Kenya yaanza kulegea, yaruhusu Precision Air kuingia Kenya. Je, inatosha kuiridhisha Tanzania?

Kenya yaanza kulegea, yaruhusu Precision Air kuingia Kenya. Je, inatosha kuiridhisha Tanzania?

Wewe jaribu kuwaelewa wakenya, hiyo walibadilisha baada ya Tanzania kuzuia KQ zisije Tanzania, orodha waliyotoa inahusu nchi ambazo ndege zao zitaruhusiwa kuingia Kenya, walipoona tumezuia KQ ndio wajabadilisha maneno kama kawaida yao, soma "heading" ya ile list waliyotoa
U communist hautatufikisha popote. Kama ambavyo u communist haujaitoa nchi yoyote mrisi duniani, zaidi ya uzalendo uchwara.
 
tatizo tanzania ni wastaaarabu sana na wanahuruma, sometimes wanatakiwa kujitoa ufahamu na kukaushia kabisa hiyo issue, ili kama hasara ijulikane imekula hasara upande wa kenya. wasiruhusu kijinga jinga kuchezewa na majirani. Wasiruhusu kitu kuingia hadi uchaguzi uishe tupate rais wetu mpya yeye ndio aamue kufungua au kukaushia hiyo issue
 
Even KQ is a Kenyan airline but it pays parking fees at our airports. For Tanzanians, you have to remain in your country. Precision will be carrying South Africans and Zimbabweans
Mnatapa tapa Mara hili Mara lile ,Tanzania tuna msimamo hatufanyi mambo ya kukurupuka ni kwamba bila ya Kenya tunasonga mbele ni muda utasema .
 
Kenya is busy with your money, you have to know that Precision air will have to pay parking fees in all the Kenyan airports that it will land in. All those money will be taken by KAA. And then also remember that KQ owns 41% of that airline so it is more of a KQ.
Hakuna chochote wanajaribu kufurukuta baada ya kuona hasara wanayopata haina mfano baada ya kufungiwa mashirika matatu wiliyokua wanalingia wamekaa kuumiza vichwa tutaingiaje TZ wakaona watumie shirika la huku wanajua halitafungiwa sasa ngoja dawa yenu inachemka mpaka maji muite mma
 
Najua sayansi ya COVID-19 yote isipokuwa ile ya kupima mbuzi na papai.
Dah....kama mnyarwanda na mtanzania watasafiri kwa ndege moja...kutoka Dar hadi Nairobi...kisha mtanzania unamuweka karantini kwa 2 weeks....basi sisiti kukuita mpumbavu [emoji2960]
 
Wakenya wana majority share kwenye hilo shirika ndiyo maana wanalirusu kuingia huko lakini issue ni hao abiria wataingia Kenya bila kuwekwa kwenye karantini?? Au ni danganya toto tu!
KQ ina 41% ndani ya PW!
 
Dah....kama mnyarwanda na mtanzania watasafiri kwa ndege moja...kutoka Dar hadi Nairobi...kisha mtanzania unamuweka karantini kwa 2 weeks....basi sisiti kukuita mpumbavu [emoji2960]
mnyarwanda akatoa negative covid 19 certificate tutaiamini kwa kuwa wale wapo serious na hili janga na hawana la kuficha ila nyinyi hadi mnaeza forge certificate kwaivo kaeni kwenu kama hamtaki kupimwa na kuwekwa karantini, mmekaribishwa tena tukimalizana na hili janga
 
Kenya haitafuta haki za usafiri za kampuni ya ndege yenye makao yake Tanzania Precision Air ambayo itaanza safari zake kuelekea Jijini Nairobi siku ya Alhamisi licha ya mgogoro uliopo ambao umeilazimu Dar es Salaam kusitisha kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuelekea nchini humo kulingana na gazeti la Business Daily.

''Precision Air ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika kufuatia mgogoro na Tanzania ''

Kenya haitafuta haki za usafiri za kampuni ya ndege yenye makao yake Tanzania Precision Air ambayo itaanza safari zake kuelekea Jijini Nairobi siku ya Alhamisi licha ya mgogoro uliopo ambao umeilazimu Dar es Salaam kusitisha kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuelekea nchini humo, kulingana na gazeti la Business Daily.

Gazeti hilo limemnukuu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya safari za ndege nchini Kenya KCAA Gilbert Kibe akisema kwamba kampuni ya ndege ya Precision ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika kufuatia mgogoro uliopo kati ya Kenya na Tanzania.

Kampuni ya Kenya Airways ambayo ilikuwa na haki zake za usafiri kuelekea Tanzania mwanzo wa mwezi huu wakati kampuni hiyo ya ndege ilipoendelea na safari zake za kimataifa, imezuiwa na mamlaka ya Tanzania kuingia nchini humo kama hatua ya ili kulipa kisasi baada ya Kenya kutoiorodhesha Dar es Salaam katika orodha ya mataifa yalio salama.

''Kampuni ya ndege ya Precision ina haki zilizopo na ninachofahamu ni kwamba haitazuiwa kutua Kenya'', alisema bwana Kibe akizungmza na gazeti la Business Daily.

Bwana Kibe alinukuliwa akisema kwamba anaendelea kufanya majadiliano na wenzake wa Tanzania ili kuondoa masharti yaliowekwa na Tanzania .

Tanzania ilizipiga marufuku kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuingia nchini humo kama hatua ya kulipiza kisasi vita vya kibiashara ambavyo vimekuwepo kati ya mataifa hayo kuhusu usimamizi wa mlipuko wa virusi vya corona.

