Wakati Jana ulisomwa wosia wa mzungu Tob Cohen aliyegundulika kuuwawa katika makazi yake huko Nairobi, Kenya wosia huo haukumpa hata senti moja mkewe raia wa Kenya
Sarah Wairimu ambaye walifunga ndoa mwaka 2007 na ambaye mtuhumiwa wa kwanza katika mauaji hayo.
Ni bayana kwamba marehemu Tob Cohen hakumwachia Sarah Wairimu urithi wowote.
Katika wasia wa Tob, jumba la kiwango cha hela Milioni 400 limeachiwa dadake Gabrielle Van Straten na watoto wake.
Kwa mujibu wa stakabadhi hizo, asilimia 50 ya maskani alipoishi itakwenda kwa dadake.
Asilimia 25 kwa watoto wa dadake wawili.
Na asilimia 25 iliyosalia kwa kakake Bernard Cohen.
Chanzo cha karibu na familia ya Tob Cohen kimeripoti kuwa marehemu alikuwa na Milioni 150 katika akaunti 2 za benki tofauti.
Akaunti moja ina kiwango cha hela Milioni 100 na nyingine Milioni 50.
Kitita hiki cha Milioni 150 kitagawanywa kati ya Gabrielle na Benard huku watoto pia wakipata mgao wa kuridhisha.
Huu wosia ni kinyume na ule watajiri marehemu mzee Mengi ambao uliacha ukwasi wa kutosha kwa mjane Jackline.
Nasaha yangu kwa Dada zangu gold diggers msipende kuwavamia wazee wa kuzungu mkadhani ni sawa na hawa wazee wetu. Mzungu hana huruma hata kidogo linapokuja suala la Mali, na wako very sensitive kujua kama umefuata mapenzi au pesa atakutumia finally Mali watarithi hata wapwa zake mjapo mnasemaga kwa mjomba hakuna urithi.