Kenya yaidhinisha matumizi ya Sindano ya Lenacapavir kama Kinga ya Maambukizi ya VVU

Kenya yaidhinisha matumizi ya Sindano ya Lenacapavir kama Kinga ya Maambukizi ya VVU

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Wizara ya Afya nchini Kenya imeidhinisha kuanza kutumika kwa dawa ya kuzuia maambukizi ya VVU ijulikanayo kama lenacapavir, ambayo hutolewa mara mbili tu kwa mwaka.

Wizara imesema uamuzi huo umetokana na tathmini ya kina ya kisayansi kuhusu ubora, usalama na ufanisi wa dawa hiyo, iliyofanyika kwa kuzingatia sheria za Kenya pamoja na viwango vya kimataifa vya udhibiti wa dawa.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Waziri wa Afya Aden Duale alisema kuwa mfumo wa muda mrefu wa lenacapavir unaorahisisha kutolewa mara mbili kwa mwaka ni mbadala muhimu kwa dawa za kumeza kila siku, hasa kwa watu wanaopata changamoto ya kutumia vidonge kila siku.

Duale amesema Kenya ni miongoni mwa nchi za kwanza barani Afrika kupendekeza lenacapavir kusajiliwa, hatua inayolingana na miongozo ya hivi karibuni ya afya ya umma duniani, ikiwemo mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani.

vaccine.png

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo Kenya iliripoti ongezeko la asilimia 19 ya maambukizi mapya ya VVU mwezi Desemba 2025, huku idadi ya visa ikiongezeka kutoka 16,752 mwaka 2023 hadi 19,991 mwaka 2024, kulingana na taarifa ya Baraza la Taifa la Kudhibiti Magonjwa ya Syndemic.

=================================

The Ministry of Health has approved the rollout of lenacapavir, a twice-yearly HIV prevention drug.

The ministry says the recommendation follows a comprehensive scientific assessment of the quality, safety, and efficacy of lenacapavir, conducted in line with Kenyan law and applicable international regulatory standards.

“Its long-acting formulation allows it to be administered only twice a year, offering an important alternative to daily oral HIV prevention medicines. This is particularly beneficial for individuals who face challenges with taking pills every day,” Health CS Aden Duale says.

Kenya is among the first African countries to recommend lenacapavir for registration, a decision that aligns with recent global public health guidance, including recommendations by the World Health Organization, Duale says.

He adds that the move reflects the country’s growing regulatory capacity and leadership in enabling timely access to innovative health technologies of public health importance. Duale says the ministry will ensure the medicine is introduced in a timely, equitable and responsible manner for populations at substantial risk of HIV infection.

Source: Buzzroom Kenya
 
Wazungu walileta waya ili kutumaliza dawa wanazo.
Huu ugonjwa ulimtoa machozi Mkapa, nakumbuka Mkapa alilia kama mtoto wakati anazindua ARV back in the days 2003.

Gen Z hawawezi kuelewa tunaposema Moto/Umeme/Gridi wanaona tunawaletea mapicha picha tuu.

Moto ulikuwa Moto kweli. Unakufa kilo mbili kwenye kiroba.
 
Kama hukuuona ukimwi wa enzi hizo. Bhasi huujui ukimwi vizuri aseee

Mtu anabaki mifupa, kichwa kimenyolewa nywele zote, midomo kama imebabuka na yale mapele na mabaka ya kwenye ngozi.

Sitosahaua🙌🙌🙌🏾🙌🏾🙌🏾
 
Huu ugonjwa ulimtoa machozi Mkapa, nakumbuka Mkapa alilia kama mtoto wakati anazindua ARV back in the days 2003.
Acha kaka, umepoteza ndugu,jamaa na marafiki na nguvukazi ya dunia kwa ujumla.
Ngoma ya zamani mgonjwa anatengwa kuanzia sehemu ya kulala mpaka vyombo vya chakula, ngoma ya zamani mgonjwa anafichwa ndani watu wasimuone.
 
Acha mkuu, nimeshuhudia mimi mtu anatolewa ndani kuota jua amefungwa kwenye taulo. Amebaki mifupa mitupu na kichwa.

Tumetoka mbali aisee! Tumeona mengi.
 
Wazungu tiba wanayo, wamepanga kumaliza waya 2030. Ila wataleta kitu kingine cha kudhibiti population hasa ya waafrika.
Mkuu unafikiri ni kwanini watake kudhibiti population hasa ya waafrika? ukizingatia waafrika ni asilimia ndogo sana kwa ukiangalia World population kwa mabara.
 
Back
Top Bottom