Kama bandari ya Bagamoyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia konteina 500 kwa saa, kwa muda wa saa 12 watahudumia kontainer 6000 ambazo ni sawa na tani 120,000 (assuming 20ton weight for one container).
Tutakuwa na uwezo wa kusafirisha tani 120,000 kwa siku ukichukulia kwamba sasa kwa reli hivi tunasafirisha tani pungufu ya 500,000?!
sidhan kama DRC na burundi wanaweza pitisha mizigo yao kupitia mombasa!!!! ila its a good move ktk kuondoa ubabaushaj kwa kua na office huko!!!
Burundi zambia congo wataendelea kuwa wateja wetu wanahangaika na ujio wa bagamoyo port,
kama kawaida tutaendelea kuiita Rwanda 'mkoa' na dharau zingine huku tukisahau kuwa Kigali huenda ndio ikawa hub ya Kisangani, North Kivu, Bukavu nk. Vita inayoendelea huko ni swala la muda mfupi sana tu na punde hawa jamaa watafurahia maisha.
kusema kweli, nilisikia taarifa ile jana, wanasema wanataka kutageti usafirishaji kupitia bandari ya Mombasa kwa mizigo ya uganda,Rwanda, burundi na DRC. Tz wametuachia Zambia peke yake, malawi nayo mara nyingi inapitishia mizigo yake mozambique na south africa. utakuja kuona kuwa, hata vizuizi vingi ambavyo kenya wameondoa barabarani, hapa tz tunavyo vingi mno hadi unapokuwa unasafiri unapoteza muda mwingi. ukianza kusafiri mfano toka hapa dsm kwenda mwanza, kwenye weigh bridge utakuta mafoleni, kuanizia tu hapo kibaha, nenda chalinze, nenda moro, nenda dodoma, singida, Tinde shindayanga na ile ya mwisho kuingilia mwanza....balaa tupu, muda mwingi unapotea. kama issue ni kuwa makini katika ugaguzi na kudhibiti ukwepaji wa kodi au uzidishaji uzito wa mizigo, wangetafuta njia nyingine ya kisasa mbadala ambayo nchi zingine duniani wanazitumia na kuwa successiful bila kupoteza muda kiasi kile. Mwakyembe please, tusaidiane kupambana na hao jamaa katika competition. nafikiri wameamsa zaidi baada ya kusikia fununu kuwa bagamoyo itajengwa bandari itakayowafunika kabisa wale mombasa. Mungu ibariki Tanzania.
Moja ya sababu inayotufanya tuendelee kuwa maskini ni hili la akili yetu kuiegemeza kwa wanasiasa....na ajabu ya mwaka unaweza kuta hata decision makers wa TPA nao wanatoa comment kama zako za kumhoji Mwakyembe!!
Bandari ni Mamlaka kamili yenye wataalamu na watendaji wa aina mbalimbali na wala sio Mwakyembe! Hawa ndio wanaotakiwa kuwa creative na kupeleka Propasal serikalini....hapo ndipo inapofuata role ya akina Mwakyembe! Pale bandarini kuna watu waliosoma Ports Management, Transport Management, Investment, Planning na mambo mengine kedekede! Pale kuna Directorate of Planning and Investment; hawa ndio wanaotakiwa ku-explore different opportunities available kisha kupeleka proposal zao kwa akina Mwakyeme! Tusizani safari zote za akina Obama kuja Afrika zinakuwa initiated serikalini, la hasha....zingine zinakuwa initiated na government institutions na hata wafanyabiashara!! Kwa hapa Tanzania, taasisi za serikali kama TPA ndio wanaotakiwa ku-explore hizi opportunities na kisha kupeleka proposal serikalini.....huko zikataliwe ndipo tuje kuwahoji akina Mwakyembe! Siamini mtu kama Mwakyembe anaweza kuikataa productive project....
