atakua kaachiwa hela ya mboga tu
 
Wakati Jana ulisomwa wosia wa mzungu Tob Cohen aliyegundulika kuuwawa katika makazi yake huko Nairobi, Kenya wosia huo haukumpa hata senti moja mkewe raia wa Kenya
Sarah Wairimu ambaye walifunga ndoa mwaka 2007 na ambaye mtuhumiwa wa kwanza katika mauaji hayo.

Ni bayana kwamba marehemu Tob Cohen hakumwachia Sarah Wairimu urithi wowote.

Katika wasia wa Tob, jumba la kiwango cha hela Milioni 400 limeachiwa dadake Gabrielle Van Straten na watoto wake.

Kwa mujibu wa stakabadhi hizo, asilimia 50 ya maskani alipoishi itakwenda kwa dadake.


Asilimia 25 kwa watoto wa dadake wawili.

Na asilimia 25 iliyosalia kwa kakake Bernard Cohen.

Chanzo cha karibu na familia ya Tob Cohen kimeripoti kuwa marehemu alikuwa na Milioni 150 katika akaunti 2 za benki tofauti.

Akaunti moja ina kiwango cha hela Milioni 100 na nyingine Milioni 50.

Kitita hiki cha Milioni 150 kitagawanywa kati ya Gabrielle na Benard huku watoto pia wakipata mgao wa kuridhisha.

Huu wosia ni kinyume na ule watajiri marehemu mzee Mengi ambao uliacha ukwasi wa kutosha kwa mjane Jackline.

Nasaha yangu kwa Dada zangu gold diggers msipende kuwavamia wazee wa kuzungu mkadhani ni sawa na hawa wazee wetu. Mzungu hana huruma hata kidogo linapokuja suala la Mali, na wako very sensitive kujua kama umefuata mapenzi au pesa atakutumia finally Mali watarithi hata wapwa zake mjapo mnasemaga kwa mjomba hakuna urithi.
 
Kama mke alikuwa anakupiga na kila aina ya mateso, unamwachia ili iweje? Uzuri wenzetu wanajiendea kwa wosia, mke au yeyote aliyemuua walifikiri wamemuwahi.
 
Sometimes ni ngumu kufahamu kama mtu ana upendo wa kweli ama ana-act....nafikiri ndio kilichomkuta bwana Mengi(kama wosia ulioonekana ni wa kweli)
Heri ya huyo mzungu aliyeweza kutambua,Mengi hakujua

R.I.P Mzungu mzee
 
Inawezekana mpaka anamuua alishazichota za kutosha.
 
Sometimes ni ngumu kufahamu kama mtu ana upendo wa kweli ama ana-act....nafikiri ndio kilichomkuta bwana Mengi(kama wosia ulioonekana ni wa kweli)
Heri ya huyo mzungu aliyeweza kutambua,Mengi hakujua

R.I.P Mzungu mzee
Ni kweli ila nafikiri wazungu wapo smart sana kung'amua mbivu na mbichi. Mzungu ameuwawa tayari alikuwa yuko katika process za kumdivorce Sarah.
 
Na sheria inasemaje kuhusu mke kutopewa mali ya urithi, inawezekana kuishi na mtu kwa miaka zaidi ya kumi na usipate chochote, na mlifunga ndoa?
 
Kuna wanawake wengi wa kitanzania wanashobokea sana mabeberu weupe wakija kutalii huku, nadhani hii inawahusu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…