Kenya yachelewesha marejesho ya Mkopo wa SGR, yapigwa faini na China, Tsh. Bilioni 34

Kenya yachelewesha marejesho ya Mkopo wa SGR, yapigwa faini na China, Tsh. Bilioni 34

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Wakenya watalazimika kulipa zaidi ya KSh 1.7 Bilioni kama faini kwa kuchelewesha kulipa mkopo wa reli ya SGR kutoka kwa Benki ya Exim ya China katika mwaka wa fedha wa 2023/24.

Hii ni kutokana na mkopo wa KSh 167.5 Bilioni ambao Shirika la Kenya Railways limeshindwa kulipa, ukichukua asilimia 62 ya jumla ya mikopo inayodaiwa mashirika ya serikali.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Usimamizi wa Deni ya Hazina ya Taifa ya 2023/24, mkopo huu ambao haujalipwa unatozwa faini ya asilimia 1 ya kiasi kinachodaiwa.

Hii inamaanisha kuwa Kenya italipa faini ya KSh 1.68 bilioni. Ripoti hiyo imeeleza kuwa mkopo huo wa SGR, ambao ulitarajiwa kulipwa kupitia mapato ya reli hiyo tangu 2020, sasa mzigo wake umeangukia serikali kuu kwa sababu mapato ya SGR hayatoshi.

Mikopo ya reli ya SGR inayodaiwa Kenya Railways Corporation imefikia KSh 737.5 bilioni, ikiwa ni asilimia 61 ya jumla ya mikopo ambayo serikali imewakopesha mashirika. Jumla ya deni la SGR limeongezeka kwa asilimia 36.8, kutoka KSh 539 bilioni hadi KSh 737.5 bilioni kutokana na faini hiyo pamoja na ongezeko la thamani ya dola.

Kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya dola, malipo ya mkopo wa SGR yaliongezeka kwa KSh 14 bilioni mnamo Januari 2024.

Benki ya Dunia imeripoti kuwa Kenya inatarajiwa kulipa $536.9 milioni (KSh 84.7 bilioni) mwaka huu, ikilinganishwa na KSh 70.2 bilioni zilizolipwa mwaka uliopita kwa kipindi kama hicho.

.........

SGR Loan: Kenyan Taxpayers to Pay Over KSh 1.7b in Penalties for Defaulted Chinese Debt

Kenya defaulted on the Standard Gauge Railway (SGR) loan payment to the China Exim Bank in the financial year 2023/2024

Data from the National Treasury indicated that Kenya Railways failed to pay KSh 167.5 billion, accounting for 62% of the total loan owed by state agencies

Treasury said the defaulted loan attracts a fine of 1% of the unpaid amount, which accounts KSh 1.68 billion in penalties

Kenyans will be forced to pay over KSh 1.7 billion in penalties for the defaulted Standard Gauge Railway (SGR) loan to China Exim Bank.

The National Treasury reported that Kenya Railways failed to pay KSh 167.5 billion owed to the Chinese lender in the financial year 2023/24.

What's the penalty for defaulting SGR loan?

According to the Treasury Annual Debt Management Report 2023/24, the defaulted SGR loan accounts for 62% of the KSh 266.5 billion loan owed by state agencies.

The report indicated that loan defaults attract a fine of 1% of the unpaid amount, which amounts to KSh 1.68 billion in penalties.

"The SGR loan accrued and not paid in FY 2023/2024 amounted to KSh 167.5 billion," read the report in part, as quoted by Business Daily.

What's the total SGR loan?

This attracted a 1% penalty, which increased the total SGR loan by 36.8% to KSh 737.5 billion, up from the KSh 539 billion issued by China Exim Bank.

The SGR line, which runs from Mombasa to Naivasha, was expected to start serving the loan in 2020 from its revenue, however, the burden has since been shifted to the exchequer.

"SGR loans to Kenya Railways Corporation amount to Sh737.5 billion, which accounted for 61% of the total on-lent loans," Treasury revealed.

How SGR loan increases

Due to the weakening shilling, the Standard Gauge Railway (SGR) loan repayment increased by KSh 14 billion in January 2024.

The World Bank reported that Kenya is scheduled to pay $536.9 million (KSh 84.7 billion), compared to KSh 70.2 billion paid during a similar period in 2023.

This followed a further decline in the shilling's value against the US dollar, which is currently at KSh 157 per dollar

Chanzo: Business Daily
 
Wakenya watalazimika kulipa zaidi ya KSh 1.7 Bilioni kama faini kwa kuchelewesha kulipa mkopo wa reli ya SGR kutoka kwa Benki ya Exim ya China katika mwaka wa fedha wa 2023/24.

Hii ni kutokana na mkopo wa KSh 167.5 Bilioni ambao Shirika la Kenya Railways limeshindwa kulipa, ukichukua asilimia 62 ya jumla ya mikopo inayodaiwa mashirika ya serikali.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Usimamizi wa Deni ya Hazina ya Taifa ya 2023/24, mkopo huu ambao haujalipwa unatozwa faini ya asilimia 1 ya kiasi kinachodaiwa.

Hii inamaanisha kuwa Kenya italipa faini ya KSh 1.68 bilioni. Ripoti hiyo imeeleza kuwa mkopo huo wa SGR, ambao ulitarajiwa kulipwa kupitia mapato ya reli hiyo tangu 2020, sasa mzigo wake umeangukia serikali kuu kwa sababu mapato ya SGR hayatoshi.

Mikopo ya reli ya SGR inayodaiwa Kenya Railways Corporation imefikia KSh 737.5 bilioni, ikiwa ni asilimia 61 ya jumla ya mikopo ambayo serikali imewakopesha mashirika. Jumla ya deni la SGR limeongezeka kwa asilimia 36.8, kutoka KSh 539 bilioni hadi KSh 737.5 bilioni kutokana na faini hiyo pamoja na ongezeko la thamani ya dola.

Kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya dola, malipo ya mkopo wa SGR yaliongezeka kwa KSh 14 bilioni mnamo Januari 2024.

Benki ya Dunia imeripoti kuwa Kenya inatarajiwa kulipa $536.9 milioni (KSh 84.7 bilioni) mwaka huu, ikilinganishwa na KSh 70.2 bilioni zilizolipwa mwaka uliopita kwa kipindi kama hicho.

Chanzo: Business Daily
CC: Saa100 TZ
 
Back
Top Bottom