Unaweza pia kutazama:

Hatua hiyo iliochukuliwa na Tanzania inajiri baada ya Nairobi , kwa mara ya pili mfululizo, kuiweka Tanzania miongoni mwa mataifa ambayo sio salama na virusi vya corona.

Hatua hiyo ina maana kwamba wasafiri kutoka Tanzania wataendelea kukabiliwa na masharti ya lazima ya kuwekwa katika karantini kwa wiki mbili wanapowasili Kenya ili kuzuia maambukizi ya maradhi hayo.

Wasafiri kutoka mataifa 130, hatahivyo wako huru kuingia nchini Kenya bila masharti yoyote kufuatia hatua ya pili ambapo serikali iliongeza mataifa mengine 90 katika orodha yake ya mataifa yanayostahili kuingia nchini humo.

Hatua hiyo ilikasirisha mamlaka nchini Tanzania ambayo wiki iliopita ilijibu kwa kuzifungia kampuni tatu za ndege ikiwemo, Airkenya Express, Fly540 na Safarilink Aviation kutosafiri katika maeneo yoyote nchini Tanzania.

"Sababu ya uamuzi wa kufungia kampuni tatu za ndege kutoka Kenya ni mgogoro uliopo kati ya mataifa haya mawili, Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya safari za ndege nchini Tanzania TCAA Hamza Johari alithibitisha katika mahojiano na gazeti la Business Daily mjini Dar es Salaam.

''Baadhi ya mataifa yanaruhusiwa kuingia Kenya bila masharti kama hayo licha ya kwamba yana viwango vya juu vya maambukizi ya Covid-19'', alisema bwana Johari.

Kenya na Tanzania katika kipindi cha miaka minne zimekuwa zikizozana kuhusu visa, kodi na haki ya kuingia katika soka kwa biadha kama vile sukari na maziwa.

Hatua hiyo imeathiri biashara kati ya mataifa hayo mawili, na kusabavisha misururu ya mikutano ikiwemo mkutano wa Arusha kutoka mwezi Novemba 12-16 mwaka uliopita ili kujaribu kuimarisha uhusiano .

Afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Kenya Airways Allan Kilavuka alisema kwamba njia ya kuelekea Tanzania inasalia kuwa muhimu kutokana na idadi ya wateja inaowaleta Kenya kwa safari nynegine za kimataifa kwa kutumia ndege za kampuni hiyo.

Tunatumai kwamba tatizo hili litatatuliwa haraka iwezekanavyo , alisema bwana Kilavuka.

Kenya kuiruhusu kampuni ya ndege kutoka Tanzania kuingia nchini humo
MY TAKE: [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tutaheshimiana tu
 
mnyarwanda akatoa negative covid 19 certificate tutaiamini kwa kuwa wale wapo serious na hili janga na hawana la kuficha ila nyinyi hadi mnaeza forge certificate kwaivo kaeni kwenu kama hamtaki kupimwa na kuwekwa karantini, mmekaribishwa tena tukimalizana na hili janga
Dah...kama mnyarwanda katokea Dar. ndiyo maana naita upumbavu...kwa mujibu wa sayansi ya COVID-19 [emoji2960]
 
Acheni porojo . Tangu mwanzo Kenya walisema hawajazuia ndege zetu. Isipikuwa karantini ni lazima.
Soma hii habari toka katika gazeti la Kanya vizuri, utaelewa kwamba Kenya walifungia ndege zetu.
Tourism dips amid Kenya, TZ tiff

Hata ukimsikiliza huyo mwenyekiti wa wawekezaji katika sekta ya utalii anavyosema kwamba "Kenya tumewakosea sana wenzetu, haiwezikani sisi twende kwao lakini wao wasije kwetu", hilo ndio lilikua lengo lao, walibadilisha maneno baada ya kuizuia KQ kuja Tanzania
 
KQ ina 41% ndani ya PW!
Sasa hapa ndo tujue kama wakenya hawana akili kuanzia viongozi wao mpaka kibera wametegwa kidogo wametegega , maana yake walikuwa chuki yao wanaificha ficha sasa ipo wazi kumbe ishu sio Corona kama Corona inamana abiria wakipanda ndege ambayo wao wana yao korona haiambukizi ? Wanazidi kujivua nguo mi naomba viongo TZ wasiwape mgongo waendelee kukaza hiyo nati mpaka kwenye hili shirika mpaka wakose pakutokea maana hawa [emoji205] toka zaman walikua wanatumia mwianya yetu kama hii kujifaidisha
 
Tupo Busy nayetu
Hao wapuuzi Waache wapige ngoma na kuyakata wenyewe
 
Hawa hapa wameanza kujipendekeza..




MY TAKE
Trick za kitoto sana...Our demands r pretty simple!
  1. No Air tanzania to Kenya's Nairobi, Mombasa, Eldoret and Kisumu no any airline from Kunyaland to be allowed to land in Tanzania!
  2. No free movement of tanzanians in Kunyaland no any airline from Kunyaland is to be allowed to land in Tanzania


nomasana, sam999, NairobiWalker, hbuyosh, msemakweli, simplemind, Kimweri, Bulldog, MK254, Kafrican, Ngongo, Ab_Titchaz, mtanganyika mpya, JokaKuu, Ngongo, Askari Kanzu, Dhuks, Yule-Msee, waltham, Mzee, mombasite gabriel, Juakali1980, Boda254, mwaswast, MwendaOmo, Iconoclastes, oneflash, Kambalanick, 1 Africa, saadeque, burukenge, nyangau mkenya, Teen-Upperhill Nairobi, kadoda11
 
Back
Top Bottom