joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kwamba, mwanzoni wa huu ugonjwa nilisema Tanzania ni mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya Corona.
Tanzania ni nchi ya kwanza hapa Africa kufungua uchumi wake na kuruhusu safari za ndege kuanza kuingia na kutoka. Tanzania haikuwahi kufunga mipaka yake zaidi ya kusimamisha safari za ndege za abiria.
Tanzania imeamua kufungua mipaka yake baada ya kujiridhisha kwamba wagonjwa wa Covid nchini wamepingua hivyo shughuli za usafiri zinaweza kuendelea.
Kenya imeendelea kutangaza wagonjwa kila siku, na idadi ya wagonjwa imekua ikiongezeka kwa kasi sana, jambo la kushangaza ni Kenya kuamua kufungua anga na kuruhusu ndege za abiria kuanza kuingia na kutoka, wakati ambapo Nairobi ipo chini ya vikwazo vya kutoka na kuingia jijini humo.
Katika account yake ya twitter, rais Uhuru Kenyatta Jana alisema kwamba kutokana na idadi kubwa ya maambukizi, Jiji la Nairobi litaendelea kuwa chini ya karantini kwa muda mrefu zaidi. Swali la kujiuliza, kama Nairobi itaendelea kuwa na karantini hakuna watu wanaoruhusiwa kuingia na kutoka, hizo ndege za abiria zitatua uwanja gani kama sio JKIA?.
Kweli Kenya ilistahili kuanza kuruhusu ndege za abiria, au imeamua kufanya hivyo ili kushindana na Tanzania, lengo ni kuhakikisha watalii wasitembelee Tanzania pekee?
Source: Kenya Airways To Resume Passenger Operations In June