Kinachokera ni hii kauli Maarufu ya kwamba "tumefanya tathimini na upembuzi yakinifu na hela ziko tayari tunasubiri Utekelezaji tu.
kenya are trying to win back wateja waliowapoteza mombasa na kuhamia tanzania in the past 18 months, lakini kuwin wateja si kufungua office tu kigali au kampala au bujumbura au bukavu au goma au lumbumbashi, tanzania wanamalizia kujenga vituo vya pamoja mpakani(one stop border posts) kwenye mipaka yake na nchi jirani, pia wanakaribia kuanza kujenga vituo vya ukaguzi vya pamoja njiani (one stop inspection stations) kwa ajili ya magari ya transit kwa lengo la kuyapunguzia muda wa safari kutoka bandari ya dar kwenda nchi husika, mipaka inayonufaika mpaka sasa ni rusumo(na rwanda), mutukula(na uganda), kabanga(na burundi), tunduma/makonde(zambia). namanga(kenya), horiri/taveta(kenya) lengo ni kutumia masaa 48 tu kutoka bandarini kwenda nchi husika, then hizo office zitafunguliwa kwa sasa kinachofanyika ni Dar port marketing stategy kwa wateja wa nje ya nchi, na wiki tatu zilizopita tanzania wamezindua system ya kusaidia kupunguza vikwazo na kutambua wakwamishaji wa usafirishaji kati ya bandari/ticts/weigh bridges/police/immigration na clearing agents.........
Kinachokera ni hii kauli Maarufu ya kwamba "tumefanya tathimini na upembuzi yakinifu na hela ziko tayari tunasubiri Utekelezaji tu.
Replacement ya TUko mbioni!!
View attachment 103724
BANDARI YA MOMBASA KENYA WAMEFUNGUA OFFICE KIGALI-MWAYKEMBE SISI TUMEJIPANGAJE?
Kufuatia kikao cha triple K (Kenyatta, Kagame na Kaguta (Mseveni)) kilichofanyika Kampala mwezi uliopita, jana bandari ya Mombasa wamefungua rasmi ofisi yao Kigali kwa ajili ya kuhudumia nchi za Rwanda, Burundi na DRC.
Moja ya mambo waliyokubaliana triple K ni kuondoa matatizo yote yanayofanya biashara baina ya nchi hizi kuwa ngumu.
Sote tunafahamu mahusiano mabovu yaliyopo kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kwa sasa. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa Bandari ndio cash cow ya Tanzania, hakuna cha kilimo,madini, utalii au chochoteutakachotaja.
Kama kumbukumbu zangu bado ziko poa, bandari inaingiza over 50 bil kwa mwezi.
Swali ninalojiuliza, hivi tumejipangaje ili kuwa competitive zaidi in case nchi hizi nne kwa maana ya DRC, Burundi, Rwanda na Uganda zitaamua kwa kiasi kikubwa kuanza kutumia bandari ya Mombasa? Think of hayo mapato niliyotaja, ajira, biashara za mafuta, hotel n.k.
Wenzetu wako serious sana linapokuja suala la maendeleo na sio ububaishaji kama sisi
Congrats. You have valid questions.BTW Mombasa port is being expanded into a megaport, one that has the capacity to handle the largest sea faring vessel.On completion, the port's capacity will rise to 1.7 Million TEus by 2015. The country is also planning to build a second railway line from MSa to Kisumu in order to increase speed and ease congestion at the Port. Dar- wamejipangaje?View attachment 103724
BANDARI YA MOMBASA KENYA WAMEFUNGUA OFFICE KIGALI-MWAYKEMBE SISI TUMEJIPANGAJE?
Kufuatia kikao cha triple K (Kenyatta, Kagame na Kaguta (Mseveni)) kilichofanyika Kampala mwezi uliopita, jana bandari ya Mombasa wamefungua rasmi ofisi yao Kigali kwa ajili ya kuhudumia nchi za Rwanda, Burundi na DRC.
Moja ya mambo waliyokubaliana triple K ni kuondoa matatizo yote yanayofanya biashara baina ya nchi hizi kuwa ngumu.
Sote tunafahamu mahusiano mabovu yaliyopo kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kwa sasa. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa Bandari ndio cash cow ya Tanzania, hakuna cha kilimo,madini, utalii au chochoteutakachotaja.
Kama kumbukumbu zangu bado ziko poa, bandari inaingiza over 50 bil kwa mwezi.
Swali ninalojiuliza, hivi tumejipangaje ili kuwa competitive zaidi in case nchi hizi nne kwa maana ya DRC, Burundi, Rwanda na Uganda zitaamua kwa kiasi kikubwa kuanza kutumia bandari ya Mombasa? Think of hayo mapato niliyotaja, ajira, biashara za mafuta, hotel n.k.
issue siyo bandari tuu pia wanajenga standard guage railway itakoyounganisha mombasa,uganda hadi kigali. Mizigo itafika kigali chini ya masaa 24.
Hivi ule urasimu pale dar port umeisha?