Kenya Yafungua Tawi La Bandari Kigali Rwanda

Kenya Yafungua Tawi La Bandari Kigali Rwanda

Kama bandari ya Bagamoyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia konteina 500 kwa saa, kwa muda wa saa 12 watahudumia kontainer 6000 ambazo ni sawa na tani 120,000 (assuming 20ton weight for one container).

Tutakuwa na uwezo wa kusafirisha tani 120,000 kwa siku ukichukulia kwamba sasa kwa reli hivi tunasafirisha tani pungufu ya 500,000?!

umesahau kuwa siyo reli tu na barabara zipo. kwa sasa barbr inatumika sn kuliko reli
 
kenya are trying to win back wateja waliowapoteza mombasa na kuhamia tanzania in the past 18 months, lakini kuwin wateja si kufungua office tu kigali au kampala au bujumbura au bukavu au goma au lumbumbashi, tanzania wanamalizia kujenga vituo vya pamoja mpakani(one stop border posts) kwenye mipaka yake na nchi jirani, pia wanakaribia kuanza kujenga vituo vya ukaguzi vya pamoja njiani (one stop inspection stations) kwa ajili ya magari ya transit kwa lengo la kuyapunguzia muda wa safari kutoka bandari ya dar kwenda nchi husika, mipaka inayonufaika mpaka sasa ni rusumo(na rwanda), mutukula(na uganda), kabanga(na burundi), tunduma/makonde(zambia). namanga(kenya), horiri/taveta(kenya) lengo ni kutumia masaa 48 tu kutoka bandarini kwenda nchi husika, then hizo office zitafunguliwa kwa sasa kinachofanyika ni Dar port marketing stategy kwa wateja wa nje ya nchi, na wiki tatu zilizopita tanzania wamezindua system ya kusaidia kupunguza vikwazo na kutambua wakwamishaji wa usafirishaji kati ya bandari/ticts/weigh bridges/police/immigration na clearing agents.........
 
Tatizo letu ni nini hasa?
Ni kuchelewa kuchukua maamuzi?
Ni kukosa wataalamu? maana humu ndani walisema wasomi wetu hawauziki.
Ni kukosa ushirikiano ndani na nje ya nchi?
Ni upeo wa viongozi kugota?
Ni utaniutani badala ya kufanya kazi?
Ni mfumo mbovu wa ccm na Serikali? (ILANI)

TUCHUKUE HATUA HATA MUNGU ALIWAPIGA CHINI WAFALME VIHIYO NA KUSIMIKA IMARA.
 
sidhan kama DRC na burundi wanaweza pitisha mizigo yao kupitia mombasa!!!! ila its a good move ktk kuondoa ubabaushaj kwa kua na office huko!!!

Burundi zambia congo wataendelea kuwa wateja wetu wanahangaika na ujio wa bagamoyo port,
 
Burundi zambia congo wataendelea kuwa wateja wetu wanahangaika na ujio wa bagamoyo port,

issue siyo bandari tuu pia wanajenga standard guage railway itakoyounganisha mombasa,uganda hadi kigali. Mizigo itafika kigali chini ya masaa 24.
 
kama kawaida tutaendelea kuiita Rwanda 'mkoa' na dharau zingine huku tukisahau kuwa Kigali huenda ndio ikawa hub ya Kisangani, North Kivu, Bukavu nk. Vita inayoendelea huko ni swala la muda mfupi sana tu na punde hawa jamaa watafurahia maisha.

Sijui tupewe miwani ya aina gani ili tuweze kuona fursa tunazopoteza. Na hapo ni suala dogo tu la ukiritimba usio na tija. Pita mizani uone milori iliyoko kwenye foleni, ikisubiri kupima uzito, nenda mipakani milori hiyo hiyo inasubiri kuvuka, documents siku mbili zinakaguliwa. Hapo bandarini wakati wa kutoa mizigo ndio usisome, sijui hata kama zile hesabu za "Queuing theory" zina-apply huko.
 
kusema kweli, nilisikia taarifa ile jana, wanasema wanataka kutageti usafirishaji kupitia bandari ya Mombasa kwa mizigo ya uganda,Rwanda, burundi na DRC. Tz wametuachia Zambia peke yake, malawi nayo mara nyingi inapitishia mizigo yake mozambique na south africa. utakuja kuona kuwa, hata vizuizi vingi ambavyo kenya wameondoa barabarani, hapa tz tunavyo vingi mno hadi unapokuwa unasafiri unapoteza muda mwingi. ukianza kusafiri mfano toka hapa dsm kwenda mwanza, kwenye weigh bridge utakuta mafoleni, kuanizia tu hapo kibaha, nenda chalinze, nenda moro, nenda dodoma, singida, Tinde shindayanga na ile ya mwisho kuingilia mwanza....balaa tupu, muda mwingi unapotea. kama issue ni kuwa makini katika ugaguzi na kudhibiti ukwepaji wa kodi au uzidishaji uzito wa mizigo, wangetafuta njia nyingine ya kisasa mbadala ambayo nchi zingine duniani wanazitumia na kuwa successiful bila kupoteza muda kiasi kile. Mwakyembe please, tusaidiane kupambana na hao jamaa katika competition. nafikiri wameamsa zaidi baada ya kusikia fununu kuwa bagamoyo itajengwa bandari itakayowafunika kabisa wale mombasa. Mungu ibariki Tanzania.

Mkuu hivyo vizuizi vingi unavyoviona ndio vinaongeza mianya ya hawa jamaa kuendelea kula vizuri hiyo hela. Wafanyakazi wengi wa kwenye hizo weighbridge hela nyingi zinaishia mifukoni mwao. Wachunguze uone maendeleo waliyojilimbikizia binafsi. Its a shame
 
Moja ya sababu inayotufanya tuendelee kuwa maskini ni hili la akili yetu kuiegemeza kwa wanasiasa....na ajabu ya mwaka unaweza kuta hata decision makers wa TPA nao wanatoa comment kama zako za kumhoji Mwakyembe!!

Bandari ni Mamlaka kamili yenye wataalamu na watendaji wa aina mbalimbali na wala sio Mwakyembe! Hawa ndio wanaotakiwa kuwa creative na kupeleka Propasal serikalini....hapo ndipo inapofuata role ya akina Mwakyembe! Pale bandarini kuna watu waliosoma Ports Management, Transport Management, Investment, Planning na mambo mengine kedekede! Pale kuna Directorate of Planning and Investment; hawa ndio wanaotakiwa ku-explore different opportunities available kisha kupeleka proposal zao kwa akina Mwakyeme! Tusizani safari zote za akina Obama kuja Afrika zinakuwa initiated serikalini, la hasha....zingine zinakuwa initiated na government institutions na hata wafanyabiashara!! Kwa hapa Tanzania, taasisi za serikali kama TPA ndio wanaotakiwa ku-explore hizi opportunities na kisha kupeleka proposal serikalini.....huko zikataliwe ndipo tuje kuwahoji akina Mwakyembe! Siamini mtu kama Mwakyembe anaweza kuikataa productive project....

Kuita nyeusi ni nyeusi, tatizo kubwa ni hao watu waliosimama kwa hivyo vyeo ulivyotajwa. Labda tu watuhakikishie kuwa walishapeleka proposal ila ziko makabatini zinapigwa feni zenye upepo wa vumbi. Manake tukipita nje ya ofisi za gavumenti kuna makabrasha huwa tunayaona kwenye vioo, sijui ndio hizo proposal!
 
Kinachokera ni hii kauli Maarufu ya kwamba "tumefanya tathimini na upembuzi yakinifu na hela ziko tayari tunasubiri Utekelezaji tu.

Yaani ni wimbo ambao hata uutie vyombo vya aina gani, haunogi tena masikioni!
 
kenya are trying to win back wateja waliowapoteza mombasa na kuhamia tanzania in the past 18 months, lakini kuwin wateja si kufungua office tu kigali au kampala au bujumbura au bukavu au goma au lumbumbashi, tanzania wanamalizia kujenga vituo vya pamoja mpakani(one stop border posts) kwenye mipaka yake na nchi jirani, pia wanakaribia kuanza kujenga vituo vya ukaguzi vya pamoja njiani (one stop inspection stations) kwa ajili ya magari ya transit kwa lengo la kuyapunguzia muda wa safari kutoka bandari ya dar kwenda nchi husika, mipaka inayonufaika mpaka sasa ni rusumo(na rwanda), mutukula(na uganda), kabanga(na burundi), tunduma/makonde(zambia). namanga(kenya), horiri/taveta(kenya) lengo ni kutumia masaa 48 tu kutoka bandarini kwenda nchi husika, then hizo office zitafunguliwa kwa sasa kinachofanyika ni Dar port marketing stategy kwa wateja wa nje ya nchi, na wiki tatu zilizopita tanzania wamezindua system ya kusaidia kupunguza vikwazo na kutambua wakwamishaji wa usafirishaji kati ya bandari/ticts/weigh bridges/police/immigration na clearing agents.........

Nimegonga like mbili lakini zikagoma.

Kinashongaza ni huo uboreshaji wa mipakani wakati pale Bandarini penyewe ni mizengwe A to Z.

I have been a victim there. Kuna ujinga mmoja eti mkaguzi mmoja pale getini you stay there for hours waiting for your car.

grrrrrrrr!!!!!!!!!
 
Wabongo tuache uoga kenya wanajua kua tz tunajenga badar ya kisasa b/moyo so wanachokifanya ni kuimalisha masoko yao la msingi ni kumwomba mungu huo mradi utimie otherwise wakenya imekula kwao..
 
Hayo ni mapatano ya kisiasa yaliyoasisiwa na kagame na museveni kuikomoa tanzania lakini kiuchumi hawawezi kuiepuka bandari ya dar-es-salaam. Wewe subiri tu uhuru akitofautiana na sera zao za kimbari watamtolea nje namiradi yao ya alnacha. Tz inajenga miundombinu yake, watakuja bila kupenda.
 
View attachment 103724

BANDARI YA MOMBASA KENYA WAMEFUNGUA OFFICE KIGALI-MWAYKEMBE SISI TUMEJIPANGAJE?

Kufuatia kikao cha triple K (Kenyatta, Kagame na Kaguta (Mseveni)) kilichofanyika Kampala mwezi uliopita, jana bandari ya Mombasa wamefungua rasmi ofisi yao Kigali kwa ajili ya kuhudumia nchi za Rwanda, Burundi na DRC.

Moja ya mambo waliyokubaliana triple K ni kuondoa matatizo yote yanayofanya biashara baina ya nchi hizi kuwa ngumu.

Sote tunafahamu mahusiano mabovu yaliyopo kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kwa sasa. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa Bandari ndio cash cow ya Tanzania, hakuna cha kilimo,madini, utalii au chochoteutakachotaja.

Kama kumbukumbu zangu bado ziko poa, bandari inaingiza over 50 bil kwa mwezi.

Swali ninalojiuliza, hivi tumejipangaje ili kuwa competitive zaidi in case nchi hizi nne kwa maana ya DRC, Burundi, Rwanda na Uganda zitaamua kwa kiasi kikubwa kuanza kutumia bandari ya Mombasa? Think of hayo mapato niliyotaja, ajira, biashara za mafuta, hotel n.k.

unataka kutwambia kuwa kufungua bandali Kigali ndiyo yatakuwa maendeleo kwa Tanzania nani kakwambia kuwa bandari yetu inategemea pekee mizigo ya Rwanda,uganda na Kenya.
 
Kenya pia wametangaza tenda ya ujenzi wa high speed train railway 500km kutoka Nairobi mpaka Kisumu...

Yatupasa na sisi tuchangamke kufufua reli ya kati na kujenga fasta ile ya Mchuchuma mpaka Mtwara
 
View attachment 103724

BANDARI YA MOMBASA KENYA WAMEFUNGUA OFFICE KIGALI-MWAYKEMBE SISI TUMEJIPANGAJE?

Kufuatia kikao cha triple K (Kenyatta, Kagame na Kaguta (Mseveni)) kilichofanyika Kampala mwezi uliopita, jana bandari ya Mombasa wamefungua rasmi ofisi yao Kigali kwa ajili ya kuhudumia nchi za Rwanda, Burundi na DRC.

Moja ya mambo waliyokubaliana triple K ni kuondoa matatizo yote yanayofanya biashara baina ya nchi hizi kuwa ngumu.

Sote tunafahamu mahusiano mabovu yaliyopo kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kwa sasa. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa Bandari ndio cash cow ya Tanzania, hakuna cha kilimo,madini, utalii au chochoteutakachotaja.

Kama kumbukumbu zangu bado ziko poa, bandari inaingiza over 50 bil kwa mwezi.

Swali ninalojiuliza, hivi tumejipangaje ili kuwa competitive zaidi in case nchi hizi nne kwa maana ya DRC, Burundi, Rwanda na Uganda zitaamua kwa kiasi kikubwa kuanza kutumia bandari ya Mombasa? Think of hayo mapato niliyotaja, ajira, biashara za mafuta, hotel n.k.
Congrats. You have valid questions.BTW Mombasa port is being expanded into a megaport, one that has the capacity to handle the largest sea faring vessel.On completion, the port's capacity will rise to 1.7 Million TEus by 2015. The country is also planning to build a second railway line from MSa to Kisumu in order to increase speed and ease congestion at the Port. Dar- wamejipangaje?
 
issue siyo bandari tuu pia wanajenga standard guage railway itakoyounganisha mombasa,uganda hadi kigali. Mizigo itafika kigali chini ya masaa 24.

Rwanda na kenya wamekuwa na chuki na sisi siku nyingi ila contribution ya rwanda si kubwa kwenye bandari yetu kwahiyo haitutishi sana congo zambia ndiyo wenye contribution kubwa
 
Back
Top Bottom